Pascal Mayalla: vyama vya Siasa visipewe ruzuku

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
769
1,959
"Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya utumishi wa chama ni wa kujitolea, chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa funded na wapenzi na wanachama, ifikie muda tuingie imani na Watanzania na umaskini wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku?,"....

Jana, Zitto nimemsikia anadai ruzuku, kama kweli ni kiongozi wa chama na unakipenda chama kwa moyo wako jitolee, uwe na shughuli nyingine ya kuendesha maisha yako utumishi wa chama uwe wa ziada, sio fedha za watanzania kwenda kugharamia vyama vya siasa," - Pascal Mayalla
 
Hakuna Upinzani wa kweli Tanzania

Mpinzani aliyebaki ni Tindu Lissu TU, sio Zitto sio Mbowe sio Lipumba

Ukiwanyima Ruzuku wataandamana na ikibidi wataua watu mpaka waipate

Na bado Ruzuku haitoshi kuna wakati wanahitaji support ya michango ya wanachama....lakini hata wasio wanachama wakitoa inapokelewa

Nani alijua kuwa akina Halima Mdee na Ester Bulaya wangekaribishwa na Mbowe katika harambee ya kuchangia kanisa hapo Nshara kwa kina Mbowe na kuzungumza na Mbowe muda mrefu nje ya kanisa?
 
Ruzuku vipewe ila vile kweli HAI,vyenye wawakilishi kwenye vyombo vya MAAMUZi ila sio hivi vya mifukoni..

Visipopewa CCM itazidi KUTAMALAKI na tutazidi kunyorooshwa hadi tukome

Pia KODI tunazotozwa na Serikali ni nyingi, bado tena TUVICHANGIE vyama vyetu?..hata kama ni HIYARI hapana..Mwisho tujue hii ndio GHARAMA ya Demokrasia
 
Back
Top Bottom