Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Na Peter Mwenda
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema
kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.

Mnfiki huyu wala sitaki kumsikia. Anakumbuka alisema nini juu ya MWEMBE CHAI NA PEMBA katika radio TUMAINI.

Au niibandike hapa sauti yake? Kwa maelezo yake MWEBE CHAI NA PEMBA WALIKUWA WANYAMA.

Huyu mtu amechanganyikiwa, simuelewi hata kidogo.

ET GODS PEOPLE!
 
Acheni kupotosha habari hata kama tunawajua mnaongoza kwa udini humu JF lakini toeni mawazo yenu kiliko ku distort message, habari nzima hii hapa.

GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

Paragraph ya pili ya makala imeandikwa kuwa

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

Unachoweza kutetea ni kuwa si direct quote ya maneno yake Pengo, na sio kuwa kuna mwanaJF amezusha.

Waandishi wanatakiwa wawe makini, unless awe amefanya kwa kukusudia.
 
source: majira

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Na Peter Mwenda
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema
kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.

Ila alitarajia kuambiwa maaskofu wavue majoho waingie kwenye siasa?
 
Mhh si madogo.
Watu wakitafsiri kuwa 'hawaonei huruma' watu wa visiwani itakuwaje? Na hawatasita hapo, watasema 'anawachukia kwa sababu kule ni Waislam'
Kwa nini hatuwi makini na maneno tunayoyatumia?
Juu ya hivyo hiyo si direct quote kwa hiyo labda hakusema hivyo ni opinion ya muandishi tu
Watu wenye tatizo la udini siku zote utawajua watachukulia maneno ya mwandishi wa gazeti tena la 'Majira' kama issue kubwa kuliko message ya msemaji mwenyewe. Hizi ndizo quote zao kama ni mtu wa akili utaelewa mwandishi alikuwa na lengo gani lakini kama ni mpenda mambo ya udini kama akina mhogomchungu watachukua maneno ya mwandishi.

Pengo

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.
Mwandishi wa Majira

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.
 
Naona watu wamefikia kumtukana Cardinal Pengo. Tuanzishe mada ya kumtusi Shekh Simba?
 
Watu wenye tatizo la udini siku zote utawajua watachukulia maneno ya mwandishi wa gazeti tena la 'Majira' kama issue kubwa kuliko message ya msemaji mwenyewe. Hizi ndizo quote zao kama ni mtu wa akili utaelewa mwandishi alikuwa na lengo gani lakini kama ni mpenda mambo ya udini kama akina mhogomchungu watachukua maneno ya mwandishi.

Unaweza ukawanyooshea vidole hao uliowataja lakini kumbuka Tanzania kuna mamilioni ya watu ambao hawana uelewa wa kutosha wa kutofautisha maneno ya Pengo na ya Mwandishi.

Ni wajibu wetu kupinga uandishi wa aina hii unaomlisha mtu maneno ambayo yanaweza kutafsirika vibaya kwa jamii.

btw ni rahisi kumsema mtu mdini bila ya kujiona nafsi yako wakati wewe binafsi una Avatar ambayo ina stink of udini. Kweli JF tambarare
 
Mnfiki huyu wala sitaki kumsikia. Anakumbuka alisema nini juu ya MWEMBE CHAI NA PEMBA katika radio TUMAINI.

Au niibandike hapa sauti yake? Kwa maelezo yake MWEBE CHAI NA PEMBA WALIKUWA WANYAMA.

Huyu mtu amechanganyikiwa, simuelewi hata kidogo.

ET GODS PEOPLE!

MS umerudi... "tanzania bara" sioni tatizo lipo wapi kama waislamu wapo hata bara, na wabara wapo zenji, swala la polisi kuua/kutumia nguvu kupita kiasi/kubambika kesi/kufanya ujambazi limekuwa sugu bara siku hizi sisikiii polisi wa zenji kuua raia
 
Unaweza ukawanyooshea vidole hao uliowataja lakini kumbuka Tanzania kuna mamilioni ya watu ambao hawana uelewa wa kutosha wa kutofautisha maneno ya Pengo na ya Mwandishi.

Ni wajibu wetu kupinga uandishi wa aina hii unaomlisha mtu maneno ambayo yanaweza kutafsirika vibaya kwa jamii.

btw ni rahisi kumsema mtu mdini bila ya kujiona nafsi yako wakati wewe binafsi una Avatar ambayo ina stink of udini. Kweli JF tambarare
Wanaoendeleza udini ndio huwa tagert yangu kubwa kupambana nao.

Ukianza kuangalia avatar za watu utapotea ndugu Gai kuna zingine watu wanatoboana utumbo si kuwa yeye ni muuaji kuna wengine wana lundo la vitabu unawezakuta ni jinga la kutupwa.
 
shhhh... kesi ya kwanza haijaisha unaanzisha mpya!!:smile-big:

Waandishi wa Tanzania!! Wanaandika kwa kulenga wanunuzi na si habari kusudiwa, ndio maana uchochezi na matatizo mengi yanasababishwa na wao kwa sasa nchi hii. Wanaandika wanaoona kwamba kitauzika na wao watapata mshahara wao haiwajalishi jamii itapokea vipi. (mtindo ni uleule kama magazeti ya udaku) habari moja ili izae nyingine tuendelee kuuza! Hatujawa na waandishi makini, hata wakiona ukweli kutoka upande wasioutaka hawauandiki kwa maana si lengo lao.

