Mawazo yangu kuhusu ya Mikel Arteta kuwa kocha

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
Kwa mara ya kwanza kwenye historia yake, Arsenal itakua na cheo cha Football director ambae ni Raul Sanllehi *(kabla hajaja Arsenal alikaa miaka 15 kwenye cheo icho Barcelona, engineered Neymar, Suarez, dembele, Coutinho moves and convinced Barcelona to sign Paulinho ambae kila mtu alimkataa ikiwemo Barcelona directors and fans)*

Kwa mara ya kwanza Arsenal ina department ya recruitment na head wake ni Sven Minslintant *(they call him a diamond eye, Kwa kusaidiana na Jurgen Klopp waliifanya ile Dortmund ya 2000-2015 vile ilivyokua)*

Kwa mara ya kwanza kwenye historia yake bodi ya Arsenal imekua na bodi member ambae ana chini ya miaka 40 na mtu wa pili kwenye maamuzi makubwa juu ya klabu Arsenal *(Josh Kroenke, 37)*

Kwa mara ya kwanza Chief executive wa Arsenal Ivan Gazidis atakua na mamlaka ya halisi ya CEO tangu aondoke David Dein 2007, kwa miaka yote hii amekua kwenye kivuli cha Arsene Wenger *(before hajaja Arsenal Ivan alikua moja wa wakurugenzi wa Bodi ya ligi kuu soka ya marekani, MLS. He played a major role on developing it)*

Kwa mara ya kwanza kwenye historia yake Arsenal inabadilisha mfumo wake wa uendeshwaji. Sasa timu itakua inafundishwa na Kocha na sio Manager. Na huyu kocha atakua answerable to Club's CEO na Director of football kama timu zote ulaya zinavyofanya kwa sasa.

Na huyu kocha kama inavyozungumziwa na kuhusiwa na wengi anaitwa *Mikel Arteta*

Kumchagua Arteta kama mrithi wa Arsene Wenger ni kamari. Uwalakini na wasiwasi unaeleweka. Tayari uteuaji huu umeshaanza kugawanya mashabiki ambao walikua wameshagawanyika tayari kwa
uwepo wa Arsene Wenger.

Mikel Arteta hajawahi kufundisha timu yoyote kama kocha mkuu. Uzoefu wake umekuja kama kocha msaidizi Pep Guardiola at Manchester City

Mshabiki yoyote Arsenal angetamani kuona kocha atakae mrithi Arsene Wenger awe ni kocha mzoefu mwenye CV kubwa na nzuri.

Mikel Arteta alilelewa kwenye shule ya soka ya Barcelona maarufu kama La Masia, amecheza na kuongozwa Mauricio Pochetino kama captain wake (kocha wa sasa wa Tottenham) huko Rangers

Amefundishwa Everton na David Moyes zaidi ya miaka 3, Amefundishwa na Arsene Wenger kwa miaka 5. Alikua Captain wa Arsenal, yeye na viongozi wengine kama Per Mertesecker waliisaidia Arsenal kuvuka moja ya kipindi kigumu katika historia ya Arsenal (2011-2013, Arsenal iliuza wachezaji wengi nyota, kupigwa 8-2 n.k)

Baada ya miaka 9 bila kikombe chochote, Arsenal Under captain Mikel Arteta walishinda kombe la FA kwa misimu miwili mfululizo. Akiwa Arsenal aliendelea kuchukua course ndogo ndogo mbalimbali za ukocha *(Cha kushangaza kama alikua hachezi, Arteta alikuaga hakai kwenye benchi la wachezaji wa akiba Arsenal, alikua anakaa kwenye benchi la ufundi la Arsenal)* Hii ni kengele ya kwanza kulia kwenye akili yangu, ilitokea msimu wa mwisho wa Arteta ambao alikaa sana nje kwa majeruhi na nikahisi kuna kitu hapa. How can this happen? was he a player-coach?

Na Mwaka 2016, aliamua kuacha kucheza soka baada ya kusumbuliwa na majeraha. Na siku ya mwisho anachezea Arsenal alilia sana huku akiwaaga mashabiki uwanjani Emirates *(Kengele ya pili ililia kwenye akili yangu, huyu analia nini na hajakaa kivile hapa)*

wakati akijiandaaa kuondoka Arsenal Simu ya kwanza ilitoka kwa Mentor wake wa zamani Mauricio Pochetino akimuhitaji kama msaidizi wake Tottenham Spurs.

