Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Tanzania ni moja ya Nchi Duniani ambayo imebarikiwa na kila kitu.
Tanzania imebarikiwa Madini ya kila aina, pongezi kubwa kwa Serikali na Wizara ya Madini kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi kwenye utafiti na sasa Madini adimu kabisa ya Lithium yamegunduliwa na utafiti unaendelea.
Tanzania tumebarikiwa ardhi ya kutosha, tumebarikiwa mito ya kutosha, maziwa, Chemchem za kutosha na bahari pia.
Kama yakifanyika mapinduzi ya Kilimo, zao gani ambalo halistawi Tanzania? . Mipango mikubwa ya Kilimo ipelekwe Njombe, Mbeya, Rukwa, Kigoma, etc, ili Kilimo cha kisasa chenye uhakika cha kutokutegemea mvua kikafanyike..
Pengine ni muda sahihi wa kuanza Mipango ya baada ya miaka 20 ijayo kutumia bahari yetu kwa Kilimo. Yes inawezekana, maji ya bahari ikawa chanzo cha maji ya kutumia majumbani, viwandani na mashambani. Kama imewezekana kufanya miradi mikubwa ya SGR, inawezekana kutoa maji ya Bahari kutoka Tanga kwenda Kigoma.
Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania.