Mwenyekiti JET: Elimu ya utunzaji mazingira iingizwe kwenye Mitaala ya Elimu kuanzia ngazi ya chini

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
104A3721.JPG
Umoja wa Maafisa Watendaji Wakuu Tanzania wakiwemo wa Mashirika Binafsi na Serikali (CEOrt) wakishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (Journalists' Environmental Association of Tanzania – JET) wamekutana na Wadau mbalimbali katika warsha ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, leo Februari 29, 2024.

Warsha hiyo iliyofanyika Hyatt Kilimanjaro Hotel Jijini Dar es Salaam ambayo ilibeba mada inayohusu “Kufafanua Jukumu la Vyombo vya Habari katika Kuendesha Ajenda ya Hali ya Mabadiliko ya Hewa” ililenga kutoa elimu kuhusu njia zinazoweza kutumika kufikisha ujumbe kwenye jamii na jinsi Wadau wanavyoweza kushirikiana kusaidia jamii katika mabadiliko hayo.

Mmoja wa walioshiriki na kupata nafasi ya kuchangia mada ni Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Santina Benson ambaye umoja anaouongoza una Wanachama 200.
104A3802.JPG

104A3763.JPG
Jacqueline Senyagwa, Mtafiti wa Mazingira
Akizungumza katika tukio hilo, alitoa wito kuwa kuna umuhimu wa jamii kutambua kuwa kila mtu anatakiwa kushirikia kwa kuwa binadamu wote wamezungukwa na mizingira.

Anasema “Inabidi tuwe sehemu ya mikakati ya kudhibiti uharibifu wa mazingira ikiwezekana kuiga mifano ya nchi zilizoendelea, inawezekana tusiinge kile wanachokifanya moja kwa moja kwa kuwa mazingira yetu ni tofauti lakini tunaweza kujifunza kitu.

"Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanaweza kuwa na athari za kiuchumi na zisizo za kiuchumi, mfano uharibifu wa mazingira ukitokea unaweza kusababisha vifo, kupotea kwa tamaduni, uharibifu wa miundombinu, uharibifu wa mazao na mengine mengi.

"Ni muhimu kuendelea kutoa elimu mara kwa mara kuhusu mazingira na madhara yake."
104A3894.JPG
Ellen Utaru Okoedion (JET):
Ellen ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) anasema uzoefu unaonesha watu wanaokua wakiwa katika mazingira chanya (positive) wanakuwa na fikra chanya pia.

Anasema watu wa aina hiyo wanapata nafasi ya kufikiria na kuwa wabunifu kuliko ambao wanakuwa katika mazingira mabovu au ambayo si rafiki, anasisitiza kuwa uharibifu wa mazingira unaweza kuwa na madhara mengi ya kijamii ambayo yanaweza kuathiri watu wengi.

Anasema “Ili kuwa na mazingira mazuri ya kuishi pamoja na biashara tunatakiwa kuwa na mazingira bora pia, hapo ndipo kunaingia umuhimu wa Media katika kusaidia jamii kuelewa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

“Elimu ikianza sasa na kuwa endelevu itafanya jamii iweze kuwa na uelewa mkubwa kuhusu changamoto ya kukabiliana na mazingira, muhimu ni kuwa tunahitaji kuwa na Vyombo vya Habari vinavyoelewa uhalisia wa mazingira ya sehemu husika.”
1.png

2.png
Swali? Kwa nini elimu ya mazingira ipo chini Tanzania?

Ellen:
Jibu lipo wazi, ni kwa sababu hatuna elimu nzuri ya mazingira kuanzia ngazi ya elimu ya chini.
Elimu tunayofundishwa ni kufagia, kupanda na kumwagilia maua pamoja na vitu kama hivyo, kiuhalisia elimu kama hiyo ni sehemu ndogo sana ya kile ambacho kinatakiwa kueleweka kwenye jamii.

Unapozungumzia Elimu ya Mazingira ni kama kitu kigeni Tanzania, mfano tunatakiwa kutambua masuala ya matumizi ya nishati ni sehemu ya mazingira.

Kwa ufupi Watanzania wengi hawaielewi elimu ya mazingira kwa upana wake.

Tunatakiwa kuingiza elimu ya mazingira katika mitaala yetu, hilo linatakiwa kufanyika kuanzia katika ngazi ya chini na liwe somo endelevu, kila hatua wafundishwe kulingana na uelewa wao hadi wanapofika ngazi ya chuo.

Sisi kama Wadau wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na mazingira kwa jumla tumewasilisha hilo, na limepokelewa Wizarani lipo kwenye mchakato.

Pamoja na yote elimu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa inatakiwa kutolewa hata katika taasisi na maeneo mengine mfano kazini, viwandani na kwenye mikusanyiko mbalimbali.

Nitoe mfano, unapopata nafasi ya kuzungumza na Mama Lishe wa mtaani unatakiwa kujua jinsi ya maneno ya kuzungumza naye kuhusu mazingira badala ya kwenda na ‘approach’ ya mambo magumu.

