Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,356
- 21,390
Sidhani kama kuna mtu anapinga Mahakama ya Kadhi,ila tunachopinga ni nani aigharamie Mahakama hiyo?Je ni halali kwa serikali kuigharamia ilhali walipa kodi ni wakristu na waislamu? Je kama Mkristu Mahakama hiyo inamsaidiaje?Kama waislamu wenyewe wanauwezo wa kuigharamia mahakama hiyo wamepewa ruhusa ya kuifungua na kuitumia.
Swala la NECTA sidhani kama linaukweli kwani kuna watoto wakiislamu waliosoma shule za Wakatoliki au Wakristu na wamefaulu vizuri kuliko hata wakristu wenyewe,tatizo ni bidii za watoto wetu kujifunza na kutilia maanani masomo na shule.Makosa mdogomadogo yasifanye tatizo kuwa kubwa sana.Nina historia na kusoma na mabinti kutoka Handeni miaka ya themanini ,mabinti wale walikuwa shule hawaithamini kabisa na wengi walifeli karibu asilimia tisini na tano ya wasichana toka Handeni walifeli,je utawalaumu walimu au NECTA?
Tuwafundishe watoto wetu kujali masomo bila kuangalia udini wao,kwani taifa letu limejengwa na watu waimani tofauti (wakristu,waislamu,wapagani wahindu N.k)
Hata huyo mtoto mkristu leo kesho anaweza akabadili kuwa muislamu na muislamu kuwa Mkiristu,tusiwabague watoto wetu.