Picha ya leo - Waliopitia JKT enzi hizo itawakumbusha makubwa

sisi ndo tulikuwa wa mwisho kumalizia jeshi kukaa kwa mwaka mzima,tena tulimaliza mwezi may badala ya june,ndo wakaingia wa miezi sita,nadhani hukunielewa vizuri

Nadhani nyie ndio mlikamilisha kwa kuwa sio mwaka tu bali ni wa mwisho kabisa maana waliomaliza 1994 na kendelea mpaka sasa hawakwenda ila kuna vitu mlijifunza kwani waliosoma miaka hiyo kushuka chini walisoma mazingira flani magumu ya boarding lakini pamoja na kula dona maharage lakini wanafunzi walikuwa wana-enjoy sana japo siku hizi watoto wetu wanakwenda shule huku na kachupa ka juice
 
Kila kizazi kina enzi zake, enzi zile kiukweli watu walijifunza mengi, mie nimejifunza kulima matuta nilipoanza form 1 na kuchunga mbuzi na ng'ombe nilipofika A-level pale Mazengo High School kwani kila form 1 na form 5 lazima achunge mbuzi na ng'ombe na kusafisha bwalo la chakula Candid Scope
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo maana hata makanisani hawawezi hata kuimba mapambio kwa kupiga makofi, watoto wa siku hizi, nusu watu, nusu kuku wa kisasa: legelege kweli! unadhani hayo nayo mazoezi? umeshawahi kunywa uji wa moto sana kwenye mistini huku filimbi imeshapigwa? hebu fanyeni basi vijimazoezi japo kidogo vitawasaidia kwenye afya zenu na ukakamavu...leo akidondoka mtu mpaka ije forklift kumnyanyua! kisa legelege: serikali legelege, vijana-legelege; mawaziri -legelege, bunge-legelege, askari-legelege, kila kitu legelege! changamka kijana mtanzania!
 
Ndiyo maana hata makanisani hawawezi hata kuimba mapambio kwa kupiga makofi, watoto wa siku hizi, nusu watu, nusu kuku wa kisasa: legelege kweli! unadhani hayo nayo mazoezi? umeshawahi kunywa uji wa moto sana kwenye mistini huku filimbi imeshapigwa? hebu fanyeni basi vijimazoezi japo kidogo vitawasaidia kwenye afya zenu na ukakamavu...leo akidondoka mtu mpaka ije forklift kumnyanyua! kisa legelege: serikali legelege, vijana-legelege; mawaziri -legelege, bunge-legelege, askari-legelege, kila kitu legelege! changamka kijana mtanzania!

Kijijini kwangu wengi waliokuwa na kilimo na kisasa na wakulima wakubwa walikuwa ni wale standard 8 and seven graduates ambao hawakuwa na nafasi ya kuendelea na masomo. Hivyo wakati wa likizo tukawa tunafanya vibarua kwao na kutuambia tukazane kusoma na kama hatutaendelea tujifunze elimu ya kujitegemea mashuleni kwani tutakuwa wakulima wazuri kama wao.

Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa na bustani yangu ya mbogamboga, vitunguu, nyanya, miwa ambavyo vilinisaidia kupata hela ya kununulia madaftari na fountain pen kwa ajili ya mtumizi ya shuleni. Siku sile hatukutumia hici bic, tulitumia pen cha kuchovya kwenye vidao vya wino, na wino ulikuwa unagawiwa bure shuleni, na hata daftari ikijaa maandishi namwonyesha mwalimu wa darasa au somo anatia sahihi na kuipeleka store ya shule na wananipatia daftari mpya for free. Leo je?

Umesema kweli mtupu leo wengi ni legelege kila mahali, hata akili zimekuwa legelege, kama akili ni legelege nini zaidi kitasimama kama si kulalamika tu? Kulalamika kwingi ni dalili ya watu kuwa legelege, wanataka njia ya mkato bila kutoka jasho. Vijana kukimbilia mjini eti kuna ajira, hatimaye hakuna kinachopatikana na kuishia kuwa watembeza bidhaa barabarani. Je wangetulia vijijini na kulima mazao ingwa ni ya msimu maisha yangekuwa bomba zaidi kuliko yanayojilia mijini.

