PM Confirm the New MPs Sitting Allowance

Mimi naona 200,000 ni kidogo sana kwa mbunge, unless uwe umeshawekeza kama Zitto kwenye ma biashara mengine.
Yaah! hasa ukilinganisha na 10,000 wanazopata Drs wakiwa on call kuanzia saa9 jioni hadi saa 2 asubuhi ya kesho yake.
Hii ndiyo CCM bwana!
 
Mchukie mungu wako kwa kukukosesha marks za kuingia UDSM matokeo yake ukaenda vyuo vya waliofeli. Rejao ni level nyingine!


Hivi ni nini hasa kilichopofusha akili yako mpaka unachafua hewa kiasi hicho..anyway tukianza kulinanganisha vyuo vikuu kwa viwango vya ubora kielimu hapatatosha humu... Habari za level ingine hapa sio mahala pake lete hoja inayoeleweka.
 
Mchukie mungu wako kwa kukukosesha marks za kuingia UDSM matokeo yake ukaenda vyuo vya waliofeli. Rejao ni level nyingine!

Nikiangalia "sura yako" hapo, nikalinganisha na ulichosema nasikia kucheka hadi nianguke!
Kumbe umo kwenye mipasho ehh? Nilidhani umo kwenye siasa tu R.O.R( as per Lizzy)
 
How much PROOF do people need of this regime's disconnect with the events of the world. & of its commitment to sustain the statusQUO-(Corruption)! Indeed "flagrant failure by head of state"! ONLY the people of Tanzania can change Tanzania, NOT any politician or leader. ONLY the people, if they wake up & demand that the government is there to serve them not themselves!!
 
Jamani huyu mzee cjui anafikiriaje,hizi zitakua dharau rasmi kwa madaktari,yani hakuna hata siku moja ameamua sahihi katika maswala makubwa ya kitaifa,angeshusha basi hata iwe 150000 au hata chini kidogo ili tujue amefikiria pande zote
 
Sina hakika kama wabunge wote wa CDM (ukiondoa Shibuda) wanazipinga hizi posho, lakini kama ni kweli kwa umoja wao wanazipinga nawapongeza na waendelee kuzipinga. kutokana na uwingi wa wa wabunge wa CCM ni wazi pingamizi hili litashindwa na wabunge wataendelea kupokea posho kama kawaida labda kwa wale watakaoamua kususa kama Mh. Zitto alivyofanya huko nyuma.

Mtazamo wangu ni kwamba, kama pingamizi hili halitasikilizwa, na hatimaye posho kupitishwa, na kama kweli wabunge wa CDM kwa ujumla wao (47)hawazitaki hizi posho (kitu ambacho siamini) nawashauri wazichukue na wazifungulie account huko CDM makao makuu na zipangiwe shughuli za maendeleo kwenye majimbo yanayowakilishwa na CDM pamoja na maeneo mengine yanayohitaji kujiimarisha kisiasa.

Sisi wananchi kwenye majimbo yenu tuna shida nyingi sana, hatuna maji, hatuna zahanati, watoto hawana madawati, wengine hawana vyoo, hawana madarasa ya kutosha, pelekeni hizo pesa kwenye maeneo hayo nasi tutawaona kweli mlizikataa posho lakini mkazirudisha kwetu kwa njia nyingine. (nimejaribu kuzipigia hesabu ni karibu milioni tisini kwa kikao cha siku kumi kwa wabunge 48 wa CDM).

Mkizisusa, hao majambazi kamwe hawatazipeleka kwenye mfuko wa maendeleo kama mnavyotaka, watazitafuna mchana kweupe.
 
This is from Mh. Zitto Kabwe Zitto kwenye mtandao wake wa Twitter…

Just informed that the PM had a meeting with Editors today and confirmed a new rate for sitting allowance to MPs ie 200,000 tshs a day.

