Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Landscapping ya Ikulu imechokaaaa!
Huyu angetuleteaje maendeleo wakati ye mwenyewe anakanyaga vumbi Ikulu na haoni ni tatizo?
Samahani sana ndugu yangu kwani nitasema kwamba maneno yako yamenitia kinyaa kwa hiyo naitapika hoja yako!! kama Landscapping kwako ndiyo kipimo cha maendeleo basi wanyama wana maendeleo zaidi kuliko sisi binadamu.
Waulize waliouza viwanda vyetu kama vilijengwa enzi za nani kama siyo mwalimu. mgawanyo wa rasirilimali na mipango ya maendeleo kila baada ya miaka mitano mitano pamoja na kufanya tathimini ya kule tulikotoka ni mambo yaliyokuwa yanafanyika enzi za mwalimu. Sisi wengine tulikula unga wa njano (Yanga) na kununua kwa foleni vitu vya kawaida kabisa kama sabuni na dawa ya mswaki lakini tulijua ni kwa nini.
Nakumbuka uswahilini kwetu maandazi yalipopanda bei kutoka Senti 25 hadi 50 zogo lake lilikuwa ni balaa. Mwalimu hakuwaza kuajiri watu kwa mamilioni ya shilingi ili watunze landscape wakati watu wake hawana chakula. Kila Mwaka ikulu siku hizi inatengewa mabilioni ya shilingi ili kuikarabati, ukarabati huo umeleta maendeleo gani kwa watanzania wa kawaida?