Pinda aendelea kulalamika!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Waziri mkuu ameendela kulalamika kwamba tatizo la uvushaji wa chakula na sukari kwenda nchi za jirani limekuwa kubwa kwa kuwa kuna baadhi ya vigogo ambapo baadhi ni mawaziri wamekuwa wakijihusisha ktk bishara hiyo ya uvushaji wa bidhaa kwa magendo mipakani.

Mbali na kunihuzunisha imebidi nicheke pia, kwani yeye kama waziri mkuu yuko kwenye nafasi ya kuwashughulikia hao watu badala ya kulalamika hadharani kwa mambo ambayo mbali na kuonyesha udhaifu wake kiutawala anamdhalilisha rais wake kwa kuonyesha kuwa ana wasaidizi ambao ni kama 'wahujumu' uchumi kwa serikali waliyoaminiwa kumsaidia Rais kuiongoza.

Hiv tatizo la Pinda ni lipi linalomfanya mara nyingi awe mtu wa kulalamika badala ya kufanya maamuzi?
 
2+(2).jpg

Napita tu nitacomment baadaye
 
na hawa jamaa wanajua 'kukamata ulabu' aisee usiombe. Nimeipenda hasa hapo premier anaposikilizia utamu kwa mbaaaaaaaaaaaaaaaali!
 
This is why there has been an increasing sense of nostalgia for EL among the public. Despite a few Achilles heels, EL was inclined to live up to his commitments and had a less propensity to talking.
 
Waziri mkuu ameendela kulalamika kwamba tatizo la uvushaji wa chakula na sukari kwenda nchi za jirani limekuwa kubwa kwa kuwa kuna baadhi ya vigogo ambapo baadhi ni mawaziri wamekuwa wakijihusisha ktk bishara hiyo ya uvushaji wa bidhaa kwa magendo mipakani.

Mbali na kunihuzunisha imebidi nicheke pia, kwani yeye kama waziri mkuu yuko kwenye nafasi ya kuwashughulikia hao watu badala ya kulalamika hadharani kwa mambo ambayo mbali na kuonyesha udhaifu wake kiutawala anamdhalilisha rais wake kwa kuonyesha kuwa ana wasaidizi ambao ni kama 'wahujumu' uchumi kwa serikali waliyoaminiwa kumsaidia Rais kuiongoza.

Hiv tatizo la Pinda ni lipi linalomfanya mara nyingi awe mtu wa kulalamika badala ya kufanya maamuzi?
Kinachoendelea Tz kiutawala ni jambo la kumsikitisha kila mtu makini. Ni kama mfumo wa dola umekufa. Kila mtu anatoa tamko, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba hata wale ambao tunadhani wana mamalaka, nao wanaonekana hawana nguvu na wanalalamika kama raia wa kawaida. Ukweli ni kwamba, kwa mfumo wetu wa kiutawala, rais wa nchi ndiye mwenye mamlaka yote. Hao wengine kama Waziri Mkuu hawana mamlaka ya kufanya kitu chochote tofauti na utashi wa rais.

Matokeo yake ni kwamba rais akiwa mchapakazi, mfumo wote unakuwa hai. Kinyume chake, rais akilala, mfumo wote nao unaenda likizo, na hapo ndipo tunaona watu wakijichotea rasilimali za nchi bila bughudha, huku wale ambao wanapaswa kuwaadabisha wakiishia kulalamika tu. Pinda sijui sana uwezo wake kiutendaji. Ninachojua ni kwamba si fisadi kama hao wenzake.

Pamoja na hayo, hata angekuwa mkali kama Sokoine, angeishia frustration tu, na hata kupoteza nafasi yake, kwa sababu bosi wake ni mtu wa maneno tu bila utendaji wowote. Hilo ni moja. Pili, tusisahau kwamba Pinda ni mwana-CCM, na hao vigogo wanaoibia nchi nao wengi wao ama ni wana-CCM au ni maswahiba wa karibu na watawala wa CCM (ambayo m/kiti wake ndiye rais).

Tunarudi kule kule. Kwa maslahi ya kisiasa, Pinda na watendaji wake hawawezi kuwafanya lolote hao wahujumu uchumi kwa kuwa wanatoa mchango wa maana ndani ya chama. Naamini watu hao wanafahamika vizuri, tena kwa majina, lakini ndo hivyo tena. Zaidi ya yote ni kwamba hii nchi imeshaoza kwa rushwa na ufisadi. Ingawa hawa wahujumu wanafahamika, wale wanaopaswa kuwachukulia hatua wanawaogopa kwani hata wenyewe nao si wasafi.

Wapo mmoja mmoja wasafi lakini wengi ni wale wale. Je, nani amfunge paka kengele? Tumuombe Mungu awamu ijayo tupate rais mchapa kazi. Kinyume na hapo hakuna njia ya mkato, inabidi tuwe tu wapole.
 
The so called Tanzania PM.
Act wananchi ndo wa kulalamika sio wewe kama hawakuheshimu achia ngazi ukaendelee na mashamba yako ya mahindi na mizinga ya nyuki uliyowekeza kule Mpanda
 
2+(2).jpg

Napita tu nitacomment baadaye

Ndo maana nchi haiendelei, yaani pinda anasema anawajua mawaziri wanaovusha sukari na mahindi, halafu anabaki kulia tuu. Kumbe si ulevi wa madaraka tu, bali hata ulevi laivi, kweli picha huongea zaidi.
 
Waziri mkuu ameendela kulalamika kwamba tatizo la uvushaji wa chakula na sukari kwenda nchi za jirani limekuwa kubwa kwa kuwa kuna baadhi ya vigogo ambapo baadhi ni mawaziri wamekuwa wakijihusisha ktk bishara hiyo ya uvushaji wa bidhaa kwa magendo mipakani.

Mbali na kunihuzunisha imebidi nicheke pia, kwani yeye kama waziri mkuu yuko kwenye nafasi ya kuwashughulikia hao watu badala ya kulalamika hadharani kwa mambo ambayo mbali na kuonyesha udhaifu wake kiutawala anamdhalilisha rais wake kwa kuonyesha kuwa ana wasaidizi ambao ni kama 'wahujumu' uchumi kwa serikali waliyoaminiwa kumsaidia Rais kuiongoza.

Hiv tatizo la Pinda ni lipi linalomfanya mara nyingi awe mtu wa kulalamika badala ya kufanya maamuzi?

Kabla ya yote nakuomba ukaisikilize hotuba ya JK akiongea na wazee wa DSM, baada yahapo ndio useme kwamba nani anamdhalilisha mwenzake! I think masuala mengi sana yanabakia kufanyiwa uamuzi na rais ilhali rais wa sasa inaonekana ni mgumu wa kufanya maamuzi hili linaweza kuwa ndio chanzo cha hata mawaziri wake akiwemo PM kuonekana ni walalamikaji!
 
Kama ba Riz1 hamsikilizi,atafanyeje anabaki kulia,tatizo sio pinda tatizo KATIBA
 
Bora EL wa maamuzi ya kuiba pesa kuliko huyu asiye na maamuzi hata ya kijinga!!!!!
 
Back
Top Bottom