Pinda: Serikali inakabiliwa na hali mbaya kifedha

Sasa Mkulo alikuwa anakanusha nini?
Na Pinda naye kazi yake ni kulalamika tu, achukue hatua.
 
Mambo ya kujifunga mkanda? duh waanze wao

1) Punguza safari fanya majadiliano mengine kwa Tele conference
2)Punguza magari kwenye misafara
3)Punguza ziara zisizo la lazima mikoani
4)Punguza kununua magari ya watumishi, wakopeshe wajihudumie wenyewe
5)Punguza warsha, semina zisizo na tija
6) Fanya "Jerry-Mandering" upunguze constituency za ubunge tuwe na 50% ya wabunge tulionao sasa
7)Rekebisha sheria za uchaguzi , no chaguzi ndogo ndogo
8)Punguza watumishi wa serikali wasio na tija
9) Angalia upya sheria za manunuzi ya umma na taratibu zake ambazo zinaigharimu sana serikali, private sector wananunua vitu hivyo hivyo kwa 50% ya bei.
 
Miradi mingi imesimama kitambo sasa
cha kusikitisha hata ilemiradi iliyokuwa inachangiwa nusu kwa nusu na wafadhali serekali imeshindwa kutoa fuungu lake ikaishia kusimama

chanzo sio kukosa pesa kikubwa ni matumize ya sio ya msingi
Waziri wa fedha hastahili hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi lakini bado kwa watawala anaonekana lulu, kwenye mashirika ya uma kuna ufujaji mkubwa saana wa pesa, wafanyakazi wa taasisi mbali mabli za uma wameona isiwe tabu wanaiba kama serekali imeenda usingizini

cha kufurahisha wafadhili hususani waingereza wameishtukia hii gvnt ya kiujanja ujanja, UK kuna NGO imeshaanza kuwahamasisha walipa kodi waishinikize serekali yao iache kuipa msaada serekali ya Tanzania, wanaona misada inasababisha inflation kwani misaada mingi haiendi kwenye maeneo yaliyokusudiwa, inaishia mifukoni mwa wateule wachache

Ni matumaini makubwa kwamba wafadhili wengi watajiondoa kuisaidia budget ya mwaka huu, na utakuwa mwisho wa matanuzi kwa hawawateule wachache
 
Mi nashangaa tuifanya hii kuwa issue sasa, Serikali ya JK ilikwishafilisika kitambo tu...

Kwa kuwa walitaka kusubiri facts ziwaumbue, basi na wameona...
 
hebu fikiria kwanini wameanzisha mikoa mipya wakati hawana pesa? au ipo kwa ajili ya kuwapatia jamaa zao kazi na mashangingi ya kulipa fadhila wakati wa kampeni?
 
hali hii ilianza kuonekana soon before 2010 election. na hapa wenye akili walijadili.leo hii hali inakuwa ngumu sana kwasababu ya ujinga wa walioko madarakani kushindwa kusoma alama za nyakati. sijui ni kwanini serikali iliamua kufanya sherehe kubwa sana ya miaka 50 ilihali hela hakuna. hivi zaidi ya walim na wanajeshi watumish wengine wote wa serikali huwa wanapokea mshahara hadi tarehe 36-40. siipendi tanzania kwa kushindwa kutujali wananchi wake.
 
Hawa CCM na serikali yake watupishe,hakuna sababu ya kunq'anq'ania kuendesha nchi wakati mumeshindwa kuongeza pato la taifa,hebu Mh, Jakaya Mrisho atueleze amejipendekeza kwa hao wazungu,wamemfanya nini sasa,mbona wamemuacha angamie kama hajui kwamba wanamsomesha basi agutuke
Ondoa Waziri wa fedha kwa sababu ameshindwa kukusanya kodi na kudhibiti mfumuko wa bei

Ondoa Ndulu hana maana kabisa ameifanya shilingi yetu kukosa thamani na kurusu dolla kutoroshwa kiasi kikubwa leo hii wakenya wanatoka kenya na shilingi ya Tanzania na kuja kubadili Arusha kupata dola uliona wapi nchi gani haina mfumo mzuri wa kudhibiti fedha
Ondoa waziri wa mawasiliano ana uchukuzi ameshindwa hata kufanya bandari zetu zikawa kitovu cha mapato
Ondoa Ngereja ,huyu ni kati ya wale mumiani wa rasilimali wa taifa mikataba ya ajabu ajabu inasaniniwa mbele ya uso wake Uranium,gesi,mafuta,dhahabu,shaba,vito kuna kitu kitabaki kweli
Ondoa ezekiel Maige mali asili huyu ndio ovyooooooooo ,kabisa misitu inavunwa kama kawa,wanyama,hakuna utalii
Ondoa waziri wa mifugo na samaki
waziri wa kilimo
Ondoa Jakaya mwenyewe na waziri wake mkuu Pinda
Kabidhini nchi kabla wenyewe hawajaichukua
 
Sasa Mkulo alikuwa anakanusha nini?
Na Pinda naye kazi yake ni kulalamika tu, achukue hatua.

pinda analalamika nini? walivyokuwa wanaiba hela ya serikali
na kuwekeza kwenye mabasi ya s.,u.mry alifikiri hazitaisha?
asituzuge, auze mabasi na kurudisha hela zetu, na awaambie
na wenzake, halafu inakuwaje serikali haina hela but inatoa
mil 10 kama rambirambi? nadhani kwenye fungu la rambirambi
kuna hela bwerere... tuanze kuzitumia hizo badala ya kulalama tu
kama anat.i.wa.
 
