Please be extra carefull

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Napenda kuwataatharisha kuwa muwe makini zaidi mkiwa barabaran hasa kwenye foleni.Kuna kundi la vijana zaidi ya 30 wanavamia magari wakiwa na mapanga,nondo na visu kwa lengo la kupora chochote ulichonacho na halikadhalika wanauwa ama kujeruhi.


Maeneo hatari ni maeneo ya Jangwani- Morogoro Road,Ocean Road Seaview,Salender Bridge, Bonde la Kigogo ukitokea Ilala kuja Magomeni, Daraja la Ubungo karibu na njia panda ya kwenda UDSM na barabara ya Mandera Road ukitokea Tazara kuja Ubungo (NDIPO aLIPOVAMIWA RAFIKI YANGU)


His Case. Akiwa kwenye folen majira ya saa mbili usiku, ghafla lilitokea kundi la vijana kama kumi na mapanga na kuanza kupiga vioo vya gari wakitaka kuvunja, aidha waliongezeka ghafla na wakafunga barabara kama kwa dk 7 hivi wakiendelea kumshambulia (kwenye gari walikuwa watatu), kumbuka kwenye folen huwezi kukimbia popote, mungu aliwasaidia sana kwani milango ya gari ilikuwa imefungwa/locked, na vioo vilikuwa vimefungwa kasoro kimoja kilikuwa wazi nusu. Baada ya mapambano na kelele za kuomba msaada,ndipo msamalia mwema aliyekuwa na silaha aliingilia kati na ndipo alipowatawanya.


Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali, haya matukio yamekuwa yakiongezeka sana katika siku za usoni, kwa hilo nawatahadharisha msinunue vitu ovyo kwenye trafic light, vioo msishushe ovyo na lock za milango ya magari mfunge, muwe makini.Ujambazi huu unafanyika kila siku sehemu tofauti kuanzia saa 12 jioni kuendelea.


Namshukuru mungu hakuna aliyeumizwa sana, japo walifanikiwa kupata baadhi ya vitu ikiwemo simu ya mwenye gari.

Natambua unaweza kuona kama sinema,ila haya ndio yanayotokea Katika jiji la Dar kwenye folen za magari.

Una lipi la kuongezea? BYE.
 
Asante sana Mhache kwa ushauri huo manake wengi wetu tukiwa kwenye foleni ndo tunazama kuongea na simu saana na kujisahau.Mwenye kuelewa na aelewe mwache anayebisha yaamkuta.
 
Thanks kwa kutukumbusha mkubwa na kututajia maeneo hatari sana....nafikiri ndugu zteu kina Mwema itabidi nao waongeze wale vijana wao ma ''TIGO'' kny maeneo hayo kulinda zaidi usalama wa raia!
 
Naomba Invisible umtumie E-mail Aande chagonja na Tossi kuhusiana na hili.

Ila suluhisho ni nini?
 
Ninashukuru waliosoma mada hii na kuiona kwamba ni muhimu na wataifuatilia ili kutokumbwa na maswaiba hayo ya kwenye foleni.
 
sasa serekali haijachukuwa hatuwa zozote ikiwa imefikia hali kuwa hivi ?
 
Mhache, mkuu nakushukuru kwa kufanya your civic duty kwa kuwatahadharisha wananchi wenzako. Nadhani ni vyema tahadhari yako ungesambaza pia kwa njia ya email. Wazungu wanakuwa na Alert system yao, na wanasambaza taarifa kwa njia hii.
Tafadhali muwe makini na mkae wote salama... naona suluhisho sasa ni kutembea na silaha!
Mungu atunusuru!
 
Hakika usalama umekuwa mdogo sana kama hali ndiyo hiyo. Tunashukuru kwa taarifa lakini kwa tahadhari jingine ni kutoa lift kwa watu usio na uhakika nao; kwa mfano rafiki yangu alitoa lift kwa vijana wawili wakionyesha kuwa wewe unafahamiana na kaka yao (wanamtaja)halafu wakipanda wakati unaendesha gari wao wanachomoa 'power window machines' halafu wakimaliza wanakuambia tushushe hapa.. wakiwa na mashine hizo. Unagundua baadae huna power windows wanaingia na bisbis kwenye gari.
 
Kinachonisikitisha ni kuwa hakuna mtu anayejali! Kwa kuwa Wakulu maeneo yao yako salama wanatuachia tubebe mzigo wetu!

Naona kila mtu achukue tahadhari kwani hii hali inatisha sana. Na wale wenye gari zisizo na vioo (mfano wa chuma chakavu) itabidi wabadili njia au wakiona muda umeshaenda waziache ofisini wakamate daladala. Vinginevyo kila mtu tatakiwa kiwa kama Dito! Akikuribia kijana hata kama anauza miwa unawasha tu!! Tutafika kweli???
 
Back
Top Bottom