Pinda: Karibu asilimia Tisini na Tisa (99%) ya Wanzanzibar ni Waislam

Status
Not open for further replies.

Simba mnyama

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
348
129
Wana- JF,

Hivi punde katika kipindi cha maswali na majibu Waziri Mkuu, Pinda ameulizwa swali na Mh. Mchungaji Msigwa kuwa huko Zanzibar kuna tamko limetolewa na kiongozi mmoja kuwataka wafanyabiashara wote wa mahoteli kutokuuza chakula hasa wakati wa mchana kwa vile waislamu wako katika mfungo wa Ramadhani. Mbali na hilo kuna pia agizo kuwa wanawake wasivae nguo fupi katika kipindi hiki kwa vile wanawatamanisha wanaume.

Aidha, Waziri mkuu amesema amri ya kutokuuza chakula huko iko sawa kwa vile mazingira ya huko zanzibar yanaonesha kuwa asilimia kama tisini na tisa (99%) ya wananchi huko ni waislamu. Licha ya kuingilia haki za watu wengine na imani za watu wengine, naona kwa mtazamo wangu suala hili halikutakiwa kujibiwa namna hiyo na Waziri Mkuu.

Naomba wenye takwimu watuambie kama kweli 99% ya wananchi wote ni waislamu na kama watu wengine wanaoishi huko hawana haki kwa mujibu wa Katiba.

Nawasilisha.
 
Unaonaje kama kwenye sensa kingekubalika kile kipengele cha dini ! Ni kujifanya kujua zaidi ,hata huku Tanganyika waislamu ni 85% waliobaki wanaabudu masanamu au hawana kabisa.
 
Leo bungeni katika hali ambayo imeshangaza wengi,Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kayanza Peter Mizengo Pinda amejibu swali gumu kirahisi sana kwa maono yangu. Ameliuzwa kuhusu kauli iliyotolewa na viongozi wa kiislamu ,Zanzibar...kauli ambayo iliamuru kukomesha uvaaji wa nguo zisizoendana na uislamu pia wameamuru kukomesha vitendo vya watu kula (hovyo) katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mhe, Pinda amedai kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Zanzibar ni Waislamu (hilo silipingi) hivyo suala la sheria na kanuni za kiislamu kutumika siyo hoja. Je,ni sawa kanuni hizi zisizokuwemo kwenye katiba yetu kutumika huku ikijulikana nchi haina dini? Pili , Wakristo kuwa wachache Zanzibar ni kigezo cha kuwalazimisha kufanya hata kile wasichokipenda? Tatu, naomba wale wanaoijua katiba ya Zanzibar kama imeainisha kwamba zanzibar ni nchi ya kiislamu kinyume na katiba ya muungano..!
 
Leo bungeni katika hali ambayo imeshangaza wengi,Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kayanza Peter Mizengo Pinda amejibu swali gumu kirahisi sana kwa maono yangu. Ameliuzwa kuhusu kauli iliyotolewa na viongozi wa kiislamu ,Zanzibar...kauli ambayo iliamuru kukomesha uvaaji wa nguo zisizoendana na uislamu pia wameamuru kukomesha vitendo vya watu kula (hovyo) katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.Mhe, Pinda amedai kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Zanzibar ni Waislamu (hilo silipingi) hivyo suala la sheria na kanuni za kiislamu kutumika siyo hoja. Je,ni sawa kanuni hizi zisizokuwemo kwenye katiba yetu kutumika huku ikijulikana nchi haina dini? Pili , Wakristo kuwa wachache Zanzibar ni kigezo cha kuwalazimisha kufanya hata kile wasichokipenda? Tatu, naomba wale wanaoijua katiba ya Zanzibar kama imeainisha kwamba zanzibar ni nchi ya kiislamu kinyume na katiba ya muungano..!
Sina uhakika kula hovyo kukoje hasa ila najiuliza kula kwangu kunakuhusu nini wewe uliyefunga?? Huwa sipati jibu pengine leo naweza kupata jibu hapa hebu nisaidieni jamani yaani nile mimi namdhuru vipi aliyefunga??
 
hvi kweli tumekomboka? miaka 50 uhuru wa nini tulio nao? je tunaendeshwa kidini ama kisiasa?

nisivae nguo fupi kama ndo zinazonata na mwili nifanyeje? kwani wewe kunitazama tu watamani? jamani basi hawa wenzetu wanaimani za kushikiwa na wala si za kweli manake nijuavyo mimi majaribu hayana budi kutokea ila wapaswa uyashinde. na pia imeandikwa ole wake yeye aletaye makwazo kwa mwenzie so wewe shinda jaribu huyu aliyekuletea makwazo mwache ole uwe wake.
 
huu uzi muelekeo wake si mzuri upo kidini zaidi, hata ivo mtoa mada tupe mtazamo wako basi ambao unahisi ungekufurahisha kuusika,
 
hvi kweli tumekomboka? miaka 50 uhuru wa nini tulio nao? je tunaendeshwa kidini ama kisiasa?