Pinda alikiri kuwa hali ya maisha imepanda, lakini si kwa Watanzania tu kwani hata nchi zinazoizunguka nchi hali ni hivyo hivyo.
“
CHANZO: NIPASHE

Mijadala ya awali:

Kauli za WATAWALA wasiokuwa na majibu ya matatizo ya wananchi ni kama hapo kwenye red, kila wakibanwa, wanasema hata kwa majirani zetu au dunia nzima hali iko hivyo! HOVYO kabisa! China na Korea walisema kwenye miaka ya '60 walikuwa kama sisi, lakini hawakuwa na majibu mepesi kwa maswali magumu kama sisi! Leo wakituletea bidhaa tunazibeza wakati kimaendeleo wanatoka nduki wakati sisi bado tumelala!
 
Mambo ya kujifunga mkanda? duh waanze wao

1) Punguza safari fanya majadiliano mengine kwa Tele conference
2)Punguza magari kwenye misafara
3)Punguza ziara zisizo la lazima mikoani
4)Punguza kununua magari ya watumishi, wakopeshe wajihudumie wenyewe
5)Punguza warsha, semina zisizo na tija
6) Fanya "Jerry-Mandering" upunguze constituency za ubunge tuwe na 50% ya wabunge tulionao sasa
7)Rekebisha sheria za uchaguzi , no chaguzi ndogo ndogo
8)Punguza watumishi wa serikali wasio na tija
9) Angalia upya sheria za manunuzi ya umma na taratibu zake ambazo zinaigharimu sana serikali, private sector wananunua vitu hivyo hivyo kwa 50% ya bei.
Mimi penda hii!
Labda kwa nyongeza....
10) Rudisha mikoa 17 na wilaya zilizokuwepo kabla ya kuongeza mikoa kuwapatiau laji washikaji wenu
11) Vunja baraza la mawaziri na unda baraza lisilozidi wizara zisizozidi 20. Kwa nini nchi zilizoendelea zina wizara 14, sisi tuwe wizara zaidi ya sitini? Mzigo mkubwa wa serikali umo katika utawala kuliko katika uzalishaji.
12) Vunja makampuni yote ya umma ambayo si wazalishaji na yatakayobakia kwa kuwa niwazalishaji yajiendeshe wenyewe.
13) Acha kuwaonea haya wezi serikalini; badala ya mwizi kumsimamisha kazi au kumpangia wizara nyengine, kwanza alipe kila senti aliyoiba na ikibidi kwa interest.
14) Vunja mikataba yote bomu na muanze upya kwa masharti itakayoweka serikali na siyo kwa masharti mtakayowekewa na wawekezaji.
15) Usisamehe kodi kwa wawekezaji ambao mwisho wa yote hawaiingizii faida serikali bali faida yote wanachukua wao.
16) Wekeza katika elimu - taifa linalodharau elimu linafuga wajinga baadaye wanageuka vibaka na wajanja.
 
Mambo ya kujifunga mkanda? duh waanze wao

1) Punguza safari fanya majadiliano mengine kwa Tele conference
2)Punguza magari kwenye misafara
3)Punguza ziara zisizo la lazima mikoani
4)Punguza kununua magari ya watumishi, wakopeshe wajihudumie wenyewe
5)Punguza warsha, semina zisizo na tija
6) Fanya "Jerry-Mandering" upunguze constituency za ubunge tuwe na 50% ya wabunge tulionao sasa
7)Rekebisha sheria za uchaguzi , no chaguzi ndogo ndogo
8)Punguza watumishi wa serikali wasio na tija
9) Angalia upya sheria za manunuzi ya umma na taratibu zake ambazo zinaigharimu sana serikali, private sector wananunua vitu hivyo hivyo kwa 50% ya bei.
Kumbe siku nyingine magamba hukuachia ufikiri kama msomi!
 
[/LEFT]
Matumizi yasiyo ya lazima ni yapi hayo na nani anayeamua kuwa matumizi fulani ni ya lazima na mengine siyo na kwa sababu zipi? Kwa mfano, matumizi kwa ajili ya vazi la taifa ni ya lazima?

