Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

muhogomchungu

JF-Expert Member
Jan 9, 2011
375
3
source: majira

Na Peter Mwenda

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea,"
alisema kardinali Pengo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.
 
Pengo: Sikutarajia polisi kuua raia

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Na Peter Mwenda
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema
kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.
 
Jamii nzima inafahamu kilichotendeka hata jeshi la polisi lijaribu kujinasua vipi its too late for them na hakuna kitakachobadilika kwa sasa maana wamesahau majukumu yao ya msingi na kuanza kuua raia
 
hii mada kuandikwa Polisi kuua raia wa tanzania bara, mbona imekaa kama kimajungu?

lengo kutaka kutupambanisha baina ya wazanzibari na watanzania bara, tuamini kuwa maaskofu huwa na uchungu zaidi na wakristo wenzao kulikoni waislam na hasa wazanzibar
 
Mtoa mada....pengo kasema hakutarajiwa watu wa Tanzania bara au Tanzania?
 
Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, amesema

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea,"

Source: Gazeti la Majira
 
Siku ya mazishi kulikuwa kuna mkusanyiko mkubwa sana viwanja vya NMC lakini hakuna fujo iliyotokea wala mtu kuuawa wala mtu kupokonywa mali yake, kutona na hilo nafanya majumuisho kwamba Polisi ndiyo wanao anzisha fujo kwa lengo la kuua watu na kupokonya mali zao kama vile simu na kadhalika. mwisho wa majumuisho
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, amesema

Source: Gazeti la Majira

Mnafiki mkubwa huyu, sitaki hata kumsikia wala kumuona. HIVI AMESAHAU ALISEMA NINI KATIKA REDIO TUMAINI WAKATI WA MAUAJI YA MWEMBE CHAI. Na yale ya PEMBA?

Hivi pale Polisi waliuwa WANYAMA? Huyu ndio tatizo la Tanzania. Hana hata aibu anazungumza kama vile matukio ya Mwembechai na PEMBA yalitokea miaka 70 iliyopita.

Mwenye kumbukumbu ndogo juu ya maneno yake wakati huo anieleze niweke sauti yake hapa JF. KANDA NINAZO LAKINI SITAKI KUPOTEZA WAKATI KWANI NYIE WOTE MLIMSIKIA NA KUMUUNGA MKONO.

Maendeleo ya Tanzania yanategemea KIFO CHA HUYU MNAFIKI.
 
Mkuu alisemaje, hebu tujuze kidogo tafadhali..!
 
Siku ya mazishi kulikuwa kuna mkusanyiko mkubwa sana viwanja vya NMC lakini hakuna fujo iliyotokea wala mtu kuuawa wala mtu kupokonywa mali yake, kutona na hilo nafanya majumuisho kwamba Polisi ndiyo wanao anzisha fujo kwa lengo la kuua watu na kupokonya mali zao kama vile simu na kadhalika. mwisho wa majumuisho

sawa kabisa
 
Mnafiki mkubwa huyu, sitaki hata kumsikia wala kumuona. HIVI AMESAHAU ALISEMA NINI KATIKA REDIO TUMAINI WAKATI WA MAUAJI YA MWEMBE CHAI. Na yale ya PEMBA?

Hivi pale Polisi waliuwa WANYAMA? Huyu ndio tatizo la Tanzania. Hana hata aibu anazungumza kama vile matukio ya Mwembechai na PEMBA yalitokea miaka 70 iliyopita.

Mwenye kumbukumbu ndogo juu ya maneno yake wakati huo anieleze niweke sauti yake hapa JF. KANDA NINAZO LAKINI SITAKI KUPOTEZA WAKATI KWANI NYIE WOTE MLIMSIKIA NA KUMUUNGA MKONO.

Maendeleo ya Tanzania yanategemea KIFO CHA HUYU MNAFIKI.

Wengine hatujamsikia/hatuna kumbukumbu na alichokisema. Bora utukumbushe au uweke mkanda kama unavyodai. Halafu sioni uhusiano wake na maendeleo ya Tanzania hadi unadai yanategemea kifo chake. Kwani yeye ni kiongozi wa nchi?
 
Mhh si madogo.
Watu wakitafsiri kuwa 'hawaonei huruma' watu wa visiwani itakuwaje? Na hawatasita hapo, watasema 'anawachukia kwa sababu kule ni Waislam'
Kwa nini hatuwi makini na maneno tunayoyatumia?
Juu ya hivyo hiyo si direct quote kwa hiyo labda hakusema hivyo ni opinion ya muandishi tu

Back
Top Bottom