Paul Sozigwa amepotea katika mazingira ya kitatanishi

Watu wa aina hii waliolitumikia Taifa yangu enzi za Uhuru walipaswa kutazamwa kwa karibu. Mzee kaachwa aishi kilofa kana kwamba hakuna la maana alilofanyia Taifa hili. Utawala huu ndo umemuumiza kabisa huyu mzee baada ya kubeba mafaili yaliyojaa 'escrow' za Dk. JK. Mungu ni mwema. Tuongeze dua.
Sasa kama hakujipanga jakaya inamuhusu nini?Mbona mwenzie mtei na msuya wapo safi? Hawa wazee walijisahau walidhani watakaa ikulu milele,
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV saa 2 usiku huu kuwa Mzee Paul Sozigwa amepotea nyumbani kwake Magomeni. Huyu mzee alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM zama za Mwalimu JKN

Enzi hizo kulikuwa na vichwa kweli kweli, eti sasa hivi katibu mwenezi Nape!!!!
 
Sasa kama hakujipanga jakaya inamuhusu nini?Mbona mwenzie mtei na msuya wapo safi? Hawa wazee walijisahau walidhani watakaa ikulu milele,

Mkuu hii siyo kauli ya kuisema.. Huyu ni mmoja wa wazee ambao waliitumikia nchi kwa kufuata miiko ya uongozi.. Tulitegemea wazee kama hawa waishi kwa pensheni lakini kwa gharama ya maisha yalivyopanda malipo yao yamebaki kwa kiwango kile cha zamani..! Matokeo yake wanajikuta wanapata Tshs. 50,000 tu kwa mwezi..! Tunawalipa pesa hiyo kiduchu kwa ajili ya uzalendo wao..

Leo wewe unawadhihaki hawa na kuwacheka ujinga, lakini hawa ambao wanapora sasa na kuuza mali za watanzania wote kwa faida na maslahi yao binafsi ndo unawaona wajanja sio..!
 
Unamjua vizuri Paulo Sozigwa au unaongea tu?
 
Namkumbuka mzee Paul Sozigwa ndiye aliyemshauri Mwalimu Nyerere astaafu ili apishe watu wengine wasimamie mageuzi ya kiuchumi kwani asingeweza kupingana na misimamo yake.

Baada ya maelezo ya Sozigwa, mawaziri wanafiki kama Malechela walitegemea mwalimu angehamaki na kumfuta kazi mwalimu, badala yake mwalimu alikuwa mpole na kumsifu sozigwa kwa ushauri wake.

Baada ya kikao kile mwalimu alimwita Cleopa Msuya na kumpatia kazi ya kusimamia mageuzi kama alivyopendekezwa na tume ya Paul Bomani. Msuya akapewa kazi ya kuzungumza na world bank na IMF juu ya reforms za kiuchumi na hapo mzee akaanza safari ya kung'atuka.

Kwangu mie mzee Sozingwa kupotea kama mlevi wa kimpumu sikubaliani hata kidogo, nakumbuka mara ya mwisho nilimwona akiwa na Majidd Mjengwa Sweden alikokuwa kwa matibabu, chonde JK hakikisha huyu mzee anapewa heshima inayostahili.
 
Mkuu hii siyo kauli ya kuisema.. Huyu ni mmoja wa wazee ambao waliitumikia nchi kwa kufuata miiko ya uongozi.. Tulitegemea wazee kama hawa waishi kwa pensheni lakini kwa gharama ya maisha yalivyopanda malipo yao yamebaki kwa kiwango kile cha zamani..! Matokeo yake wanajikuta wanapata Tshs. 50,000 tu kwa mwezi..! Tunawalipa pesa hiyo kiduchu kwa ajili ya uzalendo wao..

Leo wewe unawadhihaki hawa na kuwacheka ujinga, lakini hawa ambao wanapora sasa na kuuza mali za watanzania wote kwa faida na maslahi yao binafsi ndo unawaona wajanja sio..!

Nimesoma comment ya huyo kijana nimesikitika sana,nafikiri ni hawa vijana waliozaliwa 90s ambao ukiwauliza miziki ya zamani watakutajia ya Juma Nature! Hajui madhila yanayowafika hawa wazee kwa sababu ya uzalendo wao kwa nchi hii. Mungu asaidie mzee Sozigwa apatikane akiwa na afya njema.
 
Uzalendo upi? Wa kupeleka watu wakaliwe na simba?
 
