Pinda kwenda Uswiss

FOE

Member
Sep 21, 2009
87
6
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anaondoka Dar es Salaam leo usiku kwenda Geneva, Uswisi kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye Mkutano Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Kimataifa (International Telecommunication Union – ITU).
Pinda atafuatana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msola.
Mkutano huo utajadili wajibu mkubwa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendeleza uchumi. Katika mkutano huo kutakuwa na kikao maalum cha wakuu wa nchi.
Serikali inatilia mkazo uendelezaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Sijui atarudi na kituko gani huko. Let's wait and see!!:)

Mkuu sina uhakika kama tunachosubiri ni PM kurudi na kituko ila cha muhimu ni kuona anamuwakilisha Rais kikamilifu kwenye huu mkutano maana IT ni suala nyeti sana kwa maendeleo ya taifa na pia mahusiano yetu kimataifa.
 
Sijui atarudi na kituko gani huko. Let's wait and see!!:)

Mvua za kutengeneza, au kupiga marufuku viongozi kuvaa suti au kingine chochote kinachofanana na hivyo. Usitegemee zaidi ya hayo mkuu.
 
Mvua za kutengeneza, au kupiga marufuku viongozi kuvaa suti au kingine chochote kinachofanana na hivyo. Usitegemee zaidi ya hayo mkuu.

They say this is related to ICT. May be atapiga marufuku matumizi ya laptop na blackberry kwa watz. It is too expensive!!!!
 
Back
Top Bottom