.............Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii, alisema Pinda na kuongeza: Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu.
Hata hivyo, Pinda alisema kuwa serikali haijafilisika. Pamoja na hayo serikali haijafilisika kwani ingekuwa hivyo wewe usingekuwa hapa bungeni? alihoji...............
Kumbe siku nyingine magamba hukuachia ufikiri kama msomi!
Mimi penda hii!
Labda kwa nyongeza....
10) Rudisha mikoa 17 na wilaya zilizokuwepo kabla ya kuongeza mikoa kuwapatiau laji washikaji wenu
11) Vunja baraza la mawaziri na unda baraza lisilozidi wizara zisizozidi 20. Kwa nini nchi zilizoendelea zina wizara 14, sisi tuwe wizara zaidi ya sitini? Mzigo mkubwa wa serikali umo katika utawala kuliko katika uzalishaji.
12) Vunja makampuni yote ya umma ambayo si wazalishaji na yatakayobakia kwa kuwa niwazalishaji yajiendeshe wenyewe.
13) Acha kuwaonea haya wezi serikalini; badala ya mwizi kumsimamisha kazi au kumpangia wizara nyengine, kwanza alipe kila senti aliyoiba na ikibidi kwa interest.
14) Vunja mikataba yote bomu na muanze upya kwa masharti itakayoweka serikali na siyo kwa masharti mtakayowekewa na wawekezaji.
15) Usisamehe kodi kwa wawekezaji ambao mwisho wa yote hawaiingizii faida serikali bali faida yote wanachukua wao.
16) Wekeza katika elimu - taifa linalodharau elimu linafuga wajinga baadaye wanageuka vibaka na wajanja.