Pesa ninazo nisaidie wazo

Tyegelo

Member
Apr 25, 2011
29
2
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.
 
Njoo hapa bar kwanza tuweke heshima, baada ya raundi nne mawazo tutayapata tu:loco:

On a serious note: Kwa nini usijaribu kilimo (horticulture)?
 
Nashauri usi-invest on one business. Kilimo nafikiri ukijipanga vizuri itakutoa.
 
Njoo hapa bar kwanza tuweke heshima, baada ya raundi nne mawazo tuyapata tu:loco:

On a serious note: Kwa nini usijaribu kilimo (horticulture)?

Kilimo? Tatizo huku Songea ardhi imechoka sana, yatahitajika matumizi makubwa ya mbolea ambayo yataongeza gharama za uzalishaji na hivyo kunipunguzia faida, mkuu. Heshima bar? Tusile mtaji, mh.
 
Mkubwa hapo inatakiwa urudishe sh 1,464,489/= kwa mwezi that means kwa miaka 15 utakuwa umepeleka bank sh 263,520,000/= hapa bank wametengeneza faida ya sh. 187m,Je ni biashara gani utayofanya inayoweza zalisha sh 2.5m(1.5m makato+1m interest) kwa mwezi? Ni PM nikupe Mchakato!
 
wakati unashangaashangaa, weka 80% kwenye fixed deposit zitazaa badala ya kupotea.
Kilimo ndo biashara nzuri la sivyo nenda china, au anzisha duka la pembejeo za kilimo

Usiogope kununua mbolea ndiyo dawa pekee ya kufufua ardhi.
Ungekuwa hapa dsm ningekupa darasa ama kukupeleka kwa wataalamu wa ngo za kilimo.
 
Aiseee babaangu nikopeshe buku 50 niongeze mtaji wangu wa ngurue

nitakurudishia buku 80 miezi 3 na mbege lita 20
 
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.
Huo mkopa au msala/kitanzi? Why? Tshs 80m x 5yrs x21% = ~Tshs 130m. Kwa maana nyingine lazima biashara utakayoifanya ikupe faida ya Tshs 2.5m kwa mwezi, kwa sababu marejesho tu kwa mwezi ~ Tshs 2.2m . Biashara gani itakuwa na faida ya Tshs 2.5m kwa mwezi huko Songea Mkuu?
 
Sasa wewe walikupaje mkopo?hata aliyekupa mkopo akikusikia meneja wa mikopo anafukuzwa kazi.uliomba mkopo wa kufanyia nini?
 
wakati unashangaashangaa, weka 80% kwenye fixed deposit zitazaa badala ya kupotea.
Kilimo ndo biashara nzuri la sivyo nenda china, au anzisha duka la pembejeo za kilimo

Usiogope kununua mbolea ndiyo dawa pekee ya kufufua ardhi.
Ungekuwa hapa dsm ningekupa darasa ama kukupeleka kwa wataalamu wa ngo za kilimo.
Mkuu Moony, mimi nipo kwenye NGO na inashughulika na masuala ya vijana, Naomba uniunganishe na hao watu wa NGO wanaoshughulika na kilimo. Tunadhani kilimo kinaweza saidia vijana kwenye ajira. Tupo Dar
 
Hilo Ndo tatizo kubwa sana kwa sisi watanzania, Ila mimi sitaki kuamini kwamba ulikopa Benk make benki ni lazima uwe na Mpango Kazi au Bsiness planing na some time uwe na Biashara kabisa na uwe na kila kitu kinacho takiwa kwa ajili ya Biashara.

Na kama kweli umekopa bila kujua utafanya nini basi inakula kwako mkuu, kwa sababu kabla hujakopa ni lazima ujirizishe kwamba Project unayo enda kuifanya inalipa, na kumbuka biashara si lele mama kuna kuyumba hata ndani ya miaka 3,

So mkuu unahitaji ushauri wa hali ya juu kwa huo mtaji wako
 
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.

Unamwamini Mungu kupitia nani? nijibu bila utani nikupe mchakato.
 
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.

Mkuu kwanza nikupe hongera kwa kuwa hapo umecheza kama pele. Hatua ya kwanza ogopa saaaaaana
na ya pili omba Mungu saaaaana. Kulipa mkopo miaka 15 ni ishu kweli au unamaanisha mwaka 1.5? Takwimu zinaonyesha 95% ya biashara mpya hufeli ndani ya miaka mitano. Kama yako itakuwa moja ya hizo utakuwa umebaki na miaka 10 ya kulipa mkopo baada ya biashara kuanguka. Kwa hiyo hakikisha yako ipo ndani ya 5% zinazo faulu. Ndio sababu mikopo ya mda huo uwa ni ya kujenga au kununua nyumba. Inakubidi uanze biashara ukiwa unalenga kulipa mkopo wote ndani ya miaka miwili. Kuna biashara nyingi sana unaweza kufanya na hela hiyo, wacha kwanza niendelee kuwasikiliza wadau wa JF wanavyokushauri.
 
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.

Tumekusamehe ila mie namtafuta huyo aliekupa mkopo nahisi kama ulimpa rushwa maana atatoaje mkopo kwa mtu ambae hana business idea au hana hata biashara inayo exist wakati kipindi hiki hela ilitakiwa iwepo kwenye mzunguuko as soon as ilipotoka alafu bado tunajadili sijui mpaka lini, ngoja na mie ntafakari nitarudi baadae na mawazo maana ni mapema mno kutoa mawazo
 
Back
Top Bottom