Kwa heshima aliyokua nayo Arsenal alikataa ofa ya Spurs. Simu ya pili ilikua ya Pep Guardiola. Huwezi kukataa kufanya kazi na kocha ambae to many ndie kocha bora zaidi kwenye ramani ya soka kwa sasa. Akaenda kua kocha msaidizi wa Pep G at Manchester City. Hata mimi nisingekataa.

Aliondoka Arsenal kwa baraka zote, na tetesi nyepesi sana zilivuja kua siku moja Arteta atarudi Arsenal, nilihisi hiki kitu lakini sikutegemea kama itakua mapema kiasi hiki.

Na miezi 24 baadae, hatimae Mikel Arteta anarudi "nyumbani" Arsenal kama kocha mkuu. Kama una akili kama mimi, utahisi kitu. Hii inaonekana ni kama dili ambayo ilishapangwa muda mrefu. Sema tu imewahi kidogo. Nafikiri Arteta alishaandaliwa kuja kua mrithi wa Arsene Wenger na ilipangwa iwe 2019. Sema mwenendo m'mbovu wa Arsene Wenger umewaisha mpango mzima

Wengi wana wasiwasi na uteuzi huu lakini kwa maoni yangu mimi nafikiri huu uteuzi unaweza ukawa chachu mpya, mwanzo mpya wa historia ya Arsenal, mwanzo mpya wa mfumo mpya wa Uendeshaji wa Arsenal. Nafikiri kwa timu iliyo nyuma ya Arteta, itampa msingi mzuri, mkubwa na nafikiri atafanya vizuri. Arsenal kabla ya kuondoka Arsene bado ilikua inaendeshwa kama its 1990's

Timu hii ni utatu mtakatifu wa *IVAN GAZIDIS, RAUL SANLLEHI NA SVAN MINSLATAT*. Mafanikio ya Arsenal kwa sasa yanategemea mahusiano mazuri ya hawa watu wao kwa wao, na wao na kocha mpya ambae tunaamini ni Mikel Arteta.

Chini ya Arsene Wenger Arsenal imemaliza ligi nafasi ya 6, ikicheza soka bovu kabisa lisiloeleweka tangu nianze kuifahamu Arsenal. mwaka 2018 Arsenal imefungwa game zote za ugenini kasoro mechi moja na ina wachezaji kama Lacazette, ozil, Aubamayeng na Mikhtryan. Hawa ni World class players, ni wachezaji ambao kila kocha anataka kua nao

Je unafikiri Arsenal under Arteta itamaliza nafasi ya 7, 8, 9.....?

Itafungwa mechi za Ugenini zaidi ya 12 ndani ya msimu mmoja?

Unafikiri kiungo ya Arsenal chini ya Arteta itakua unbalanced kama ilivyo saivi?

Je Arsenal ya Arteta ukabaji wake utakua kama ulivyo sasa?

Mimi nafikiri yote haya hayatokea. Je nafikiri Arsenal itachukua ubingwa? Kwa kweli sijui, atleast not next season.

Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Arsenal itabadilika. Ninajua namna yao ya kucheza itabadilika.

Mikel Arteta hana uzoefu wowote wa ukocha. Lakini by the out look ana kila dalili ya kua kocha mzuri wa kisasa.

-He is young
-He is visionary
-He is ambitious
-Anapenda ukocha, he has admited that.

Sifa nyingi zimemiminika kutoka Coaching staffs wa Arsenal, wachezaji wa Arsenal na to his credit watu wengi ambao ni Manchester City insiders wanamsifia sana Mikel.

Amekua sehemu ya Manchester City iliyoandika historia msimu huu na kuvunja kila aina ya rekodi kwenye ligi kuu ya Uingereza, na yeye kama kocha msaidizi na kiongozi wa mazoezi according to reports, then he is very much part of it.

Mashabiki wa Arsenal hawatakiwi kuogopa. *I think wana haki ya kua waoga, kua nervous but they should absolutely feel excited*

Kinachotakiwa ni kumsupport kwa 100%, ku support timu kwa 100% na kumpa muda. I predict msimu wake wa kwanza na wa pili kutokua misimu mizuri sana. Hata uongozi wa Arsenal unalijua hili. Arteta ana miaka 36 and for sure uteuzi huu si wa muda mfupi ni dhahiri kabisa *this is a long term strategy*.