Umeona hapa JF ukileta mada ya kujadili mambo ya kiakili haina wachangiaji labda mtu kama wewe Mkulima wa Kuku, vinginevyo wengi wapo kwenye mada za mipasho ya matukio na kuhusu watu. Kwa kujadili watu na matukio hakutuletei maendelea na katu hatujaibua mbinu za kujenga hali ya kujiamini katika maendeleo, bali kujadili mada nzito za kutadhmini njia mbadala ya kuyatengeneza maisha yetu mazuri.
 
mkuu stineriga huu ndo ukweli bwana , sometimes naisi hawa jamaa wanastaili kupewa shughuli* za iyo waliyopewa kwani wanastahili . na ndo inayowafanya wajione ni special wakali si tunaona akili yao haina akili , ila wana umuhimu mkubwa sana, ndo wanasabibisha tunakula weekend kwa raha bila hofu yoyote ,( kwa mara nyingine ) big wanajeshi
kila mtu na kazi yake na ni mgawanyo wa kazi
 
Nadhani nyie ndio mlikamilisha kwa kuwa sio mwaka tu bali ni wa mwisho kabisa maana waliomaliza 1994 na kendelea mpaka sasa hawakwenda ila kuna vitu mlijifunza kwani waliosoma miaka hiyo kushuka chini walisoma mazingira flani magumu ya boarding lakini pamoja na kula dona maharage lakini wanafunzi walikuwa wana-enjoy sana japo siku hizi watoto wetu wanakwenda shule huku na kachupa ka juice
nyuma yetu walikuja wa miezi sita,na wale wote tuliokuwa tunatoroka jeshini,tulilipia idadi ya siku zile ulizokuwa umetoroka,mimi nililipia hadi june mwishoni ndo mana hata wale waliokuja miezi sita tuliwaona japokuwa hatukuwa nao anga(bwenu) moja!jeshi ukitoroka,unalipa kwa kuendelea kubaki,wenzako wakiondoka!chezea jeshi wewe,na tulikuwa watoro wengi wa dar,hakuna cha baba wala mama kuja kukutoa,hata kama mzazi wako ni mkubwa fulani!nashukuru sana serikali,mana jeshi limenifanya niweze kuishi popote na kufanya kazi na mtu yoyote!
 
Nipo airtel world wide head office hapa mumbai, yaani technology nayoiona humu ndani na watoto wa 21 yrs old walivyopendeza wanapiga mzigo hawajui cha jkt wala nini na airtel inakuwa vibaya, halafu wabongo tunajivunia kupoteza muda jkt kwa kuweka vichwa chini miguu juu,,, kwa imani yangu best teacher ni experience, exposure and education, hayo mambo ya jkt sijui makutopora ni ujinga na ndio chanzo cha tanzania kuwa ya tatu kutola mwisho kwa umaskini
 
JKT ni mfumo wa nchi za kikomunist za urusi ya zamani, korea kaskazini , uchina cuba etc sisi vi-KOmunist vidogo tuliiga tu, na baadhi ya hizo nchi waanzilish wa ukomunist wameacha hizo JKT sababu wameona hazina manufaa kwao. Urusi sasa wameacha hiyo JKT isiyo na faida, hizo JKT hazijawapa maendeleo ya kiuchumi wala ya kijamii sababu bado hizo nchi kuna mafisadi wengi tu.

nchi za kibepari kama usa na uingereza, ujerumani hawakuwahi kuwa na JKT na bado wana maendelao makubwa na ufisadi ni mchaChe kuliko hizo nch za kikomunist zilizokuwa zinafanya JKT.

na ni kweli kwamba hizo nchi zilizokuwa za kikomunist na zinafanya JKT zipo nyuma kimaendeleo ya kiuchumi na kijamii na ufisadi umejaa kuliko nchi za kibepari zilizokuwa hazifanyi JKT.

ondoeni mawazo mgando na ya kale embu tutoleeni huo utumbo JKT hauna manufaa yoyote, labda ni sehemu nyingine mafisadi mnataka mpeleke pesa mkazile!!

Hapo kwa red umechemka! JKT tulii-import toka Israel! na siii huko unaposema!

na nchi za kibepari zoote! vijana wanaenda jeshini hadi dakika hii baada ya kumaliza High School tena wanaenda jeshi la kweli sio kama JKT wanakuja wanamaji, marine (wale the best wanaajiriwa kabisa na jeshi) huendi chuo bila kupita jeshi! hadi sasa! na in event nchi inaenda vitani hao vijana wanapigana mstari wa mbele!

Kuhusu maendeleo sasa hivyi China wako mbali kwa technology zote unazo zifahamu, na ni tajiri kulko USA and infact USA wamekopa China as we speak!

Unapoongelea jeshi kwa hizo nchi unazo zitaja unaongelea ujana wa vijana wa nchi husika! enzi za JKT vijana tuliunganishwa tukawa wamoja sasa hivi watu wa aina yako huna msaada wowote kwa taifa zaidi ya kulalamika kila kukicha! mmegawanywa na siasa za kijinga sana sana ligi ya uingereza ndiyo mnayojua!
 