nisivae nguo fupi kama ndo zinazonata na mwili nifanyeje? kwani wewe kunitazama tu watamani? jamani basi hawa wenzetu wanaimani za kushikiwa na wala si za kweli manake nijuavyo mimi majaribu hayana budi kutokea ila wapaswa uyashinde. na pia imeandikwa ole wake yeye aletaye makwazo kwa mwenzie so wewe shinda jaribu huyu aliyekuletea makwazo mwache ole uwe wake.
leo nimekushusha hadhi yako
 
kuwa wengi haisaidii katika maendeleo, Tanzania inataka watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kuamua mambo ili kuiletea maendeleo nchi hii na siyo wingi wa waumini wa dini fulani tena majua na masikini wakutupwa.
 
Hata wangekuwa asilimia 99.9 bado tanzania haina dini labda wasubiri muungano ukivunjika
 
Binafsi sioni tatizo la kukiuka haki za binadamu hata kama ni wachache kwa kisingizio cha imani.Kwani mimi nikitafuna biscuit nawe umefunga ni lazima utamani kula? Na kama utatamani hautakuwa umetenda dhambi? Mi nadhani hakuna uvumilivu wa kidini maana kama dini yangu inaniruhusu kula kila nikijisikia njaa pahala popote, ni kuingilia uhuru wa dini yangu endapo utanikataza nisifanye hivyo. Anyway,huenda hili suala ni dogo kama alivyosema Pinda lakini naomba nipate mitazamo ya Watanzania wenzangu pengine sielewi vizuri kuhusu uvumilivu wa kidini,haki za binadamu,kuheshimu katiba ya Muungano n.k Naamini tutaeleweshana kwa hoja na siyo kwa vioja.
 
Tuache upotoshaji. kauli ya mh. Msigwa sio kauli ya CHADEMA. Mh.. Msigwa sijui kama anayaelewa mazingira ya Zanzibar na hata yale ya Mafia. Na sina uhakika kama Mh msigwa anaishi na wakristo tu huko Iringa. Mh Msigwa asijaribu kuwagombanisha watu wa dini mbalimbali kule Zanzibar. Tangazo hilo limetolewa bila shaka kuwapa taarifa watu wageni wa taratibu za mwezi wa Ramadhani kama kina Msigwa. Kwa wenyeji wa dini zote Zanzibar hili sio geni na wala haliwapi shida.
 
Unaonaje kama kwenye sensa kingekubalika kile kipengele cha dini ! Ni kujifanya kujua zaidi ,hata huku Tanganyika waislamu ni 85% waliobaki wanaabudu masanamu au hawana kabisa.
mimi ni mmoja wa ambao hawana ndio maana najisikia niko huru kwani hata nikichangia huwa siwezi kuegemea upande wowoyepili siwezi kugombana kwa tamaduni za watu ninawaacha watumwa wa fikra na kitamaduni walumbane na sasa wanakaribia kuivuruga nchi.
 
hizo takwini kazipata wapi waziri mkuu wakati serikali yenyewe imeondoa kipengele cha dini kwenye sensa!
 
Unaonaje kama kwenye sensa kingekubalika kile kipengele cha dini ! Ni kujifanya kujua zaidi ,hata huku Tanganyika waislamu ni 85% waliobaki wanaabudu masanamu au hawana kabisa.

Tuko hapa kujadili masuala muhimu, I suspect umefunga na u just Insult those who do nat believe in Muslim? Ndo dini yako inavyokuelekeza?
 
hvi kweli tumekomboka? miaka 50 uhuru wa nini tulio nao? je tunaendeshwa kidini ama kisiasa?

nisivae nguo fupi kama ndo zinazonata na mwili nifanyeje? kwani wewe kunitazama tu watamani? jamani basi hawa wenzetu wanaimani za kushikiwa na wala si za kweli manake nijuavyo mimi majaribu hayana budi kutokea ila wapaswa uyashinde. na pia imeandikwa ole wake yeye aletaye makwazo kwa mwenzie so wewe shinda jaribu huyu aliyekuletea makwazo mwache ole uwe wake.

Mbona hata baadhi ya makanisa wanakataza nguo zisizo na heshima? kwa hiyo hayo makanisa hayana imani?
 
Nishaenda kanisani nikaona jamaa anasujudia sanamu ,nishaenda kwa mabaniani nako kuna sanamu wanalisujudia ,huko kama si kuabudu ni kitu gani ?
 
Hili ndilo tatizo la kuamini katika lugha za watu yaani kiarabu,watu wakisoma hawaelewi wapi imeandikwa kuwa chakula kisipikwe na wasio waislamu wasile wakati wa mfungo?Msigwa alichofanya ni kutetea Watu wasiofunga kipindi hiki maana imani hailazimishwi..Hivi tuwalazimishe watalii,wagonjwa,wasio waisilamu na vikongwe kufunga kufunga?

Tfikilie sawasawa tuache mihemko ya kidini na kisiasa katika mambo ya msingi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom