PICHA: CHADEMA yabadili Mbinu za kuwania IKULU 2015; Pia yazinduca M4C Jimbo la MBEYA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

FRIDAY, MARCH 1, 2013
[h=3]CHADEMA YABADILI MBINU ZA KUWANIA IKULU 2015. PIA YAZINDUA M4C JIMBO LA MBEYA[/h]


Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe akiongea na viongozi wa Chadema wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya

Maandamano ambayo yaliongozwa na Mbowe yaliyoanzia katika eneo la Uhasibu Mafiat hadi katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe,Mbowe aitembea kwa mwendo wa kilomita tano ambapo makundi ya waendesha bodaboda, baiskeli na watembea kwa miguu walijitokeza kwa wingi kuunga mkono maandamano hayo.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuwa kitalazimisha maandamano nchi nzima iwapo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Naibu wake hawatakubali kujiuzulu kwa kusababisha anguko la elimu nchini.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kimeamua kuanza kutekeleza sera yake ya kuongoza kwa majimbo sasa ili kuongeza nguvu ya mapambano na harakati za kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushika dola mwaka 2015, badala ya kuendelea kutumia mfumo wa zamani ambao ilikuwa rahisi kudhibitiwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .


Kadhalika, chama hicho kimesema hakitampokea mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi atakayekosa nafasi ya kugombea kwenye chama chake na kutimkia Chadema katika dakika za mwisho kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.


Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Chadema wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwa ni maandalizi ya kuzindua kanda yake kwenye kanda hiyo.


Alisema kuwa mfumo wa zamani ambao mambo yote ya harakati za chama hicho yalianzia makao makuu ya chama, ulikuwa ni rahisi kudhibitiwa na dola ya CCM kwa kuwa walikuwa wakiwavizia viongozi wa kitaifa wanapotoka nje kwenda kuendesha harakati wanawapiga mabomu, kuwakamata na kuwafungulia kesi mahakamani.


“Tunataka dola ikusubiri viongozi wa kitaifa watoke makao makuu ili wawadhibiti, wasikie mapambano yanatokea kwenye kanda zetu kama hii ya Nyanda za Juu Kusini, kanda ya Magharibi na nyinginezo,” alisema Mbowe.


Alisema kuwa katika mabadiliko hayo pia Chadema inaachana na siasa za kiuanaharakati na badala yake inaanza kujikita kwenye siasa za maandalizi ya kushika dola.


Akizungumzia utaratibu wa baadhi ya wanachama wa vyama vingine, kikiwemo chama tawala CCM kukimbilia ndani ya chama hicho baada ya kutoswa kwenye nafasi za uchaguzi, Mbowe amesema kuwa kuanzia sasa Chadema hakitampokea mwanachama yeyote wa aina hiyo.


Mbowe alisema kuwa Chadema hivi sasa ipo kwenye maandalizi makubwa ya kunyakua dola mwaka 2015 na hivyo inao wajibu wa kuwaandaa wanachama wake ipasavyo ili kiweze kuwa na wagombea wazuri, imara na wenye uwezo wa kuwezesha chama hicho kupata ushindi mkubwa.


“Kama kuna mtu leo anakula matunda ya ufisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi akidhani kuwa atahamia Chadema kwa kuwa ana fedha za kununua kura za maoni, ameula wa chuya, hatutampokea mtu wa aina hiyo, ” alisema Mbowe.


Alisema kuwa kuanzia sasa Chadema itawapokea wanachama kutoka vyama vingine baada ya kuwapima uadilifu wao, kuchunguza historia yao na utayari wao wa kutumika ndani ya chama ili waweze kupata wanachama na viongozi wazuri watakaokisaidia chama kushika dola mwaka 2015.


Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikitumia mbinu mbalimbali za kukisambaratisha Chadema, ikiwa ni pamoja na kuwatumia mamluki ndani ya chama, lakini kutokana na uimara wa Chadema mbinu hizo zimekwama na Chadema inasonga mbele.


Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema kuwa yeye pamoja na wapambanaji wenzake wametumia zaidi ya miaka 20 kuijenga Chadema na kuipa nguvu kisiasa hadi hapo na hivyo hatakubali kuruhusu chama hicho kihujumiwe au kusambaratishwa kwa namna yoyote ile.


