Pesa zilizoibiwa na mafisadi wa ccm sio michango ya wanachama wa ccm

Jan 16, 2007
721
176
Wassira amvaa Dk Slaa juu ya mafisadi


Christopher Maregesi, Bunda
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Stephen Wassira amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa kuacha mara moja kuwapakazia wanaCCM kuwa ni mafisadi na badala yake ajihusishe na ujenzi wa chama chake .

Aidha Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) alimtaka katibu huyo wa Chadema kuwapeleka mahakamani watu anaodhania kuwa ni mafisadi kama anao ushahidi juu ya madai yake hayo.

Kauli ya Wasira inakuja siku moja baada ya Jumapili ya juzi Dk Slaa katika mkutano wake wa hadhara aliouhutubia katika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora kutoa orodha ndefu ya watu aliodai ni mafisadi walioko ndani ya CCM wanaopaswa kuondolewa ndani ya chama hicho na kushitakiwa.

Akizungumza na viongozi wa CCM ngazi za kata, matawi na mashina katika ofisi za chama hicho wilayani hapa jana. Wassira ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Bunda alisema tabia ya Dk Slaa kuwataja wale anaodhania kuwa ni mafisadi inaonyesha jinsi gani kiongozi huyo alivyofilisika kisiasa.

Alisema kwa ujumla jukumu la CCM la kujisafisha liko mikononi mwa wanachama wenyewe kwani ndio wanaojua madhaifu yaliyomo ndani ya chama chao na wala siyo la kiongozi yeyote yule wa chama hivyona kwamba Dk Slaa anapaswa kuacha kwani hajatumwa na CCM kufanya kazi hiyo.


“CCM hatujamtuma Dk Slaa kutusaidia kazi ya kuwabaini mafisadi na kama anao ushahidi aupeleke PCCB (Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa) ili iwachunguze,”alisema Wassira.

Kuhusu hatua ya chama hicho ya kujivua gamba Wassira alisema ilifikiwa baada ya wanachama wa chama hicho kubaini kuwa chama chao kilichoundwa mahsusi mwaka 1977 baada ya kuvunjwa kwa TANU na ASP kwa lengo la kutetea wanyonge kilikuwa kimeacha njia na kwenda kusiko.

“Tulijitathimini na kubaini kuwa hapa katikati tulianza kuacha njia.Tuliachaje njia; ilifikia mahala huwezi kuchagua au kuchaguliwa bila fedha yaani tuliifanya fedha kuwa moja ya sifa za uongozi,”alisema Wassira.

Wassira aliyetumia takribani dakika 45 katika hotuba yake alisema katika kufanya hivyo baadhi ya wanachama ambao NEC iliwaona kuwa na doa waliachwa jambo ambalo hata hivyo alisema haimaanishi kuwa CCM haitaki matajiri.

Kuhusu kukijenga upya chama hicho kupitia falsafa yao ya kujivua gamba Wassira alisema kinachotakiwa kwa sasa ni kujenga mahusiano ya moja kwa moja kati ya uongozi wa kitaifa na ule wa shina ili kuwepo mtandao mzuri wa mawasiliano utakaokisaidia kuimarika zaidi na hivyo kujihakikishia ushindi kwa chaguzi mbalimbali.
Source: Mwananchi

Hawa Viongozi wa CCM hawana aibu tangu watangaze kujivua magamba hakuna kinachoendelea mbali na porojo.Mmevua magamba inamaana mnawafahamu mafisadi katika chama chenu ti majina na hatua zilizochukuliwa na wafikisheni katika vyombo vya sheria na sio kutuachia kitendawili cha kuwapa miezi mitatu!Miezi mitatu ya nini?????CCM HIZO FEDHA WALIZOZIIBA MAFISADI WA CCM SIO MICHANGO YA WANACHAMA WA CCM NI FEDHA ZETU NA RASILIMALI ZETU.Kauli zenu zinatia kinyaa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ukweli ndio huu, tutawaandama kwa kuwa fedha walizipora ni kodi ya watanzania. Mafisadi walioifilisi SUKITA [japokua walituibia michango yetu wlipokua wakitulazimisha kuchangia mwenge] hao tuliwaachia wao. Lakini hawa wanaotuibia EPA, Dowans, TICTS, RITE, BOT hao ni jukumu la kila mtanzania. Tutapambana mpaka kieleweke!
 
Hivi huyu wasira si ndie alieingia bungeni 2005 kwa pesa iliyokwapulowa na genge la mafya wa ccm? Kama mtakumbuka pesa ya import support iliyotolewa na serikali ya Japan iliibiwa kijanja na genge la mtandao wa kumwingiza Jk madarakani na Wasira ni mmoja wao. Baada ya kushitukiwa serikali ikaunda task force geresha kama ile ya kupokea pesa za wizi wa Epa. Na kama sikosei kampuni iliyopewa kazi hiyo ya kukusanya hizo pesa ni Majembe auction mart ila cha kusikitisha hakuna ripoti yoyote iliyoonyesha kama pesa hizo zimerudi ama la. Kweli sisi wadanganyika ni wepesi wa kusahau mpaka sasa fisadi nae anakaa viti vya mbele kuwasafisa fisadi wenzake.
.
 
Back
Top Bottom