Waandishi habari wa Tanzania ni kama Wanasiasa wa Tanzania!! (labda ni baadhi)
 
hii mada kuandikwa Polisi kuua raia wa tanzania bara, mbona imekaa kama kimajungu?

lengo kutaka kutupambanisha baina ya wazanzibari na watanzania bara, tuamini kuwa maaskofu huwa na uchungu zaidi na wakristo wenzao kulikoni waislam na hasa wazanzibar
We ulitaka asemeje???
 
Mnafiki mkubwa huyu, sitaki hata kumsikia wala kumuona. HIVI AMESAHAU ALISEMA NINI KATIKA REDIO TUMAINI WAKATI WA MAUAJI YA MWEMBE CHAI. Na yale ya PEMBA?

Hivi pale Polisi waliuwa WANYAMA? Huyu ndio tatizo la Tanzania. Hana hata aibu anazungumza kama vile matukio ya Mwembechai na PEMBA yalitokea miaka 70 iliyopita.

Mwenye kumbukumbu ndogo juu ya maneno yake wakati huo anieleze niweke sauti yake hapa JF. KANDA NINAZO LAKINI SITAKI KUPOTEZA WAKATI KWANI NYIE WOTE MLIMSIKIA NA KUMUUNGA MKONO.

Maendeleo ya Tanzania yanategemea KIFO CHA HUYU MNAFIKI.
Wewe mtu wa ajabu kweli unatuuliza sisi tena wakati wewe ndiye unayetujuza, binafsi sijawahi sikia maneno kama hayo umeyatunga kama hujayatunga tuwekee guote zake hapa.
 
Je nae Sheikh Simba amekuwa quoted na gazeti au...?
Waberoya welcome kwanini mnajificha kwenye migongo ya dini kwa majina tofauti? kwa nini msiwe kama Quinine aliye wazi ikija topic ya maslahi ya nchi naijadili kama Quinine vilevile ikija topic ya udini naijadili kama Quinine siogopi. Sasa wengine kule wanajifanya werevu kwa kutumia jina tofauti huku wanajifanya wadini kwa kutumia hili nonsense.
 
Mnafiki mkubwa huyu, sitaki hata kumsikia wala kumuona. HIVI AMESAHAU ALISEMA NINI KATIKA REDIO TUMAINI WAKATI WA MAUAJI YA MWEMBE CHAI. Na yale ya PEMBA?

Hivi pale Polisi waliuwa WANYAMA? Huyu ndio tatizo la Tanzania. Hana hata aibu anazungumza kama vile matukio ya Mwembechai na PEMBA yalitokea miaka 70 iliyopita.

Mwenye kumbukumbu ndogo juu ya maneno yake wakati huo anieleze niweke sauti yake hapa JF. KANDA NINAZO LAKINI SITAKI KUPOTEZA WAKATI KWANI NYIE WOTE MLIMSIKIA NA KUMUUNGA MKONO.

Maendeleo ya Tanzania yanategemea KIFO CHA HUYU MNAFIKI.
mdini ni Mdini tu.dini ya warabu mnaifagilia tafuta historia huone walivyotesa babu zako laiti ungejua leo hii usingekuwa na hasira ya uislamu au ukristo.kuwa na amani tu uelewe Mungu yupo Umtegemee lakini usione mwenzio kwa vile si wa dini yako ni adui.acha acha acha kabisa utaishi kwa furaha hapa duniani kabla hujafa.
 
Mnafiki mkubwa huyu, sitaki hata kumsikia wala kumuona. HIVI AMESAHAU ALISEMA NINI KATIKA REDIO TUMAINI WAKATI WA MAUAJI YA MWEMBE CHAI. Na yale ya PEMBA?

Hivi pale Polisi waliuwa WANYAMA? Huyu ndio tatizo la Tanzania. Hana hata aibu anazungumza kama vile matukio ya Mwembechai na PEMBA yalitokea miaka 70 iliyopita.

Mwenye kumbukumbu ndogo juu ya maneno yake wakati huo anieleze niweke sauti yake hapa JF. KANDA NINAZO LAKINI SITAKI KUPOTEZA WAKATI KWANI NYIE WOTE MLIMSIKIA NA KUMUUNGA MKONO.

Maendeleo ya Tanzania yanategemea KIFO CHA HUYU MNAFIKI.

Kweli Zawadi. Huyu askofu anaongea utadhani hajawahi kuishi Tanzania.

Polisi wameshaua watu wengi katika mazingira ya kutatanisha lakini hawa viongozi wa dini wapo kimya tu. Leo anajidai kushtuka kinafiki.

Tunahitaji maaskofu kama DESMOND TUTU ambao watakemea uovu popote bila kujali nani anahusika na wakati gani umetokea.
 
Kadinali pengo hana ubavu wa kulaumu polisi leo, kwani walipouwa wananchi wa zanzibar na Dar-es-salaam si aliwasifu? na kudai kuwa makosa ni ya marehemu!
Leo anathubutu kutamka kuwa Nchi imeingia doa kwa kuuliwa watu 3 Arusha? au kwa kuwa waliouliwa ni wapenzi wa CHADEMA na wale waliouliwa Zanzibar walikuwa CUF?

Sasa nimeamini kuwa Makanisa TZ wako nyuma ya pazia ktk kushabikia CHADEMA ndio maana uchaguzi mkuu walifunga makanisa yote na kukesha usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi wakifanya ibada maalum ya kumuombea mgombea wao ashinde!

PENGO huna jipya!! heri unyamaze!
 
Back
Top Bottom