Picha hisani ya Michuzi blog
Licha ya mabomu na vitisho vya serikali, waandamaji Zanzibar wangali ngangari kudai maoni yao kuhusu serikali ya Muungano. Haki ya wananchi si kitu cha kuporwa kirahisi siku hizi. Bora tu kusikiliza madi yao na kuyafanyia kazi, lakini nguvu si lo lote na si chochote kwani ni kuchochea zaidi vurugu. Madai yao hayajasikilizwa muda mrefu na kudharaulika kila walipotaka kutoa maoni yao, matokeo leo ndiyo haya.
Tusiwasingizie viongozi wa dini yao kwa kila ajenda, hili la Muungano ni kitendawili kilichotegwa, kufumba na kufumbua ipo siku wanaotetea kwa nguvu zote wataumbuka.
Ndoa za kushinikizwa zina matatizo mengi sana tofauti na ndoa za hiari ya wanandoa kwani kwa maamuzi yao sahihi wamekubaliana kwa ridhaa yao kufunga ndo, lakini hizi za mkeka matokeo ndo hayo.
Naomba Mungu aepushie mbali,Shetani ameanza Tanzania baada ya kuua sana SYRIA.Nakubaliana nawe, kwani picha hizi ni maandamano yanayoendelea baada ya mabomu usiku kucha asubuhi wameamkia maandamano. Wapeni haki yao wanayodai, kuendelea kuwanyima haki yao ni kuchochea machafuko kama haya tunayoshuhudia sasa. Somo la urahia kuhusu sheria na haki ya kuhoji muungano lililotolewa na Tundu Lisu linafanya kazi yake, na hapa wameshaamua hadi kieleweka, hakuna kurudi nyuma.
Sasa kama katiba yao tayari inatambua kuwa Zanzibar ni nchi, wanachodai ni nini?...Katiba ya Zanzibar Toleo la 2010 inatambua kwamba, "Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano." ...
Mkuu sema kwamba tatizo ni viongozi wa Dini zao wanaowafungua macho na wala siyo kuwapaka matope.
Kinachotokea Zanzibar ni FULL UDINI. Udini at its highest level. PERIOD. Viongozi (CCM) waliushabikia, wakauendekeza, na hata kuufadhili kwa maslahi mafupi ya kisiasa sasa mambo yameharibika - na bado.
Tunaisikia Boko Haram ee? Tunaisikia Al-Shabaab ee? Sasa iko mlangoni mguu mmoja ndani. Matokeo ya viongozi kutoshughulikia matatizo kwa wakati kwa hofu ya kuwaudhi akina fulani ndio haya.
Matokeo ya viongozi kusimama majukwaani tena majukwaa rasmi ya kitaifa kama Bungeni na kuanza kushadadia udini kama turufu ya kisiasa dhidi ya wengine kwa faida ya kulinda maslahi ya chama chetu badala ya kuzungumzia ukweli halisi ndio haya.
Naomba niwatahadharishe viongozi wa CCM ambao kila kukicha hawaachi kukihusisha CHADEMA na udini usiokuwepo lakini katu hutawasikia wakizungumzia makundi yaliyo dhahiri kwa udini kama hili la uamsho huko Zanzibar! Mnakoipeleka nchi siko! Kikundi hiki na mengineyo kadhaa hasa kupitia mwamvuli wa nyumba za ibada yamelelewa kwa muda mrefu na CCM hususan huko Zanzibar, yamekuwa, na sasa yanajipambanua kwa rangi zao halisi - eti Dola ya KIISLAM YA Zanzibar!
Kama wengi wasemavyo, nchi hii itaingizwa kwenye machafuko hususan ya kidini na CCM na si vinginevyo - yetu macho.
BABA WA TAIFA JULIUS KAMBARAGE NYERERE, Upo wapi Mwalimu wa nchi hii,Baba yetu ungekuwepo leo hii NENO LAKO MOJA TU LINGEBADILISHA NCHI HII.
Haya uliyasema na kuyatabiri mda mrefu sana. NAKUMBUKA WAKATI WA UCHAGUZI 1995 ULIONGEA MAMBO MENGI KUHUSU MUUNGANO. Leo hii yanatokea hakuna anayeweza kukumbuka uliyosema. NARUDIA....SEMA NENO MOJA TU HUKO ULIKO LIBADILISHE NCHI YETU.
...Katiba ya Zanzibar Toleo la 2010 inatambua kwamba, "Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano." Na huu ndi ukweli wa kihistoria, siyo?! Tatizo lisilotatuliwa ni kwa nini Tanganyika haitaki kuwa na katiba yake na kuitambulisha Tanganyika kwenye muungano (?)! Huu ni mshangao unawafanya baadhi ya Wazanzibari kudahi kwamba Tanganyika ina "agenda" ya siri nyuma ya muungano wa kulazimisha!
Cha ajabu na cha kusikitisha; CCM ilipowaruhusu Wazanzibari kuanzisha mchakato wa kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI) ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) walidhani itaishia hapo...; walijidanganya hata pale walipokubali kuanzisha mchakato "ghushi" wa katiba kwamba watawabana wananchi wa Zanzibar wasiujadili muungano, hasha; wameshindwa! Nadhani wameweza kuwatia "uzezeta" wananchi wa bara kwa kuwa watu wa Tanganyika wamezowea kuburuzwa na kwao muungano hawaujui kwa jinsi wanavyoujua wananchi wa Zanzibar. Zanzibar wanajitambua na wanajijua; Watanganyika wamejishahau kama "misukule" au "mandondocha" waliyechukuliwa na wachawi na kufanywa "mazemule."