Mtu kama huyo unatakiwa kuanza naye kwa kumuelezea athari za uharibufu wa mazingira hasa zile ambazo zinamuhusu yeye kwa ukaribu ili akuelewe, kisha umpe utatuzi, hautakiwi kuishia kumwambia matumizi ya mkaa hayafai, untakiwa kumfafanulia kivipi na atafanya nini kama njia mbadala.

Kingine cha muhimu kuna haja ya taasisi, watu binafsi na wengine wote wanaohusika kutka kufikisha ujumbe kwenye jamii kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa kukutana na wadau wanaohusika na wenye uzoefu katika fani husika, mfano unaweza kushirikiana na JET ili kurahisisha matumizi ya lugha nan jia nzuri za kujua namna ya kufikisha ujumbe wako.
104A3836.JPG
Dr. Dastan Kamanzi (TMF)
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) naye alipata nafasi ya kuzungumza kwa kuwasilisha andiko kuhusu umuhimu wa Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari kwa jumla kujua njia za kufikisha ujumbe unaohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa kwa jamii katika njia sahihi pamoj na changamoto kadhaa.

Anasema…
Kwa kawaida binadamu ana pande mbili, moja anayoonekana (mwili) nyingine ni akili na fikra hizo hazionekani kwa macho lakini unaweza kuzijua kupiti matendo yake, hivyo mazingira yanayomzunguka yanaweza kukupa picha huyo ni mtu wa aina gani.
3.png

104A3930.JPG
Swali: Kwanini stori za mazingira hazipewi nafasi kubwa kwenye Vyombo vya Habari?
Kamanzi:
Suala hilo lina ukweli japokuwa kuna sababu kadhaa, kwanza taarifa za mazingira zinaweza kutotumika au kutopewa kipaumbele kutokana na aina ya uandishi au uwasilishaji unaotumika.

Jambo la muhimu ni kuwa Mwandishi anaweza kutumia njia mbalimbali au engo tofauti ili kufanya ujumbe wake uendane na mazingira husika.

Wanahabai wengi wanachangamoto namba ya kuuweka ujumbe wao wanaoupeleka katika jamii, matokeo yake unaonekana haufai kuanzia ngazi ya ndani (katika chombo cha habari) hadi nje kwa walaji.

Jambo lingine ni kuwa hakuna ‘specialization’ kwa Waandishi, yaani wanaojikita katika habari za aina fulani mfano wa zile za mazingira ni wachache.

Hali ya aina hiyo inasababisha Wahariri au wakuu wa madawati ya Vyombo kutokuwa na watu sahihi pia nao wanakuwa na tamaa ya kuhisi kile kilichofanywa na Mwandishi wake kina manufaa makubwa na kulazimisha wagawane, hiyo yite ni njaa iliyopo katika tasnia.

Muhimu pia Wanahbari wanatakiwa kujifunza na ikiwezekana kuwashirikisha wataalam wa fani husika ili kurahisisha kazi zao, mfano kuwarahisishia matumizi ya lugha inayotumiwa na wataalam, kwani kuipeleka lugha ya kitaala kwa mwananchi wa kawaida ni jambo gumu kueleweka.
 
Elimu ya mazingira ipo kwenye mitaala yetu tangu zamani ila tatizo kubwa watu Huwa hawazingatii mambo yanayofundishwa na pengine ni kwasababu ya umasikini.
Umasikini unaweza kusababisha kutengeneza vizazi visivyozingatia mafunzo na hata kutengeneza vizazi visivyo na ubunifu chanya.

Elimu ya mazingira inafundishwa tangu elimu ya msingi Hadi elimu ya juu. Hivyo Ikiwa tutaamua elimu hiyo itolewe kupitia somo lake maalumu basi tutalazimika kufanya marekebisho kwenye masomo yanayofundisha kuhusu mazingira kwa maana ya kuondoa mada zinazohusu mazingira kwenye masomo kadhaa.

Mfano: kwenye shule zetu Kuna baadhi ya masomo kama Geography, biology, Chemistry n.k zipo baadhi ya mada zinafundisha umuhimu wa kutunza mazingira, jinsi ya kutunza mazingira, athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira, jinsi ambazo hewa anaweza kuchafuliwa, jinsi ambavyo mabadiliko ya joto yanaweza kutokea n.k
Kwahyo elimu yetu Ina mitaala ambayo haihitaji mabadiliko mengi ila inahitaji watu ambao wanaweza kuitumia kwa ufanisi.

"Kila jambo ambalo linaweza kufanywa kwa vitendo basi wazo ndilo linaloanza"
Mfano lipo wazo la kwamba nishati haiwezi kutengenezwa Wala kuharibiwa Bali inaweza kuhamishwa/kubadilishwa kutoka aina Moja na kuwa aina nyingine.
Sasa kutokana na wazo Hilo watu wakawaza kubadilisha nguvu ya jua kuwa umeme, nguvu ya mjongeo kuwa umeme, pia watu wakabuni kutumia maji kutengeneza mjongeo wa kuzalisha umeme.

Elimu>>Wazo>>Vitendo>>Mazao.
 
Back
Top Bottom