Serikali ilitumia billioni 50 kwa wizara kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa bendera ; fedha ambazo hazikuwa kwenye budget !! Je matumizi kama haya kwa nchi masikini ni ya lazima ? Nani anatakiwa kuwajibika kwa ufisadi kama huu?
 
Pinda ni msemaji sana na hajui hata analoliongea,
SERIKALI haina uhaba wa fedha! nakama hamuamini hilo subirini atakuja kukanusha soon!
 
Kama unaumwa tumbo la kuhara halafu unajizuia lazima utaumbuka tu mbele za watu...haya sasa wal;ikataa nini na wamekubali nini sasa??
 
Serikali inakabiliwa na hali mbaya kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo, serikali imeziagiza wizara na taasisi zake kufunga mkanda na kuhakikisha wanabana matumizi ili angalau fedha zilizopo ziweze kumaliza mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo bungeni jana wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Pinda alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, aliyetaka kujua serikali inafanaya nini kupunguza makali ya maisha kwa watanzania hasa kutokana na kupanda kwa kiwango cha mfumuko wa bei.

Mohamed alihoji kama serikali imefilisika kwa kuwa Wizara na idara zake zote zimekuwa zikilalamikia ukata. Mbunge huyo alisema hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa mbaya kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu, lakini serikali haionyeshi jitihada za makusudi kukabiliana na hali hiyo. Katika majibu yake, Pinda alikiri kuwa hali ya maisha imepanda, lakini si kwa Watanzania tu kwani hata nchi zinazoizunguka nchi hali ni hivyo hivyo.

“Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii,” alisema Pinda na kuongeza: “Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu.”

Hata hivyo, Pinda alisema kuwa serikali haijafilisika. “Pamoja na hayo serikali haijafilisika kwani ingekuwa hivyo wewe usingekuwa hapa bungeni?” alihoji.

CHANZO: NIPASHE

Mijadala ya awali:

Ukiona Waziri Mkuu anawaomba wafanya biashara badala ya kutoa AGIZO, ujue tumekwisha!!!! Lile jembe la Monduli lingeshaagiza siku nyingi.
 
Ukiona Waziri Mkuu anawaomba wafanya biashara badala ya kutoa AGIZO, ujue tumekwisha!!!! Lile jembe la Monduli lingeshaagiza siku nyingi.

Nae hana lolote zaidi ya ubinafsi na ulafi wa kujilimbikizia mali tu!
 
siku niliona gari linajinadi ' national planning commision , national think tank, lets think together' kwnza nikacheka kisha nikaanza kuhuzunika. hivi hawa jamaa huwa wana plan kitu gani? au wlioko huko ni wazee wa darisalam
kwa kuongezea huko juu
17. waache kununua fenicha nje maofisini wakalie viti kama vya waalimu wanunue viti jkt
 
Serikali inakabiliwa na hali mbaya kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo, serikali imeziagiza wizara na taasisi zake kufunga mkanda na kuhakikisha wanabana matumizi ili angalau fedha zilizopo ziweze kumaliza mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo bungeni jana wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Pinda alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, aliyetaka kujua serikali inafanaya nini kupunguza makali ya maisha kwa watanzania hasa kutokana na kupanda kwa kiwango cha mfumuko wa bei.

Mohamed alihoji kama serikali imefilisika kwa kuwa Wizara na idara zake zote zimekuwa zikilalamikia ukata. Mbunge huyo alisema hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa mbaya kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu, lakini serikali haionyeshi jitihada za makusudi kukabiliana na hali hiyo. Katika majibu yake, Pinda alikiri kuwa hali ya maisha imepanda, lakini si kwa Watanzania tu kwani hata nchi zinazoizunguka nchi hali ni hivyo hivyo.

“Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana
ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii,” alisema Pinda na kuongeza: “Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu.”

Hata hivyo, Pinda alisema kuwa serikali haijafilisika. “Pamoja na hayo serikali haijafilisika kwani ingekuwa hivyo wewe usingekuwa hapa bungeni?” alihoji.

CHANZO: NIPASHE

Mijadala ya awali:

Hapo kwenye RED, Wanasubiri nini kama wameshindwa kufanikiwa kupunguza hali ya Maisha ya Watanzania? Wamefeli lakini bado wanang'ang'ania Madarakani, kwanini msiachie ili watu wenye uwezo wakutumia akili wakaja na mbinu mpya? Mmeshasema kuwa mmeshindwa mbinu zenu zote za kimasaburi lakini bado tu mpo. Kweli Tanzania inaongozwa na Viongozi wanotumia Masaburi kufikiria.

Mnatutia aibu kuwa na viongozi wenzawazimu kama hawa tulionao sasa
 
Mmmhhhhhhhhhhhhhhhhh sielewi? imekuwaje???????????/////// Serikali imefilisika? iefulia? imechacha?
kwa hiyo Mh. Pinda anataka tufanyeje? mbona sababu za kuishiwa kwa serikali yetu hazisemi? tutafanya nini kuondokana na huo ukata? inatisha sana sana!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom