Pinda aendelea kulalamika!

Nanukuu “Yupo Waziri fulani alinifuata na kuniomba nimsaidie ili magari ya mwanaye yaliyokamatwa yaweze kuachiwa, nilimkatalia na kumuhoji kwa kuwa ni mwanao ndio aruhusiwe kufanya biashara haramu?” mwisho wa kunukuu kauli ya w/mkuu pinda.

Hii ndio serikali ya kikwete na hawa ndio watendaji wake wakuu. Kazi kweli kweli kama waziri mkuu huwezi kumadabisha mtu kazi yako nini? Unatawala au unaongoza. watanzania tunahitaji mabadiliko makubwa ya utawala.
 
Kinachoendelea Tz kiutawala ni jambo la kumsikitisha kila mtu makini. Ni kama mfumo wa dola umekufa. Kila mtu anatoa tamko, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba hata wale ambao tunadhani wana mamalaka, nao wanaonekana hawana nguvu na wanalalamika kama raia wa kawaida. Ukweli ni kwamba, kwa mfumo wetu wa kiutawala, rais wa nchi ndiye mwenye mamlaka yote. Hao wengine kama Waziri Mkuu hawana mamlaka ya kufanya kitu chochote tofauti na utashi wa rais.

Matokeo yake ni kwamba rais akiwa mchapakazi, mfumo wote unakuwa hai. Kinyume chake, rais akilala, mfumo wote nao unaenda likizo, na hapo ndipo tunaona watu wakijichotea rasilimali za nchi bila bughudha, huku wale ambao wanapaswa kuwaadabisha wakiishia kulalamika tu. Pinda sijui sana uwezo wake kiutendaji. Ninachojua ni kwamba si fisadi kama hao wenzake.

Pamoja na hayo, hata angekuwa mkali kama Sokoine, angeishia frustration tu, na hata kupoteza nafasi yake, kwa sababu bosi wake ni mtu wa maneno tu bila utendaji wowote. Hilo ni moja. Pili, tusisahau kwamba Pinda ni mwana-CCM, na hao vigogo wanaoibia nchi nao wengi wao ama ni wana-CCM au ni maswahiba wa karibu na watawala wa CCM (ambayo m/kiti wake ndiye rais).

Tunarudi kule kule. Kwa maslahi ya kisiasa, Pinda na watendaji wake hawawezi kuwafanya lolote hao wahujumu uchumi kwa kuwa wanatoa mchango wa maana ndani ya chama. Naamini watu hao wanafahamika vizuri, tena kwa majina, lakini ndo hivyo tena. Zaidi ya yote ni kwamba hii nchi imeshaoza kwa rushwa na ufisadi.

Ingawa hawa wahujumu wanafahamika, wale wanaopaswa kuwachukulia hatua wanawaogopa kwani hata wenyewe nao si wasafi. Wapo mmoja mmoja wasafi lakini wengi ni wale wale. Je, nani amfunge paka kengele? Tumuombe Mungu awamu ijayo tupate rais mchapa kazi. Kinyume na hapo hakuna njia ya mkato, inabidi tuwe tu wapole.

Mkuu inasikitisha sana. Wazee wa CCM asili walipenda Pinda awe PM kwa kuwa ni mtu makini, lakini sasa hivi inaonekana kuwa umakini wake upo kwenye kuongea kuliko kwenye utendaji.

Mpaka sasa sielewi ana maana gani kusema mawaziri na watoto wao wanahusika na magendo ya sukari. Anajua kabisa na kusema hadharani lakini hakuna analofanya. That is disgrace Mr PM, ni bora kukaa kimya kuliko kuliko kusema namjiu mwizi halafu unakaa naye kwenye baraza la mawaziri. Unakubali kabisa kwenye baraza la mawaziri kuna watu hao yet unaendelea kukaa nao what should we expect from you and your cabinet?
 
Huyu nae ni mzigo tu, hana faida yeyote. Mi nashngaa sana kwanini Rais asimtupilie mbali.
 
Natamani Pinda angekuwa karibu yangu, nimzabe kibao cha nguvu ili hizo pipes zilizoziba kwenye ubongo wake zizibuke aweze kufikiri vyema zaidi. *&^^%%$%$$###@#@@ zake!
 
Lakini utakuta pamoja na ujinga wote huo magamba, watu wazima hasa vijana bado wanaambatana na kukishadadia kweli.
 
Waziri mkuu ameendela kulalamika kwamba tatizo la uvushaji wa chakula na sukari kwenda nchi za jirani limekuwa kubwa kwa kuwa kuna baadhi ya vigogo ambapo baadhi ni mawaziri wamekuwa wakijihusisha ktk bishara hiyo ya uvushaji wa bidhaa kwa magendo mipakani.

Mbali na kunihuzunisha imebidi nicheke pia, kwani yeye kama waziri mkuu yuko kwenye nafasi ya kuwashughulikia hao watu badala ya kulalamika hadharani kwa mambo ambayo mbali na kuonyesha udhaifu wake kiutawala anamdhalilisha rais wake kwa kuonyesha kuwa ana wasaidizi ambao ni kama 'wahujumu' uchumi kwa serikali waliyoaminiwa kumsaidia Rais kuiongoza.

Hiv tatizo la Pinda ni lipi linalomfanya mara nyingi awe mtu wa kulalamika badala ya kufanya maamuzi?

Yaani Pinda amekuwa kama vile hana meno. Sikiliza sentensi yake:
“Yupo Waziri fulani alinifuata na kuniomba nimsaidie ili magari ya mwanaye yaliyokamatwa yaweze kuachiwa, nilimkatalia na kumuhoji kwa kuwa ni mwanao ndio aruhusiwe kufanya biashara haramu?”
“Sikumsaidia na nasisitiza Mkuu wa mkoa endelea na uzi huo huo hadi kukomesha biashara hii,” alisema Pinda.

Pinda ana uadilifu ndani yake ila inaonekana kuwa hana mamlaka ya kuwashughulikia hao wahujumu uchumi na wezi.
 
Yaani kama vile atokee Kifimbo Cheza, amtandike bakora....tena mbela ya hadhara!!!
 
4.jpg
 
Back
Top Bottom