Nimeweka kwenye title kabisa labda Mods wanisaidi namna ya kuiweka lakini yoyote kwa yote ni unyama ambao sikutegemea kama watanzania leo hii tumefikia unyama wa kiwango hiki...haivumiliki...Mkuu weka worming ya huu uzi ...Dah! Hatari hii
Wanazunguka mbuyu.......Ngoja tusubiri viongozi wa chama watasema nini lakini mambo haya haya vumiliki hata chembe....Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa kabla ya tukio Mbwamb
alikuwa na wenzake wakistarehe kwa vinywaji, lakini yeye hakuwa anakunywa
chochote lakini ghafla alipigiwa simu na watu hao, wakidai kuwapo wanachama
wa CCM waliotaka kurudisha kadi na kujiunga na Chadema. Hata hivyo, chanzo
cha tukio hilo hakijajulikana ila taarifa za awali zinahusisha masuala ya
kisiasa, kwani baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki kumalizika, malumbano ya kisiasa na kukamiana yaliendelea eneo hilo. SOURCE HABARI LEO
ni wanne na haijajulikana kama ni wana chadema moja kwamoja....lakini matukio ambayo unaweza kuya husisha moja kwamoja ni yule wakala alie uwawa kinyama kule Igunga na Kukatwa katwa kwa wabunge wa chadema kule mwanza pengine nia ya walikuwa wana wakataka ilikuwa ni kuwafanya kama walivyo mfanya mwenyekiti....Mbona Arumeru mauaji yamekuwa kitu cha kawaida? Wale watano waliokutwa wadmekufa barabarani uchunguzi ulifikia wapi? CDM jamani mbona tunaisha?
sasa kama polisi wameshaanza kusema haihusianai na mambo ya kisiasa inaelekea walisha fanya uchunguzi wa kifo cha Mbwambo hata kabla hajafa......Duh hii hatari. Mbona tunaelekea pabaya. Kwa kuwa huyu alikuwa mwanasiasa inabidi polisi wafanye uchunguzi wa kina na kuutangazia umma juu ya kilichosababisha kuuawa kinyama namna hiyo. Yasije yakawa ni mauaji yanayohusishwa na siasa.