Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya jana kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.

Pinda alisema hayo, baada ya gazeti hili kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga Sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

"Suala hilo bado tunalifanyia kazi," alisema Pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na Rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. "Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."

Akizungumzia suala hilo la Jairo bungeni juzi, Pinda alisema: "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

"Tuhuma za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.

"Tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DP kwa ajili ya utaratibu," alisema Shellukindo akiinukuu barua hiyo.

 
Ni maagizo gani mapya hayo ambayo Pinda hayasemi, halafu kulifanyia kazi maana yake ndio nini na nani analifanyia kazi????
 
Tatizo la katiba tuliyonayo uamzi wowote anaamua Rais, ilitakiwa maamuzi yawe yanaongozwa na katiba, yaani hapo angeambiwa tu kuwa kwa mjibu wa katibu ya nchi Sura ya xxx, kifungu, umevunja katiba na adhabu yake ni kumvua madaraka na kumfanyia uchunguzi kwa makosa mengine aliyoyafanya akiwa mtumishi
 
si ajabu rais anataka waanze kufanya uchunguzi kama kawaida watasema wanaunda kamati. kweli kuna haja ya mambo yote yaongozwe na katiba ya nchi si mtu moja.
 
Inakuwaje kiongozi wa serikali bungeni hana mamlaka ya kuwawajibisha anaowasimamia bungeni? nini maana ya kuwa kiongozi? And anyways tunajua Vasco alikua safarini, lakini si makamu wake yupo? Grrrrrr...... aah wacha niseme.wakati mwingine mimi naona bora Lowasa.
 
mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua
"Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."
Hizi statement mbili hizi, yaani ilipaswa huyu mtu achuliwe hatua sasa sijui hayo maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo wanalazimika kuyafanyia kazi ni yapi na kwanini hawayasemi kwani imeishakuwa ni siri?????
 
Atakuwa kaambiwa atulize mambo ikiwezekana ajaribu kuchakachua akili za wabunge bajeti ipite.

kwa vyovyote atakuwa amemwambia kuwa hata yeye anahusika.

nchi hii hatuna head of state....
 
Mimi sishangilii sana Jairo kutimuliwa kazi, hata kidogo.

Imani yangu na nitazidi kuamini hivyo mpaka siku ya Mwisho ni kwamba jairo hakuamka kitandani kwake na kuingia ofisini aandike ile barua.
Kama lilikua wazo lake Binafsi lazima walikaa vikao na kushauriana na waziri husika au mkubwa mwingine.

Kama sio wazo lake ni lazoma alipewa maelekezo na aliye juu yake.

Inaposemekana rais ametoa maagizo mapya nakubaliana mia kwa mia na na hilo kwasababu Ni issue kubwa ambayo hamhusu Jairo peke yake au haimhusu yeye kabisa.

Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?
 
wanataka kulifanya swala hili liwetamu zaidi unajua magamba huwa hawasomi alama za nyakati siku zote hufanya maamuzi too late na huwa inawagharimu sana kisiasa. Ngoja tusubiri hapa wananchelewesha tu maamuzi lakini hakuna namana ya kuokoa chochote na wakifanya vinginevyo lazima ile kwao.
 
Mapya! Nadhani alitamani kumtimua au bosi kabadili maamuzi wanatafuta kisiwa cha kumficha J.
 
Ni kweli nchi imefilisika kiuongozi. Kwa mawazo yangu nafikiri Pinda na Mkuu wa nchi wanataka kuokoa jahazi la bajeti ya wizara ya Nishati na Maadini ili ipite. Mimi NASHAURI tujitahidi kwanza tupate umeme ili tufanye kazi.
 
Tatizo la katiba tuliyonayo uamzi wowote anaamua Rais, ilitakiwa maamuzi yawe yanaongozwa na katiba, yaani hapo angeambiwa tu kuwa kwa mjibu wa katibu ya nchi Sura ya xxx, kifungu, umevunja katiba na adhabu yake ni kumvua madaraka na kumfanyia uchunguzi kwa makosa mengine aliyoyafanya akiwa mtumishi

Ubaya wa kurundika maamuzi kwa Rais ndio haya matokeo ya maneno ya Pinda, pamoja na kwamba rasimu ya katiba mpya inaandaliwa lakini kuna umuhimu wa kuujulisha uma kupitia scandali hii kwamba haki haitapatikana kwa mfumo huu tulionao hivi sasa na tegemeo letu ni vyama vya upinzani kutuunganisha kwa maandamano ili ujumbe ufike ndani na nje ya inchi
 
tunaposema jk ndo chanzo cha matatizo nchii huwa tunaamnisha.......mtu ametarifiwa na akapewa ushahid kuwa swala hili halivumiliki na huyu mtu anapaswa kufukuzwa...yeye bado analemba kwa kutoa maagizo mapya...
 
Mimi sishangilii sana Jairo kutimuliwa kazi, hata kidogo.

Imani yangu na nitazidi kuamini hivyo mpaka siku ya Mwisho ni kwamba jairo hakuamka kitandani kwake na kuingia ofisini aandike ile barua.
Kama lilikua wazo lake Binafsi lazima walikaa vikao na kushauriana na waziri husika au mkubwa mwingine.

Kama sio wazo lake ni lazoma alipewa maelekezo na aliye juu yake.

Inaposemekana rais ametoa maagizo mapya nakubaliana mia kwa mia na na hilo kwasababu Ni issue kubwa ambayo hamhusu Jairo peke yake au haimhusu yeye kabisa.

Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?
Wanatafuta jinsi gani ya kumuokoa Ngeleja na wenzake yaani Serikali hii ya kishikaji ni ujinga na ushenzi mtupu.
 
Tatizo Rais amelimbikiziwa madaraka mengi sana hadi imekuwa kero yaani kuteua Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na mengine yote hayo anafanya Rais pia kuwafukuza hadi asubiriwe Rais ndio atoe uamuzi huu ni upuuzi mtupu kama sio utumbo
 
Hamna jipya hapo..Tumeshazoe kauli za JK za kawaida sana hasa ukizingatia wizara yenyewe ina skendo nyingi..richmond, dowans, symbions, IPTL, songas na zinginezo ambazo lazima Jairo atakuwa anafahamu mchezo mzima unavyoendelea..Hapa lazima wakae kwanza Jairo aapishwe kwanza kwamba wewe unaondoka lakini kama kawaida yetu hakuna kusema neno lolote kuhusu ishu zetu..Katibu mkuu anafahamu mabo mengi sana yanayoendelea ndani ya wizara hiyo vinginevy wasipo fanya hivy basi tutasikia mengi sana...........................
 
naamini pinda anafedheeka sana moyoni na kuona Rais ni lege lege.maana kwa kauli yake ya juzi ni kwa huyu jairo angekuwa hana kazi lakini kwa kuwa syndicate nzima inamhusisha rais basi lazima afanye manuva ili a spin issue nzima.......na inavyoonekan hapa ni kuwa huyu jamaa(jairo) anaweza kusave
 
Wanatafuta jinsi gani ya kumuokoa Ngeleja na wenzake yaani Serikali hii ya kishikaji ni ujinga na ushenzi mtupu.
Mkuu afadhali umeliona hili...ushakaji na kulindana kumezidi mno..ndio maana Dr hosea aliwaambia wikileaks kuwa JK huwa hachukulii siriazi maswala ya rushwa
 
Back
Top Bottom