umemuona wapi mwinyi?Yaani upande wa serikali unakuwa na LUKUV, NCHIMBI, MWINYI? tuna safari ndefu hawa ni hamna kitu kabisa
Kweli mkuu lakini huyo ni KILAZA toka kuzaliwa alikosa madini joto!! amedumaa kiakili.
Jitahidi kuchangia kwa kuanza na msitari mmoja na taratibu utaongeza wa pili huku ukijifunza wengine wanavyofanya utafanikiwa kujenga hoja, maana si peke yako tu mwenye matatizo hayo, tupo wengi tu.
Kama shuleni ulikazania sayansi tu na kuweka kiporo masomo ya lugha hapa leo tumeona una kazi ya kufanya mazoezi. usikate tamaa ipo siku utanyosha vizuri tungo ya mchango wako wa mawazo na kueleweka vizuri.
Unapenda sana kuandika but you are missing one thing hujui kujenga hoja.
Kweli mkuu lakini huyo ni KILAZA toka kuzaliwa alikosa madini joto!! amedumaa kiakili.
Kuelewa mmeelewa ila kinachowasumbua ni upuuzi wa Personal attack
ukweli unabaki wazi CHADEMA waliweka msimamo toka mwanzo hawatambui kikwete na hawajawahi kukanusha hilo au wamewahi
lakini leo tunaona wameomba kwenda IKULU kuongea na raisi!!!
Hapo hakuna tatizo? Lini kikwete ametambulika na CHADEMA?
lakini pia wamekuwa wakisema wananchi ni mahakama ya mwisho lakini leo Magogoni imekuwa ni mahakama ya mwisho.
hii ni CCM- C in making
aisee CV yangu yakwamba nimesoma sayansi umeitoa wapi? umejuaje kama mimi ni mzungu nimejifunza kiswahili kimtindo
ina maana wewe umeweka humu post ili watu tukupigie makofi,
i thought you have some manner, ndivyo kwenye wazazi wako walivyokufundisha kuelekeza wa kwa MOCKING kisha unajiona wewe ni mzalendo kuliko wengine?
tukubali mawazo tofauti sio kila mtu ni kondoo,
Ni kipi kinakupa haki ya kudhani tungo yangu haieleweke au wewe umeshindwa kuelewa kutokana na IQ yako? ina kila usichoelewa wewe basi kina matatizo?
Comment yako ya kwanza umekubaliana na mimi lakini alipokuja huyo hapo nchi ukashusha comment hii ya pili hahahaha una tatizo la kufuata upepe sio?
cha kusikitisha wali saini mwafaka ni Nchimbi kwa hiyo walikwenda kufanya maongozi na waziri wa michezo au Raisi? kwa nini Nchimbi na waziri wa wizara ya sheria na katiba alikuwepo kwenye hicho kikao?
Nchimbi atafanya utekelezaji gani kwa hayo waliyokubalina?
Bado sio sahihi makubaliano unayofanya na Raisi yakasainiwa na mtu mwingine ndio maana nasema Kikwete kawapiga changa la macho walichofanya CHADEMA ni kujidhalilisha hapo IKULU
kama kuna mtu anadhani mimi ni magamba check post zangu za nyuma
Ukweli lazima usimamiwe
Chadema aka CCM- C hatuwataki tena mnatuyumbisha wanachama mara hatumtambui Kikwete na serikali yake mara mnamtambua huo ni uroho wa madaraka Big up Slaa and Zito kwa kutokwenda IKULU. Mkiendelea hivyo tunawapiga chini tunaungana na Jembe letu Lowasa ambalo linakuja kwa kasi na kukubalika na Rai wa Bongo waliochoshwa na utawala wa JK na Maandamano ya CDM. Lowasa jipanga kamanda CDM wanaanguka na wewe utakuwa kimbilio la watanzania tuko pamoja nawe kwa niaba ya UVCCM na BAVICHA
utafikiri wapiga debe!Kabla ya sijachangia zaidi. Hawa wapiga picha za habari hizi,mimi sijawapenda. Si bora wangevaa nguo hata asili ya vitenge au khanga? Sijapenda Tshirt na jeans kupokelewa Ikulu! Bungeni tu,kuna code of what you wear. Hata hivyo nimefarijika na bashasha za Rais na kamati ya Chadema,wote wakiwa na nia moja, katiba mpya ya wananchi! Kwa manufaa ya Taifa!
hivi umegundua magwanda yamependeza kweli ikuluNdio maana watu wanapigania kuingia Ikulu, yani jamaa wameenda kutembea tu wanachekelea namna hiyo.
Uandishi ni dhana ngumu, na naielewa hivyo. Nakumbuka tulivyopata taabu kufanya mazoezi ya tungo kweneye mafunzo ya uandishi kwenye nyanja za habari kana kwamba hatukupitia english composition au somo la fasihi. Kwa vyo vyote sikumaanisha wewe, ila kuna mtu sikusoma ni nani lakini comment yake ilikosa ladha ya mtu kuendelea kuisoma baada ya kumaliza mstari wa kwanza.
Pamoja na kwamba uandisi unatofautiana sana kati ya kanda, nchi na mabari, lakini mantiki ya kumfanya msomaji avutike kuendelea kuisoma ndio uwezo ambao mwandishi anakuwa amejenga mjengo wa kueleweka alichokiandika.
Nakumbuka profesa wangu Tom Englewood alivyotuambia chuoni, ukiweka ukingo wa kupokea kutoka kwa wanaokukosoa, kusahihisha au kukuelekeza utakosa kuyajua mengine ambayo ungeweza kuyapata kutokana na subira ya kuwa msikivu. Waafrika wengi tuna tatizo hilo, lakini wazungu wengi ukiwa unamweleza kitu hata kama anakijua utaona ametulia na kukusikiliza kwa makini kumbe lengo ni kujifunza jipya au kukusoma wewe.
Kwa vyo vyote hakuna mwenye kujua yote, na kila siku ni darasa katika maisha yetu. Hata makazini semina na mafunzo haviishi hadi siku utakapostaafu. Tufunguke akili ili tuyapate tunayoyetema, maana kuna vitamini na caroli nyingi kutoka vyakula tunavyovitema kwa ajili ya afya yetu.
Hujui kuwa JK ndio alikuwa kigeugeu?Wakati ule niliamini wanaenda kuongea kuhusu sheria za uchaguzi ambazo Salary Slip analalamikia kumbe jamaa walienda wakanywa sharubati na kupiga picha basi.
Ritz Salary Slip Lizaboni Pohamba Erythrocyte swissme