Hospitali ya Muhimbili yatoa ufafanuzi kuhusu kero ya ucheleweshwaji wa utoaji wa Medical Report

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,989
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia ucheleweshwaji wa kutoa Ripoti ya Matibabu (Medical Report) kwa Mgonjwa licha ya kuwa inalipiwa Tsh. 100,000 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akidai kuwa zamani ripoti hiyo ilikuwa bure, Uongozi wa Muhimbili umetoa majibu.

Mdau amedai kuwa alikuwa akimuuguza Mtoto katika Wodi ya Watoto, amelazimika kurejea Mkoani anapoishi na kufnaya kazi na kuwa hii ni wiki ya pili sasa hajapata Ripoti licha ya kulipia

Kusoma malalamiko ya Mdau soma hapa: Hospitali ya Taifa Muhimbili na urasimu wa kutoa Medical Report

UFAFANUZI WA MUHIMBILI
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha anasema:

“Utaratibu huu wa kulipia Medical Report Tzs. 100,000 haujaanzishwa na Prof. Janabi, ni utaratibu ambao umekuwepo takribani miaka mitano iliyopita, hivyo ameukuta.

“Kuhusu suala la Medical Report kuchukua muda mrefu naomba tulichukue..na kuliboresha.”
 
Naona huyo msemaji wa Muhimbili hajajibu kitu, amekuja na majibu rahisi kwenye maswali magumu.

Nani anataka kujua huo utaratibu ulianzishwa na nani?
Kama ulianzishwa na watu wengine au ulianzishwa na Professor Janabi, hiyo inatuhusu nini sisi?
Mbona kuna vitu vingi tu vilikuwepo hapo kabla, na Janabi alivyopewa madaraka akavifuta, kwanini na hili la kutoza laki moja kwa ajili ya uomba medical ripoti asilifute?

Kusema hilo suala la kuchelewa kutoa ripoti wamelichukua, maana yake ni nini?
 
Medical report ni haki ya mgonjwa kwanini atozwe,na kwanini kuna urasimu wingi kuipata?

Kwakweli mnaumiza watanzania sana.
 
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia ucheleweshwaji wa kutoa Ripoti ya Matibabu (Medical Report) kwa Mgonjwa licha ya kuwa inalipiwa Tsh. 100,000 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akidai kuwa zamani ripoti hiyo ilikuwa bure, Uongozi wa Muhimbili umetoa majibu.

Mdau amedai kuwa alikuwa akimuuguza Mtoto katika Wodi ya Watoto, amelazimika kurejea Mkoani anapoishi na kufnaya kazi na kuwa hii ni wiki ya pili sasa hajapata Ripoti licha ya kulipia

Kusoma malalamiko ya Mdau soma hapa: Hospitali ya Taifa Muhimbili na urasimu wa kutoa Medical Report

UFAFANUZI WA MUHIMBILI
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha anasema:

“Utaratibu huu wa kulipia Medical Report Tzs. 100,000 haujaanzishwa na Prof. Janabi, ni utaratibu ambao umekuwepo takribani miaka mitano iliyopita, hivyo ameukuta.

“Kuhusu suala la Medical Report kuchukua muda mrefu naomba tulichukue..na kuliboresha.”
Medical report Tshs 100,000?

Jamani mtu amelipia huduma zote vipimo na matibabu na bado ripoti yake mnamuuzia.

Nchi inaendeshwa kihalifu sana hii
 
Medical report laki moja?.mbona hili Taifa lina watu wajinga hivi...
Aisee...yaani karatasi na wino wa kuprint + muhuri na signature ndio laki?...isitoshe huyo taarifa yote inayoandikwa kwenye hiyo report imeshalipiwa na client...
Takataka kabisa....
 
Back
Top Bottom