Pinda: Hakuna haja ya kwenda kujifunza Kilimo Asia

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Mara nyingi sana huwa napata shida sana katika kujua Taifa letu linahitaji katika Ustawi wake, Waziri Mkuu wa Tanzania Mh pinda hivi karibuni alikuwa katika Mataifa mbalimbali ya Asia kwa ajili ya kwenda kujifunza kilimo, Na kuitikia wito wa Kilimo Kwanza,

Tanzania Kipindi cha baba wa Taifa yaani Mwalimu Nyerere alikuwa na Dira maalumu ya Taifa hili na Pia aliweza kufungua Vituo mbalimbali vya utafiti wa kilimo, Kama Chuo cha Utafiti UYOLE, Mwanza, na Lushoto, na shemu mbalimbali katika Taifa la Tanzania, Lakini katika Miaka ya 1992-1997 Vituo vyote vilifungwa na kukosa pesa kabisa katika Tafiti zao na kuondolewa wanasanyasi wote,

Katika Msukumo wake Mwalimu Nyerere aliweza pia Kufungua Chuo cha Kilimo cha SUA, yaani SOKOINE AGRICULTURE, Na pia chuo hiki ni miongoni wa vyuo ambavyo vinatoa mchango mkubwa sana katika Taifa la Tanzania na hata kusini wa Jangwa La sahara, Kama kweli Taifa letu lina Nia ya dhati ya kuendelea kilimo basi mambo yafuatayo yafanyike

1: Kujua na kutambua mchango wa Wataalamu wa Ndani yaani Taifa la Tanzania Chuo cha Sokoine University, Kuwatumia na kujua kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa katika utafiti wao

2. Serikali kuweka bajeti kubwa katika Tafiti za Kilimo na kuwekeza katika rasilimali watu yaani wataalamu wa ugani na kutoa motisha kubwa katika pesa na kuwekeza kwa hali ya juu

3. Kurudisha wataalamu wote wa Taifa hili walio nje ya Tanzania na kuwapa mishahara mikubwa katika taifa la Tanzania

4. Kutumia Tafiti mbalimbali ambazo zipo katika maktaba za vyuo mbalimbali za Taifa la Tanzania na sehemu mbalimbali

5. Kuwekeza katika sekta binafisi na kutoa incentives binafsi na kuona kuwa wanaweza kufanya mambo yao kwa kupata support ya Serikali

6. Kuwekeza pesa nyingi sana katika chuo cha SOKOINE na kuona watu wa ndani na maarifa yao yanatumika ipasavyo.

7. Kuimarisha maeneo yote ya sekta mbalimbali kama Barabara, Pembejeo za kilimo, na idara ya mifugo.

8: Hata kama watu toka Korea Kusini wakija watatumia tafiti zetu za ndani katika kuangalia na kusoma mazingira ya hapa ndani.

9:Wafanyakazi wa Idara ya Kilimo wapewa motisha katika kubuni mbinu mbalimbali katika kuendeleza kilimo chetu

10: Kuwekeza katika kilimo ambacho ni sustainable agriculture

NB: Hakuna haja ya kwenda kujifunza South Korea , Indonesia na Taiwan wakati humo ndani tunaweza kufanya mambo makubwa sana, Kipindi cha ujamaa watu na Taifa lilikuwa katika hali nzuri sana kuliko hali ilivyo hivi sasa
Nataka kutoa machozi sasa hivi
 
Alikwenda kupunga upepo wa asia ambao bado haujakuwa poluted sana na virus wa ufisadi,unafikiri kuna kingine kipya mkuu rather than refreshing?
 
Alikwenda kupunga upepo wa asia ambao bado haujakuwa poluted sana na virus wa ufisadi,unafikiri kuna kingine kipya mkuu rather than refreshing?
Nashindwa kujua kwanini alikwenda huko maana Tanzania kila kitu na tafiti kibao za kufanyia kazi kuliko kwenda huko na watu hawa watakuja tu kufanyia kazi tafiti zetu ambazo watu au Watanzania walifanya kipindi chay nyuma.. Sasa sijui tufanye nini maana naona kama vile hakuna mtu dhabiti wa kufanya mambo haya mzee wangu
 
Sasa hizi kauli za kila wakati Mara kilimo kwanza mara utigo mgongo kweli tuna nia ya dhati kabisa
 
"Pinda: Hakuna haja ya kwenda kujifunza Kilimo Asia"
Punctuation iko sawa?
Nimeelewa kwamba kauli imetolewa na Pinda, au ndivyo ulivyomaanisha?
 
"Pinda: Hakuna haja ya kwenda kujifunza Kilimo Asia"
Punctuation iko sawa?
Nimeelewa kwamba kauli imetolewa na Pinda, au ndivyo ulivyomaanisha?
Nimefanya hivyo makusudi kabisa, maana nilitaka watu wengi waje hapa na mawazo yao ili tupeleke voice ambayo ipo strong sana
 
Mkuu Josh,

Kwanza nikushukuru kwa observation yako. Kusema kweli nami nimetatizwa sana na ziara ya Pinda huko bara la Asia, kwani nilimtegemea kuwa practical zaidi katika hili kwa sababu nafahamu uelewa wake katika kilimo sio wa kitabuni bali ni ule wa kivitendo, amezaliwa na kukulia katika utamaduni wa kilimo jambo ambalo amekuwa akilibainisha katika kauli zake.

Mwaka 2006 Balozi wa Indonesia nchini alitembelea Mbeya, kama kawaida ya viongozi wetu katika utegenezi wa misaada toka nje, walichojiandaa kwa ugeni huo ni orodha ya maombi ya misaada katika kilimo ikiwemo kile cha umwagiliaji. Katika kukoleza ushawishi wao kwa Balozi huyo, walimtembeza kwenye mashamba ya umwagiliaji ya Mbarali na Igomelo wilayani Mbarali.

Alichofanya Balozi yule, kwa mtu mwenye akili timamu ilikua aibu ya mwaka, lakini kwa viongozi wetu lilikuwa jambo la kawaida. Ni kwamba baada ya kutembelea yale mashamba na kujionea mwenyewe mito ikitiririsha maji yanayopotea bila kutumia alijibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kumwela kuwa, siku ile ndio ilikuwa mara yake ya kwanza, tangu azaliwe kuona mashamba makubwa ya kilimo cha umwagiliaji kama yale yaliyoko wilayani Mbarali!!!

Mshangao wake wa pili ni kuona maji yakitiririka na kupotea bila kutumika kwa kilimo au ufugaji samaki.

Kwa ufupi, kama alivyowahi kusema marehemu Kolimba, ni kwamba nchii hii imekosa viongozi wenye dira. Hivi wakati wazee wetu wanazalisha chakula cha kujitosheleza mwaka mzima walifanya ziara gani ya mafunzo, huu ni WIZI mtupu, na hiyo KILIMO KWANZA yao ni ajenda ya uchaguzi wa mwakani, wanaudhi sana kwa kweli.
 
Nenda Sua ukaone au kuongea na watu waliboboea katika kilimo na tafiti zao bado napata shida sana katika kujua kuwa Taifa la Tanzania halina nini kwa sasa.
 
Back
Top Bottom