Picha: Hali Inavyotisha Hospitali ya Muhimbili

Hivi yupo Mtanzania ambaye hajawahi kupata manung'uniko kuhusu hali na huduma za afya nchini?

Madaktari kugoma naona hii ni arobaini tu maana hali imekuwepo toka muda mrefu! Na nilishamsikia docta mmoja mgeni katika clinic private akisema Tanzania moja ya urahisi katika kazi yake hana pressure ya kulalamikiwa hata asipogundua ugonjwa au kutibu vizuri.

Maana yake hali ni mbaya hasa hata hawa madaktari wetu wakirudi bila vifaa na mazingira machafu hivi sijui hiyo kazi itafanyikaje?
Leo Legal and Human Rights Centre wanaenda Muhimbili walisubiri nini muda wote huo? Ukizingatia afya ni moja ya haki za kibinadamu (Basic Human Rights) Na mchukue hatua ili tuone ikiwa mko HURU na serikali yetu na ikiwa mnafanya kazi kweli!

Kulikuwa na haja gani ya kufanya sherehe kubwa za Uhuru? Inasikitisha sana.

Democracy is the worst system with exception of all others - Aliyechaguliwa lazima alipe fadhila na hawezi kuwageuikia wafadhili mwisho wa siku Mwananchi is always the loser!
 
Hii hali itawafanya hata wale wenzetu waliogoma kufikiri waanze kufikiri na kuchukua maamuzi.
 
Tunaosikitika ni sisi watanzania, wenye nafasi yakufanya maamuzi wamejiwekea utaratibu wakutibiwa nje ya nchi. Asante kwa kuweka viongozi wazembe kuliongoza taifa.
 
Enyi marekani mko wapi? au wagonjwa hawahitaji haki za binadamu? njooni tuungane tuindoe serikali madarakini kwani imeshindwa kuhudumia watanzania.kila mahali Tabu mfano umeme tabu,hospitali tabu,mashuleni na chuoni tabu........Je huu ni utawala bora?
 
ff, ltz sijawaona humu! natamani kusema neno baya kwa wapiga kura wenzangu lakini nafikiri si wakati muhafaka yatosha niseme tungewapa kura 0 wangechakachuaje ? tumewapa asilimia 40 wamechakachua 20 wamepata total 60% sasa zinatutandika!! kuna mama kwenye video kakiri kapigia kura wanayemtandika hivi sasa lakini cha ajabu huyo mama hawezi kuwa balozi wa wenzake 2015 akipewa kofia, kitenge na fulana hiyo october 2015 haya yote atasahau. leo sitaki kusema mengi kwa hao wapiga kura wenzangu wanaotandikwa hivi sasa kwa kuwa wapo kwenye janga sitaki kuwaongezea maumivu nichoweza kusema

MIAAAKA HAMSIIIINI YA U-V-U-M-I-L-I-VU
 
looh!!!!!
Halafu eti mkulu yupo kimya!!!!!inatisha mno!!!
cameroon wakati moja ya gazeti binafsi kule uingereza lilipokutwa na kashfa ya udukuzi alikuwa ziarani afrika ya kusini kwa madiba lakini aliposikia tu kuna hiyo kashfa alirudi nyumbani haraka lakini kwa hili lililotokea hapa home yaaani nachoka kabisa
 
hatuna viongozi, sijui wanaogopana? maana kama hakuna hatua inayochukuliwa basi kila mtu kashika njia yake. Mwenye cheo haya! mwenye pesa haya! mwenye hospitali haya! mwenye kiwanda haya! mwenye kituo cha mafuta haya! USIYE NA KITU UTAJIJU!! kwa niliyoyaona sijui hata usalama wa taifa na wasaidizi wa ikulu wako wapi kutoa hali halisi?
 
Ndugu mzalendo manene yako swadakta, haya tangulia na bango mie niko nyuma yako lakini hala hala tusijikute tuko wawili tu, si unajua uzalendo wetu maneno, vitendo hakuna. Mie nasubiri behewa likianza naunga
 
Tunaposema ccm na uozo wao waondoke mnabaki kusema hakuna chama mbadala wajinga kweli watanzania serikali ya ccm muendelee hivyo hivyo kutochukua hatua ili watu wafe tu wengi wengi tu ndiyo watanzania wataamka toka usingizini.kiburi cha wabunge ni ujinga wa watanzania hawaelewi shida yao ni pilau na tshirt na kofia,ccmk hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Naunga mkono hoja.Watawala wetu wajua sisi ni wajinga, NDIYO,Jk keep it up mkuu.Mtoto akililila wembe mpe.(50 years poor development but still makofi mengi na vicheko bala tunapo hutubiwa ujinga ) Juzi Pinda kaeleza mengine ,leo kaja na mengine a very high level of Usaniii-yes wajinga ndio waliwao
 
Mtoto hawezi kufanya jambo bila kuambiwa au hawezi kubadili mwenendo wake mbovu bila kufokewa ama kupigwa ndivyo ilivyo kwa SERIKALI yetu ya sasa,Imekuwa mpaka aidha maandamano,vurugu,migomo au ajali ndipo inatekeleza yale yanayo wapasa;Je, ni kweli serikali ya Tanzania kulinganishwa na watoto?? Au hizi kero hazionekani mpaka migomo itokee?? INAKERA KWA KWELI!
 
Na machungu yote haya, ndg zetu ndo husahaulishwa na kofia, t-shirt, kanga, wali, nk. hivi wabongo tutaelevuka lini? mbona tunaokufa ni wale wananchi wa hali ya chini?
 
HARAMBEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE,TUWAONDOE ,MAFISADI HAO,OMBAOMBA HAO,WANAOKWENDA KUTIBIWA INDIA HAO,WANAUZA WANYAMA WETU WA BORI HAO,AKILI MATOPE HAO,WALAFI HAO.JIBU TUNALO NASEMA MAPEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA,TUWAPE KURA YA ZERO MWAKA 2015.TUWAONDOE WABUNGE WOTE WA CCM,TUSIWABAKISHE NASEMA.HII SASA NI NGUVU YA MUNGU .HUU USHENZI UKATILI HATUKUBALIANI NAO TENA.JAMANI JAMANI TUANZE KAMPENI ZA UCHAGUZi SASA HIVI.TUWEKE KWENYE KUMBUKUMBU ZETU HUU UKATILI AMBAO UMEFANYWA LAZIMA WATAULIPA.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mbona sioni cha ajabu kwenye hizo picha. Hii ni hali ya kawaida ya kila siku tu Muhimbili. Kwa ujumla, ukilazwa hapo ujuwe ni sawa na death sentence. Chances are, utaishia kuambulia maambukizo na hatimaye maradhi ya ziada kwenye wodi just by sharing congested and filthy restrooms/washrooms with 20-plus other patients (among many other dire and pathetic conditions at the hospital)
 
Back
Top Bottom