Paul Sozigwa amepotea katika mazingira ya kitatanishi

kijana acha dharau.

Mali gani ya kawawa imeuzwa na serikali ikauchuna?

Kwahio unataka kutuaminisha kwamba wale wote walouhujumu nchi yetu na sasa wanafaidi matunda ya hujuma zao walifanya hivyo kihalali kwa sababu serikali haihusiki na maisha yao ya mafao?

richard fuatilia utapata jibu yule mama wa tbr alichokifanya, hata hivyo sozigwa hajahujumu nchi kwa lolote sijui wewe umelipata wapi hilo?
 
Kova tena ??? umm
Ila nakubaliana huyu mzee ni mtu wa heshima zake kwa sana. Nimebahatika kuishi nae jirani...hawa ndiyo sampuli ya kweli ya mwalimu....nimesikitika kusikia mke mdogo sijui kauza nyumba yake !!
 
richard fuatilia utapata jibu yule mama wa tbr alichokifanya, hata hivyo sozigwa hajahujumu nchi kwa lolote sijui wewe umelipata wapi hilo?

Nimekujibu kutokana na hoja yako soma tena sentensi yako ya kwanza.

Na ndio nikakuuliza masuali.
 
Watu wa aina hii waliolitumikia Taifa yangu enzi za Uhuru walipaswa kutazamwa kwa karibu. Mzee kaachwa aishi kilofa kana kwamba hakuna la maana alilofanyia Taifa hili. Utawala huu ndo umemuumiza kabisa huyu mzee baada ya kubeba mafaili yaliyojaa 'escrow' za Dk. JK. Mungu ni mwema. Tuongeze dua.

Enzi ya Uhuru alitumikia nini? Wacha uongo.

Hao ndiyo waliiuwa nchi kwa kutetea siasa iliyokuwa haina kichwa wala miguu iliyoipelkea hii nchi kuwa masikini wa mwisho duniani. Huyo si ndiyo alikuwa akitangaza mazungumzo baada ya habari baada ya azimio la Arusha? sasa alitumikia nini wakati wa Uhuru?

Hapa tuongee kupotea kwake, lakini tusilete uongo.
 
Umesimuliwa udaku nimeishi nao miaka yote sasa unaposema kila kitu sijui unamaanisha nn !! Huyu Moses ( aka bonge enzi za utotoni) tumesaga nae sana, mabasi na hata walipokuwa forodhani ilikuwa mara moja moja kuletwa na gari...tena asubuhi tu, mchana tunapiga mihogo kwa mzee Mselemo na kudandika ikarusi kwenda home..

Viatu ni bora tuu na hata watoto wa kawawa akina Amani walikuwa wanawacheka hawa..! Sasa wewe unataka kutuambia nn..? Sawa na haya majangili akina Rz1 ??

Kwa taarifa yako sozigwa alikua na kila kitu yani alikua sawa lakini kapeleka chini street.mzaramo yule alikua hatari enzi zake.
 
Mama, mzee Sozigwa alisomea uandishi wa habari London University na baadae akateuliwa na wakoloni wa Uingereza kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe miaka ya mwishoni mwa 50 na mwanzoni nwa 60 na wakti huo Mwalumu ameanza shughuli za siasa.

Wakati Sozigwa anachaguliwa kuwa katibu wa Mwalimu mwaka 1967 alitokea wizara ya habari na utalii na iiuwa kabla Azimio hilo halijatangazwa.
 
Umesimuliwa udaku nimeishi nao miaka yote sasa unaposema kila kitu sijui unamaanisha nn !! Huyu Moses ( aka bonge enzi za utotoni) tumesaga nae sana, mabasi na hata walipokuwa forodhani ilikuwa mara moja moja kuletwa na gari...tena asubuhi tu, mchana tunapiga mihogo kwa mzee Mselemo na kudandika ikarusi kwenda home..

Viatu ni bora tuu na hata watoto wa kawawa akina Amani walikuwa wanawacheka hawa..! Sasa wewe unataka kutuambia nn..? Sawa na haya majangili akina Rz1 ??