Arsenal fans kama ni kufunga mikanda wafunge tu. This is going to be a pretty much rough ride but its gonna be an exciting journey and they will surely enjoy along the way.

Arteta ana akili sana. He was one of the anchor of an Arsenal midfield ambayo ilimfanya Aaron Ramsey acheze soka safi kuliko Yaya Toure msimu anafunga goli 18. Arteta controlled the midfield na alioongoza arsenal vizuri sana mpaka Majeruhi yaliyopoanza kuindama Arsenal na yeye pia na he never became the same player since that season na kiungo ya Arsenal haijawahi kuwa balanced since then.

Mikel Arteta atafanikiwa. Hana uzoefu lakini hata Zinedine Zidane na Pep Guardiola walipoanza kufundisha Real madrid na Barcelona *they had no experience or they had less*. na huko Madrid B na barcelona B hawakufanya vizuri sana tu.

Ebu nikumbushe kabla hajachukua ubingwa wa Ulaya na FC Porto 2004, Mourinho alikua anafundisha timu gani (mimi sijui)

Athletico Madrid ni timu ya kwanza ulaya kufundishwa na Diego Simeone na alitoka huko kwenye ligi ya Argentina ambayo wewe unaeisoma hii post hujui hata mchezaji mmoja zaidi ya Carlos Tevez, the rest aliyoyafanya Athletico Madrid ni historia.

Si kila wakati uzoefu unafanya kazi. Kama unapingana na mimi waulize ninu kimewatokea na David Moyes, Louis Van Gaal and what is happening with Jose Mourinho.

Kama ni uzoefu, Even Tony Pulis ana uzoefu na Premier league angekuwa kocha wa arsenal
IMG-20180518-WA0024.jpg
 
Nikushukuru sana My fellow Gooner kwa Mawazo haya Mazuri Kabisa!
Kwa Upande wangu nakuunga mkono kabisa kwamb Arteta tayar alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Wenger kwa Mda mrefu!
Nikujuze pia hata Arteta kwend kwa Gadiola ni mpango ulokuwa umesukwa Na Wenger kwa Baraka za Club! so Gadiola alikabidhiwa jukumu hilo kwa siri la kumkoch Arteta kwa ajil ya Arsenal baada ya Wenger!
Anyways, Nina imani AFC chini ya Arteta itabadilika na kuwa pia na approach nzuri kwa kila game!
Tumuamin, Tumsapport na Tumpe Muda Arteta ambaye kwa fununu toka Clabun AFC alikuwa pia anaitwa "coach" na wachezaj wenzake enzi akiwa Kapten!
 
Huwezi kuja kumlinganisha Arteta na Kina Zidane au Pep Gardiola katika mafanikio waliyatengeneza katika klabu za Real Madrid na Barcelona kwa muda mfupi.

Real Madrid na Barcelona ni klabu zinazotumia pesa nyingi sana katika kununua na kuwalipa wachezaji wao, Arsenal haina huo utamaduni. Mafanikio ya timu yoyote katika ligi kubwa zote duniani huwa yanategemea mambo haya muhimu.

1/Ushindani Pinzani.
2/Uwekezaji wa Kipesa.
3/Aina ya wachezaji.
4/Mfumo wa uchezaji(Hichi hufanywa na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha).

Mpaka sasa, mimi ninaamini Arsenal chini ya Wenger ilifanikiwa sana katika hicho kipengere cha nne lakini ikashindwa kwenye hivyo vipengele vingine. Pamoja na kwamb Arsenal ilishindwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa zaidi ya miaka kumi na nne, lakini bado Arsenal iliendelea kucheza mchezo mzuri zaidi, kuleta upinzani mkubwa zaidi kuliko timu zote kwa wastani wa miaka yote hiyo.

Ujio wa Arteta hautaweza kufanya chochote kipya zaidi ya kile ambacho Arsenal Wenger aliweza kukifanya. Tatizo kuu la Arsenal halikuwa Kocha, Arsenal wana matatizo makubwa zaidi kuliko la Kocha.

