Tuache upotoshaji. kauli ya mh. Msigwa sio kauli ya CHADEMA. Mh.. Msigwa sijui kama anayaelewa mazingira ya Zanzibar na hata yale ya Mafia. Na sina uhakika kama Mh msigwa anaishi na wakristo tu huko Iringa. Mh Msigwa asijaribu kuwagombanisha watu wa dini mbalimbali kule Zanzibar. Tangazo hilo limetolewa bila shaka kuwapa taarifa watu wageni wa taratibu za mwezi wa Ramadhani kama kina Msigwa. Kwa wenyeji wa dini zote Zanzibar hili sio geni na wala haliwapi shida.
Mbona hata baadhi ya makanisa wanakataza nguo zisizo na heshima? kwa hiyo hayo makanisa hayana imani?
hvi kweli tumekomboka? miaka 50 uhuru wa nini tulio nao? je tunaendeshwa kidini ama kisiasa?
nisivae nguo fupi kama ndo zinazonata na mwili nifanyeje? kwani wewe kunitazama tu watamani? jamani basi hawa wenzetu wanaimani za kushikiwa na wala si za kweli manake nijuavyo mimi majaribu hayana budi kutokea ila wapaswa uyashinde. na pia imeandikwa ole wake yeye aletaye makwazo kwa mwenzie so wewe shinda jaribu huyu aliyekuletea makwazo mwache ole uwe wake.
kama hali ni hii maana maeneo mengi sasa duniani yanavurugika kwa sababu ya hizi dini,natamka kwa kujiamini mungu yupo atazidi kuwepo lakini hakuna uhusiano wowote wa mungu na hiki kitu kinachoitwa dini zaidi naona zinachangia kuongeza maovu ulimwenguni.hebu jiulize kadiri siku zinavyozidi kwenda wahubiri wa kiislamu na kikristu wanaongezeka na kwa kadiri wanavyoongezeka ndiyo dunia inavyozidi kuharibika.dini ni saccos kama zingine.
Mbona hata baadhi ya makanisa wanakataza nguo zisizo na heshima? kwa hiyo hayo makanisa hayana imani?
Hiyo imeandikwa kwenye vitabu vyenu sisi vyetu vinasisitiza mtu avae kwa kujistiri,sio avae anavyotaka'halafu hii amri yakufunga mahotel ni amri iko nchi zote karibu zenye idadi kubwa ya waislam jaribu kutembea uone'
Wana- JF,
Hivi punde katika kipindi cha maswali na majibu Waziri Mkuu, Pinda ameulizwa swali na Mh. Mchungaji Msigwa kuwa huko Zanzibar kuna tamko limetolewa na kiongozi mmoja kuwataka wafanyabiashara wote wa mahoteli kutokuuza chakula hasa wakati wa mchana kwa vile waislamu wako katika mfungo wa Ramadhani. Mbali na hilo kuna pia agizo kuwa wanawake wasivae nguo fupi katika kipindi hiki kwa vile wanawatamanisha wanaume.
Aidha, Waziri mkuu amesema amri ya kutokuuza chakula huko iko sawa kwa vile mazingira ya huko zanzibar yanaonesha kuwa asilimia kama tisini na tisa (99%) ya wananchi huko ni waislamu. Licha ya kuingilia haki za watu wengine na imani za watu wengine, naona kwa mtazamo wangu suala hili halikutakiwa kujibiwa namna hiyo na Waziri Mkuu.
Naomba wenye takwimu watuambie kama kweli 99% ya wananchi wote ni waislamu na kama watu wengine wanaoishi huko hawana haki kwa mujibu wa Katiba.
Nawasilisha.
Unaonaje kama kwenye sensa kingekubalika kile kipengele cha dini ! Ni kujifanya kujua zaidi ,hata huku Tanganyika waislamu ni 85% waliobaki wanaabudu masanamu au hawana kabisa.