Mkuu unanikumbusha kiatu kimoja hivi tulikuwa tunakiita mkuki moyoni.

Kilikuwa kina laizoni ndefu kidogo.

lol

Halafu mkuu ulikuwa class gani?

Da! umenikumbusha mzee mselem

Mihogo ya kuchemsha na kachumbari baadae akaja Mangi na chips zake.
 
Mzee wa Mazungumzo Baada ya Habari (MBH) cha RTD. Nakumbuka alivyotunanga tarehe 12 Mei 1990 UDSM ilipofungwa kwenye MBH iliyopewa kichwa LY (Last Year). Alisema LY katika shule yao walikuwa nabvituko vingi, lakini kimojawapo ni kuvaa nguo ya ndani kichwani. Sasa anawaona kila LY halisi. Mungu amsaidie.
 
Namkumbuka mzee paul sozigwa ndiye aliyemshauri mwalimu astaafu ili apishe watu wengine wasimamie mageuzi ya kiuchumi kwani asingeweza kupingana na misimamo yake.

Baada ya maelezo ya sozigwa mawaziri wanafiki kama malechela walitegemea mwalimu angehamaki na kumfuta kazi mwalimu, badala yake mwalimu alikuwa mpole na kumsifu sozigwa kwa ushauri wake.

Baada ya kikao kile mwalimu alimwita Cleopa Msuya na kumpatia kazi ya kusimamia mageuzi kama alivyopendekezwa na tume ya paul bomani. Msuya akapewa kazi ya kuzungumza na world bank na IMF juu ya reforms za kiuchumi na hapo mzee akaanza safari ya kung'atuka.

Kwangu mie mzee sozingwa kupotea kama mlevi wa kimpumu sikubaliani hata kidogo, nakumbuka mara ya mwisho nilimwona akiwa na Majidd Mjengwa sweden alikokuwa kwa matibabu, chonde JK hakikisha huyu mzee anapewa heshima inayostahili.

Naongezea tu!
Huyu mzee wetu ni mtu muhimu sana maana 2005 kule zanzibar ndiye aliyekwenda na file lenye data za mukulu za kukosa uadilifu.ukiunga na sunami la mabadiliko nahsi kuna jambo pia.
 
Kazi ya kutelekeza wazee na hata wazee watumishi wa uma wa ngazi za juu miaka hiyo sio wengine ni hawa sisiemu alafu bado mnawakumbatia

Lazima tuwapige chini ccm mmetutesa sana tokea Enzi mpaka sasa mnatuongoza ki dikteta na kutuuma kama panya huku mnapuliza mwisho wenu umefika....
 
Kwa taarifa yako sozigwa alikua na kila kitu yani alikua sawa lakini kapeleka chini street.mzaramo yule alikua hatari enzi zake.

Mkuu wakati wa akina Sozigwa miiko ilikuwa inawabana.. Kiongozi hakutakiwa awe na hata nyumba ya kupangisha.. Kama alikuwa anapata hela ni kutokana mshahara na marupurupu mengine.. Wakati huo chama kilikuwa ni cha wakulima na wafanyakazi.. Kama wangeamua kupiga kama hawa wa sasa hivi sidhani kama kungekuwa na salio ambalo hawa viongozi unaowaona wewe ni wajanja wangezikuta mali na ardhi wanazodhulumu sasa..!

Ndo maana nikasema walitegemea wakistaafu waishi kwa pensheni ambayo ingeweza kuwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku..

Halafu Mkuu usidhani wote hatumfahamu huyu Mzee kiundani.. Hayo uliyoyasema hapo juu ni kutaka tu kumkosea adabu, ni vizuri ukawa na busara linapokuja suala linalomhusu mtu binafsi.. Sidhani kama utapenda ulichoandika wewe hapo juu kiandikiwe na mtu mwingine lakini akimlenga mzazi wako..
 
Back
Top Bottom