Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Mwanahabari Huru

Askofu Pengo unafiki sio sehemu yetu wakatoliki, sikutaka kuandika chochote kuhusiana na wewe, mimi nimebatizwa katika RC nimekuwa muumini mkubwa, nimesoma shule ya Upadri St Mary's Seminary, ninaijua Rc.

Nimesikitishwa sana na kauli zako za kipuuzi, zilizo jaa unafiki, tumekusikia sana ukijipambanua kuwa wewe si muumini wa mabadiliko, tuambie upande wako ni UPI.

Askofu wangu Pengo umemjibu Askofu Niwemugizi alie jitokeza hadhalani na kusema watanzania wanataka katiba mpya, umefufuka ulikotoka na kumshambulia Askofu kuwa katiba au maneno ya Askofu sio msimamo wa RC lakini hakusema kuwa ni msimamo wa RC. Lakini unajua Askofu Niwemugizi si msemaji wa Rc, maana yake alisema kama Mawazo yake kikatiba, na wewe unamjua msemaji wa RC ulitaka kutafuta uhalali wa kujibu mashambulizi la watawala, of target.

Naona umetoka kwa kasi sana kujibu shambulizi hill!,! Lakini hutoki hadhalani kuonya matukio ya kuuwawa kwa watanzania na kutupwa kwenye maji wakiwa wamefungwa mikono Nyuma, wanaopigwa Risasi kama kina tundu Lissu, kuonya viongozi wanao toa maneno ya kibaguzi na kikabila, huwezi kuonya kufokea au kushauri, kazi yako imekuwa ni kujibu mashambulizi kwa wanao ikosoa serikali,

Au unavyeti feki? Unamiliki Mali zisizo halali? Kiongozi wa kiroho unashindwa kujua nini wajibu wako? Sio mala ya kwanza kupingwa na maaskofu wenzio akiwepo Gwajima na kupelekana mahakamani ambapo Askofu Gwajima alikushinda kesi.

Viongozi wa dini simamieni haki na sio unafiki kujipendekeza kama mnataka ubunge, au teuzi za kina mama Lwakatale sawa, Hata mkitaka usemaji wa Ccm nafasi za kina polepole.

Swali la Kizushi: WATU WASIOJULIKANA WANATOKEA RWANDA TUMUOMBE TUNDU LISSU
Kuna shule ya upadri? na kuna mtu anasomea upadri? Mtoa mada usijipachike vitu usivyovielewa vizuri.
 
Wakuu natanguliza salamu .

Maelekezo makuu ya Mungu kwa wanadamu ni kuishi katika kweli iliyojaa haki tupu , kutenda mema na kukataa maovu , hivyo tunategemea kiongozi yeyote wa dini ya kweli aishi na atende kama Mungu alivyoelekeza .

Kardinali Pengo anatenda kinyume na Maagizo haya ya Mungu , ni wazi ameamua kujipambanua kuukumbatia unafiki , Amejipachika usemaji wa Kanisa kinyume cha utaratibu .

Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Naomba kuwasilisha .

Halafu mnaajiita wademokrasia. Mtu akiwa na mawazo tofauti na wewe mnamfukuza. Ni ngumu sana kuficha unafiki.
 
Mzizi wa CCM ni mpana sana hata yule unaemwamini ni mwenzio kumbe akitoka hapo alipo anaenda kupeleka report yake Lumumba.
 
Mleta Uzi, uwe mkweli. Wewe si Mkatoliki. Hiyo tone yako si ya Kikatoliki. Wakatoliki hatunaga retribution katika jambo lolote. Lkn siku zote tunajua maana ya "Roma Locuta causal finita". Hiyo ndiyo imani yetu. Maneno uliyosema hapo juu ni purely against what we believe in. Tunachukia dhambi na si mtenda dhambi.
 
Huyo hata asipofukuzwa umri wake na mawazo yanaonyesha amefikia mwisho

Badala atende haki kumalizia safari yeye ndio kwanza anafanya kinyume chake

Hata hivyo huyu ni Mfarisayo tu hivyo usishangae anacho kitetea
 
anapigwa mapigo saba baba askofu Kadinali Pengo si bure huwezi ukjishusha kuwa mtu wa majungu wakati unaongoza roho za mamimilioni ya watu
 
Wakuu natanguliza salamu .

Maelekezo makuu ya Mungu kwa wanadamu ni kuishi katika kweli iliyojaa haki tupu , kutenda mema na kukataa maovu , hivyo tunategemea kiongozi yeyote wa dini ya kweli aishi na atende kama Mungu alivyoelekeza .

Kardinali Pengo anatenda kinyume na Maagizo haya ya Mungu , ni wazi ameamua kujipambanua kuukumbatia unafiki , Amejipachika usemaji wa Kanisa kinyume cha utaratibu .

Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Naomba kuwasilisha .
Naomba nikuulize kosa lake ni nini? Kwani maneno ya Askofu Niwemgizi si ni msimamo wake binafsi? Ukumbuke na wala si msimamo wa jimbo lake la Rulenge. Unakosea sanaaaa na kutenda dhambi kwa kumhukumu kwa maoni yake. Cardinal ametoa naye maoni yake USIYOYAPENDA ila ukweli unabaki pale pale kuwa mpaka baraza la maaskofu likae ndipo linaweza kutoa msimamo wa kanisa katoliki hapa Tanzania. take it or reject it its your wish mkuu
 
Back
Top Bottom