Nadhani hakuna asiyeona harakati za utambuzi na utambulisho wa Wazanzibari; na mara zote kunapotokea hamkani ya kisiasa visiwani wanaotafuta sababu ya kutuliza gafugafu la joto la kisiasa huwa ni Watanganyika kwa kutumia nafasi yao kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kama alivyofanya Mwalimu Nyerere...wanafunika "kawa" mwanaharamu apite ilhali wanalikuza tatizo la sintofahamu ya muungano badala ya kutafuta ufumbuzi wa kudfumu wa muungano!
Hivi; kama Wazanzibari wanataka kupiga kura ya maoini juu ya muungano kuna kosa gani? Na hata wakiukataa muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani ni dhambi? Tuache uwendawazimu wa kudhani vile tunavyodhani kla siku itakuwa kama ilivyokuwa mwaka 1964 au 1984 au 1995 au 2000 au 2005; siku hazigandi, na wananchi wa Zanzibar kama watu huru wanawafundisha "jambo" wananchi wa Tanganyika kwa kuwa Tanganyika iliingizwa kwenye muungano ili kuimeza Zanzibar kwa vile Tanganyika haikuwekwa kwenye ramani isipokuwa Zanzibar ndiyo iliyowekwa.
Nadhani umefika wakati sasa wa kutumia akili yenye satwa ya maamuzi makini na ya kimkakati; wapo waliyehusika kwa namna moja na au nyingine kuhakikisha kwamba Sudan Kusini inajitoa kwenye SUDAN KUBWA; na leo wote ni mashahidi kwamba kuna nchi mpya mbili zilizokuwa moja zinaitwa Sudan Kusini na Sudan Kaskazini - nchi moja ya Wakristo (wengi) na nchi nyingine ya Waislam (wengi). Je, hamuoni kwamba Zanzibar wana haki ya kuamua hatma yao? Na je, hamuoni kwamba Tanganyika ina haki ya kuamua hatma yao? Kwani ni nani aliyewaambia kwamba waliyeasisi muungano ni "miungu" na au "malaika" wenye asili ya watu na walichokifanya kilikuwa maagizo ya Mungu?! Tusijitoe fahamu na au akili ya kudhani kwamba watu wanaweza kudanganywa kwa muda wote na au nguvu zinaweza kutumika muda wote kuwatisha na kuwaogopesha watu wasidai uhuru na haki yao ya kujiamulia mambo yao!
Tuache uzezeta wa akili; turuhusu uhuru na haki ya watu kujiamulia mambo yao wenyewe hata kama kwa upande mmoja ni uchungu na au fedheha. Uhuru, haki na wajibu wa wananchi ni kuamua kwa jinsi wanavyoona wao inafaa! Na hakuna katika historia ya binadamu kwamba aina ya utawala na au uongozi wa kisiasa ulilazimisha jinsi ya kutawala na ukabaki milele - kila utawala ni wenye kwisha na kunapotokea "mapinduzi ya fikra" hapo ndipo panapokuwa chemchemi ya harakati za ujenzi mpya wa nchi mpya na watu wenye mtazamo mpya wa kiakili na kifalsafa. Uhuru kwanza; ubabe na vita vya kuua haki ya kuwa huru baadaye! Huwezi kuwalazimisha binadamu wenye akili timamu ya utambuzi kama unavyoweza kuwalazimisha punda kubeba mizigo huku wakitandikwa bakora na kusukumwa alimuradi mzigo ufike! Punda; hata kama ni mnyama (hayawani) asiyejitambua, akichoka hugoma na lazima abwage mizigo na mateke ayarushe hewani kuonyesha hasira zake....inasemekana kwamba hata wakati mwingine, punda akichoka kuburuzwa na kutandikwa baokora huku amemebeshwa mizigo mizito hurusha mateke na hata kumjeruhi mmiliki. Huyu si binadamu mwenye akili ya utambuzi; nadhani serikali ya JMT na ile ya SUK (ndani ya SMZ) wasiwafanye Wazanzibari na Watanganyika kama "punda" wa kuwalazimisha vile wao (SJMT na SMZ na CCM) wanavyotaka...wafuate utashi wa wananchi unavyotaka; nadhani muafaka ni: KURA YA MAONI JUU YA MUUNGANO! Hili ndio suluhisho la kidemorasia; kama CCM imeamua twende kwa njia ya demokrasia haina budi kukubali "matokeo" ya demokrasia hata kama ni machungu kwa chama hicho!
hawana lolote,washajazwa ujinga huko madrasatul....
Lakini kumbuka wanachodai ni haki yao ya msingi, na wanawajibika kwa uhuru wao kuamua kuukubali Muungano au kuukataa kama wanavyoukana sasa. Kuna faida gani kung'ang'ania Muungano, unatufaidia nini Watanganyika kama si kutuongezea mzigo tu?
Bajeti kubwa, wanaongeza ukubwa wa Bunge, wanatuchukulia ajira zetu wabara wakati sisi Wabara hatutii pua huko Kwao Zenj.