The PM says, he was asked by the President to deal with the matter. It is against the law for a PM to approve new rates.
...

hii kitu mbona sijaisikia kwenye vyombo vya habari except hapa JF imetolewa wapi? maana hata ukisoma summary ya mazungumzo ya PINDA utaona anazungumzia kupinga posho hii. which is which?
 
pinda-mizengo-top.jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa
anaongea na vyombo vya habari jana ofisini kwake

Katika mkutano huo, (aliofanya na vyombo vya habari ofisini kwake Magogoni jana) Pinda alizungumzia mzozo wa posho mpya za wabunge na kuunga mkono kwamba zinapaswa kuongezwa.


Alisema Rais Jakaya Kikwete amelikabidhi faili la mapendekezo ya posho mpya kwake (Pinda) na kuanzia sasa ndiye mwenye mamlaka ya kusaini au kutosaini.


Pinda alisema wapo wabunge ambao mwisho wa mwezi hawabaki na kitu, kwani fedha zao zote za mishahara zimekatwa kulipia madeni waliyoingia kwa ajili ya kusaidia majimbo yao.
“Rais amerejesha lile faili kwangu, kwa hiyo nimepewa mamlaka ya kusaini au kutosaini. Lakini ukweli ni kwamba posho za wabunge ni ndogo na zinapaswa kuongezwa,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Tanzania Daima
 
Nafikiri kuna haja ya wananchi kuanza kuwatandika mawe viongozi wa Serikali popote wawapo ili wajue kwamba wananchi wamechoshwa na tabia zao za kifisadi na kutojali mustakabali wa sasa na baadaye kwa wananchi wa Tanzania.
 
Mimi naona 200,000 ni kidogo sana kwa mbunge, unless uwe umeshawekeza kama Zitto kwenye ma biashara mengine.

Na zumbemkuu likes this.

Hii kweli ni vita ndani ya CDM..yaani siku zoooote the so called Zumbemkuu amekuwa akipingana na huyu mama..ila leo kwa kuwa Zitto karushiwa kijembe naona amempa ''like'' duuuuuuuuuuuuh! chuki mpaka basi dhidi ya Zitto.
 
Mwenye mamlaka ya kutia sahihi sheria na mafao ya wabunge kikatiba ni rais au Waziri Mkuu? hapa naona kama kuna mchezo wa kuchanganya karata.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wacha wale tu!!! Ila ipo siku, watajuta kuzaliwa!!

FF na Rejao, tunawajua nyinyi ni puppets wao, kwa hiyo tunasonga nanyi tu, kiaina!! Kumbuka siku hiyo hata mbwa wao watakiona!!!
 
Na zumbemkuu likes this.

Hii kweli ni vita ndani ya CDM..yaani siku zoooote the so called Zumbemkuu amekuwa akipingana na huyu mama..ila leo kwa kuwa Zitto karushiwa kijembe naona amempa ''like'' duuuuuuuuuuuuh! chuki mpaka basi dhidi ya Zitto.

FF kanena ukweli, hakuna mwenye chuki na zitto, huo ni ukweli, mwambie aje hapa akanushe na kueleza ile gari aliyopewa na Mkono what was the gift for. Anajidai hataki kuchukua posho kuwahadaa wananchi huku ikipewa pesa nyingi na mafisadi.
 
Kiongozi shupavu ni yule anayesimama kuutetea ukweli hata ikibidi kufukuzwa ili mradi yupo juu ya kweli.

Pinda unavunja sheria ali mradi rais kakwambia.

Haya, posho 200,000 ipo siku tutatundika madaluga ya amani na kufundishana adabu.

My take: Fanyeni mfanyalo ila mjue kile kizazi kilicholelewa na Nyerere kinazidi kupotea, kizazi kinachokuja hakikulelewa kwenye sera za ujamaa na pia wengi wameenda shule na wengine wako mtaani bila ajira. Sasa muwe makini...ni hatari kwa nchi...kila mtu anataka kipande cha keki ya taifa..
 
Back
Top Bottom