Alisema kuwa ikiwa wana-Chadema wataruhusu Chadema ife leo, itawachukua tena miaka 20 mingine kuijenga na kuifikisha mahali iilipo hivi leo.


Mbowe alitolea mfano wa vyama vya siasa vilivyowahi kupata nguvu na umaarufu mkubwa wa kisiasa nchini kama vile Chama cha Wananchi, CUF, NCCR – Mageuzi na TLP ambavyo alidai kuwa CCM illifanikiwa kuvizima na kuwa hata vyenyewe itavichukua muda mrefu usiopungua miaka 20 kurejesha umaarufuvilivyokuwa nao.

Na mbeya yetu
 
644164_10151306451562548_1773539231_n.jpg
 
Sijui kwanini MIKUTANO ya CCM haijazi Wanachama au Wananchi kwa Umati kama CHADEMA; Pamoja na kuwa na PESA; Khanga, Kofia, Magwanda, Chakula, Malazi, PESA Inasikitisha sana...

Lakini MBOWE anasema Ukweli kuwa kuna Vyama Vilivyokuwa VinaVuma Sanaana lakini CCM ilifanikiwa kuvishikilia shingo zao na Sasa hivi havina Ule Umaarufu...

CCM ni Janja ina PESA rahisi kushawishi Wengi walio kwenye Siasa hawafanyi kazi za AJIRA kwahiyo ukiona Milioni 10 na unaambiwa utasafiri nchi nzima na Mwenyekiti wa UVCCM Uh PerDem



Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
 
Chadema inatisha. Ni mwendo mdundo tu hadi kieleweke.
 
Kadhalika, chama hicho kimesema hakitampokea mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi atakayekosa nafasi ya kugombea kwenye chama chake na kutimkia Chadema katika dakika za mwisho kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Niliwaambia hili tangu kuelekea kwa uchaguzi wa 2010, hususan kuhusu Shibuda. Nikaonekana sina mantiki kwa wengine.

Sasa CHADEMA wamegundua kitu kile kile nilichosema 2010, kwa majuto ya mjukuu.

6th August 2010 18:17 Nilisema

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/69028-shibuda-ahamia-chadema.html#post1015981

Sipendi kuona watu wanaokataliwa na CCM na kubaki bila jinsi ndio wanakuwa wagombea wa CHADEMA. Naelewa kuna temptation kwa CHADEMA kuwachukua kwa sababu wana name recognition, lakini naweza kumsikia Makamba akisema "Upinzani hawna kitu, wanangojea makombo ya CCM" na katika hili atakuwa right.

Kama hii habari ni kweli, hapa ninachoona ni kwamba Shibuda anataka ubunge kwa hila zote, na wala hajali siasa za vyama. Jambo la hatari sana hili.

Hamna kumpa ugombea ubunge wa CHADEMA huyu. Kuna watu wako CHADEMA miaka yote viongozi wa wilaya, wamejenga uanachama, halafu leo mtu atoke CCM mara moja apewe ugombea ubunge? Hata maji ya kijani hayajamuisha mwilini? Hii itakuwa mbaya sana kwa party morale, unles hao watu wa CHADEMA wa wilayani humo nao ni stooges tu wanaofanya siasa za hero worship and stongmen seeking.

Piga chini Shibuda, from presidential ambitions to no constituency. That's what you get for chickening on Kikwete and having no principle.

Thanks for the long overdue vindication.

Polepole CHADEMA wanajifunza.
 



Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.

Jamani watu mbona wanaharibu hapo....Mwampamba na mwenzake hawajaihama CHADEMA ila walifukuzwa...kuhama na kufukuzwa ni vitu viwili tofauti.
 
Jamani watu mbona wanaharibu hapo....Mwampamba na mwenzake hawajaihama CHADEMA ila walifukuzwa...kuhama na kufukuzwa ni vitu viwili tofauti.

Kuficha Maovu yao... Unajua CCM ni chama KISAFI hakibebi WAOVU
 
Bravo Chadema Mbeya keep up
peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee's........................power!
 
Back
Top Bottom