Mpwa nimefurahi sana sana kwa kunikosoa kwa hoja, nimejifunza pia na mimi kutoka kwako, hakuna kitu kizuri kama kuona kuwa watu wengine wanasoma comments zako, inatia faraja, hata hivyo Mpwa, si kila kitu lazima kiende sawa kwa kila wakatai, kuna nyakati ambazo mawazo mbadala na maono yaweza kutofautiana. Nimekuelewa nami naahidi kuendelea kutoa comments ambazo utaendelea kuzisoma kwa amani. Haya tukutane kwenye maandamano basi pale Mabibo mie nshamuaga shemeji yako na akzini nimesingizia ugonjwa (kidding)
Nlikua naheshm sana comments zako, umenidissapoint sana, just for the record, hii nchi inatumia syllabus ya muingereza combined na ya canada, kwa sasa inaboreshwa zaidi kutumia syllabus za nchi nyingine pia,,,

In short kila unachokiona kwny mazoezi kinafanywa na hzo nchi zinazotumia satellites na drones,,

Pia, hata ukitumia satellites na drones then ukawa na weak land force, huwezi kushinda vita, infantry lazma wakamate maeneo, waweke ngome, kwa ajili ya phases of wars zinazofatia.., sasa ukiwa na infantry ronyo ronyo wataweza haya mambo?
 
kila mtu na kazi yake na ni mgawanyo wa kazi
mgawanyiko wa kazi ???? haaaaaaaaaaaaaais this natural selection ?? unadhani wote hawapendi kuwa mawaziri ??? unadhani watu wanapenda kulala macho wanankimbia wakati wana wake ??? Mwanaweja ni kwamba kila mtu anajipachika pale anapofiti , sio sahiihi kuwa dharau ila sio mbaya kuongea ukweli , TUMIA AKILI YAKO VIZURI KAMA NI MVIVU WA KUTUMIA NGUVU
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaa., mkuu kumbe una huruma eeh!! Sure mkuu tunahitaji kuwahurumia those poor misfortuned..
sure man , hakuna mtu naependa kulala nje huku anakimbia usiku wakati na mke , those are misfortuned , wanastahili huruma yetu bwana , sema wanauzi sana wakiwa kwenye ivyo vitenge vyao wanajiona waop ndo dunia nzima, mimi nliwalaza ndani wiki zima, mkuu wa kikosi nliongea nae , yaani walihangaika mpaka wakakoma kuchezea watu wasiowajua
 
Namkumbuka Babu wa Vibwende. OP Program ya Chama 832 KJ mpooooo? Enzi za Col.Meena, Dr Omar (Maj.), Maj Mwakitosi, Sgt. Manzani, Cpl Nyundo, Sgt Basekana, Sgt Sahani, Maj Lugaimukamu, RSM Kitomari na wengineo. Tukumbushane

Du , vijana mmenikumbusha mbali sana.
Miaka hiyo Mkuu wa kikosi-Makutupora Maj Mwakanjuki(na beret yake),Mafunzo ya kivita Capt Chale , RSM(Regimental Sergent Major) Kufakunoga-alikuwa balaa tupu!

Koplo Mwiba-mwiba kweli kweli-afande wa adhabu tu!
MP Simkoko(tall kweli kweli huyu)
 
nope but i ca heal your broken kneel , unaswali zaidi ???? ok anyway ma pilot hawasimamii vichwa kama hao kabora basa

ulisema kazi ya jeshi any fool can do si ndio? Nimekuuliza wewe super genius, can u fly a jet fighter? Jibu ndio au hapana
 
kwani jet fighter pilots wanaanzia wapi? na nani alikwambia hawasimamii vichwa?? Nenda monduli pale afu ulizia pale querter guard, kubeba dunia ndio nn, then utaoneshwa...,
 
Mpwa nimefurahi sana sana kwa kunikosoa kwa hoja, nimejifunza pia na mimi kutoka kwako, hakuna kitu kizuri kama kuona kuwa watu wengine wanasoma comments zako, inatia faraja, hata hivyo Mpwa, si kila kitu lazima kiende sawa kwa kila wakatai, kuna nyakati ambazo mawazo mbadala na maono yaweza kutofautiana. Nimekuelewa nami naahidi kuendelea kutoa comments ambazo utaendelea kuzisoma kwa amani. Haya tukutane kwenye maandamano basi pale Mabibo mie nshamuaga shemeji yako na akzini nimesingizia ugonjwa (kidding)

Dont expect me there, but i might be there!
 
Back
Top Bottom