Mkuu hii siyo kauli ya kuisema.. Huyu ni mmoja wa wazee ambao waliitumikia nchi kwa kufuata miiko ya uongozi.. Tulitegemea wazee kama hawa waishi kwa pensheni lakini kwa gharama ya maisha yalivyopanda malipo yao yamebaki kwa kiwango kile cha zamani..! Matokeo yake wanajikuta wanapata Tshs. 50,000 tu kwa mwezi..! Tunawalipa pesa hiyo kiduchu kwa ajili ya uzalendo wao..

Leo wewe unawadhihaki hawa na kuwacheka ujinga, lakini hawa ambao wanapora sasa na kuuza mali za watanzania wote kwa faida na maslahi yao binafsi ndo unawaona wajanja sio..!
Kwa taarifa yako sozigwa alikua na kila kitu yani alikua sawa lakini kapeleka chini street.mzaramo yule alikua hatari enzi zake.
 
Uzalendo upi? Wa kupeleka watu wakaliwe na simba?

It had to happen,maendeleo si lelemama.Wakitokea wasaliti lazima watoswe baharini safari iendelee.Uliza USA kabla states hazijaungana walikufa watu wangapi? Uliza China enzi za mwenyekiti Mao,sacrifices haziepukiki kwenye kufikia malengo.Mtakubali watu wachache watoboe boti/mashua nyote mfie majini au mtawatosa ili majority mfike Pwani?
 
Mkuu Kiwi,

Da! poleni sana na madhila haya.

Mama yenu yeye ana shida ya pesa na kama nyumba imeuzwa ilikuwa ni kwa ajili hiyo -pesa.

Je umetoa taarifa polisi? Mumuone kamanda Kovu mwenyewe mzee si anajulikana bana?

Polisi hawana shida watampata tu mzee ikiwa mama atawekwa ndani awasaidie kuwaambia alipo mzee kabla ya kesho asubuhi.

Hali ni ngumu lakini wewe ni mwanemme na uhakikishe mama hafanikiwi kwa kuwatumia ninyi kama ngazi ya mafanikio yake.

Hio ndio mali pekee mzee aloacha hivyo keep on fight
 
Poleni sana wanafamilia.Mungu ni mwema tena ni hakimu wa kimya kimya .tuko pamoja kila mtu kwa dini yake tunamuombea ..InshaalAllah ataleta rehma zake mtampata salama.
 
Kwa taarifa yako sozigwa alikua na kila kitu yani alikua sawa lakini kapeleka chini street.mzaramo yule alikua hatari enzi zake.

Acha kukomaa hata kama umepotoka,
Huo msemo wako ndio unaohamasisha watu kupiga hela kodi za wananchi ili tu asijekwambiwa alihonga wanawake na kulewa,

Labda kama wewe si mTZ, unafurahia maendeleo duni.
 
Watu wa aina hii waliolitumikia Taifa yangu enzi za Uhuru walipaswa kutazamwa kwa karibu. Mzee kaachwa aishi kilofa kana kwamba hakuna la maana alilofanyia Taifa hili. Utawala huu ndo umemuumiza kabisa huyu mzee baada ya kubeba mafaili yaliyojaa 'escrow' za Dk. JK. Mungu ni mwema. Tuongeze dua.

Msilaumu kila kitu yeye alikuwa anafanya kazi na analipwa mshahara KWA MUJIBU WA MKATABA WAKE NA MWAJIRI WAKE -SERIKALI YA TANZANIA ilikuwa ni juu yake kutayarisha maisha yake baada ya kustaafu na si zaidi ya hilo, serikali imfanyie nini tena wakati alishalipwa stahili zake zote KWA MUJIBU WA SHERIA YA CHEO CHAKE NA MKATABA WA AJIRA YAKE? je wako wangapi waliolitumikia taifa hili watatunzwa kwa gharama zipi?, ndiyo maana ikawepo sheria kuepuka upendeleo kinachotokea hapo ni matatizo ya uzee na pia matatizo ya ndoa serikali haihusiki na ndoa ya mtu wala familia yake kwa ujumla mbona vya kawawa vimeuzwa na serikali imeuchuna TU kwa sababu haihusiki. ILA NAAMINI ATAPATIKANA AKIWA MZIMA MKEWE HAWEZI HUSIKA KUMDHULU KWA SABABU TAYARI SIYO TISHIO KWENYE INTEREST ZAKE (NYUMBA) KUTOKANA NA AFYA YAKE ILA ANGEKUWA MZIMA TUNGEHOFU JUU YA HILO.
 
Kijana acha dharau.

Mali gani ya Kawawa imeuzwa na serikali ikauchuna?

Kwahio unataka kutuaminisha kwamba wale wote walouhujumu nchi yetu na sasa wanafaidi matunda ya hujuma zao walifanya hivyo kihalali kwa sababu serikali haihusiki na maisha yao ya mafao?
 
Back
Top Bottom