Yote kwa yote, mafanikio halisi ya Arsenal chini ya Arteta yatategemea muda, na hapo mashabiki wa Arsenal inapaswa wawe wavumilivu mnoo, itahitaji misimu kama minne hivi ili kuiona Arsenal ya Arteta.
 
mpeni timu msimu ujao awashushe daraja kabisaaaaa
mie nawasubiri pale OT machinjioni safari hii ni 8 bila
 
Ingependeza kama angeshirikiana na Patrick Viera. Kuwafanya wachezaji wawe a little bit tough. Arsenal ya sasa hivi wakosoft sana.
 
Nikushukuru sana My fellow Gooner kwa Mawazo haya Mazuri Kabisa!
Kwa Upande wangu nakuunga mkono kabisa kwamb Arteta tayar alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Wenger kwa Mda mrefu!
Nikujuze pia hata Arteta kwend kwa Gadiola ni mpango ulokuwa umesukwa Na Wenger kwa Baraka za Club! so Gadiola alikabidhiwa jukumu hilo kwa siri la kumkoch Arteta kwa ajil ya Arsenal baada ya Wenger!
Anyways, Nina imani AFC chini ya Arteta itabadilika na kuwa pia na approach nzuri kwa kila game!
Tumuamin, Tumsapport na Tumpe Muda Arteta ambaye kwa fununu toka Clabun AFC alikuwa pia anaitwa "coach" na wachezaj wenzake enzi akiwa Kapten!
Uliona mbali, Arteta atatufikisha mbali
 
Huwezi kuja kumlinganisha Arteta na Kina Zidane au Pep Gardiola katika mafanikio waliyatengeneza katika klabu za Real Madrid na Barcelona kwa muda mfupi.

Real Madrid na Barcelona ni klabu zinazotumia pesa nyingi sana katika kununua na kuwalipa wachezaji wao, Arsenal haina huo utamaduni. Mafanikio ya timu yoyote katika ligi kubwa zote duniani huwa yanategemea mambo haya muhimu.

1/Ushindani Pinzani.
2/Uwekezaji wa Kipesa.
3/Aina ya wachezaji.
4/Mfumo wa uchezaji(Hichi hufanywa na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha).

Mpaka sasa, mimi ninaamini Arsenal chini ya Wenger ilifanikiwa sana katika hicho kipengere cha nne lakini ikashindwa kwenye hivyo vipengele vingine. Pamoja na kwamb Arsenal ilishindwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa zaidi ya miaka kumi na nne, lakini bado Arsenal iliendelea kucheza mchezo mzuri zaidi, kuleta upinzani mkubwa zaidi kuliko timu zote kwa wastani wa miaka yote hiyo.

Ujio wa Arteta hautaweza kufanya chochote kipya zaidi ya kile ambacho Arsenal Wenger aliweza kukifanya. Tatizo kuu la Arsenal halikuwa Kocha, Arsenal wana matatizo makubwa zaidi kuliko la Kocha.

Yote kwa yote, mafanikio halisi ya Arsenal chini ya Arteta yatategemea muda, na hapo mashabiki wa Arsenal inapaswa wawe wavumilivu mnoo, itahitaji misimu kama minne hivi ili kuiona Arsenal ya Arteta.
Misimu mitatu tunaiona Arsenal ya Arteta
 
Nikushukuru sana My fellow Gooner kwa Mawazo haya Mazuri Kabisa!
Kwa Upande wangu nakuunga mkono kabisa kwamb Arteta tayar alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Wenger kwa Mda mrefu!
Nikujuze pia hata Arteta kwend kwa Gadiola ni mpango ulokuwa umesukwa Na Wenger kwa Baraka za Club! so Gadiola alikabidhiwa jukumu hilo kwa siri la kumkoch Arteta kwa ajil ya Arsenal baada ya Wenger!
Anyways, Nina imani AFC chini ya Arteta itabadilika na kuwa pia na approach nzuri kwa kila game!
Tumuamin, Tumsapport na Tumpe Muda Arteta ambaye kwa fununu toka Clabun AFC alikuwa pia anaitwa "coach" na wachezaj wenzake enzi akiwa Kapten!
😂😂 Hii siri uliitoa wapi?
 
Back
Top Bottom