Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Akiwa ndani ya Sabasaba na PPR na baada ya kuona bidhaa fulani inayovutia katika banda la maonyesho, hukosi kumsikia akinena, "……….utafikiri vinatoka ulaya…." au atajishtua na kuuliza "………hivi kweli hivi / hizi si ready made……..?".
Kaka yangu Mayalla,
1. Haijalishi unafanya mzaa au unataka kunogesha kipindi chako; matumizi ya mara kwa mara (kwenye public media) ya kuona kitu kizuri unasema kinatoka Ulaya au nje ya nchi ni mabaya sana na ni dalili za ukosefu wa kuwa na mawazo mapana. Aidha matumizi hayo yanaweza kuwa na athari kwa jamii (hususani watoto na vijana) ambao wanaangalia TV na kumsikia Mwanahabari mzoefu na Mwasisi wa Kiti-Moto kama wewe unakiri kwa kinywa (by implication) kuwa vizuri vinatoka Ulaya au nje tu kwa kutoweka TAHADHALI mwanzoni au mwishoni mwa kipindi chako kuwa baadhi ya maneno yako unayoyatumia (kama hayo) ni ya kuchekesha tu na yasichukuliwe maanani.
2. Tena utambulisho wa ‘ready-made' kwa bidhaa zenye mvuto au ubora ni wa utata mkubwa sana. Hivi ‘ready-made' huwa ni already made toka lini na nini na nani? Je, kuna bidhaa tunazipokea toka mbinguni kama mikate iliyodondoka pale jangwani kwa wana wa Israel? Maana wao wangeweza kusema, "We received Manna prepared / processed / ‘ready- made by Allah". Kama unamaanisha ‘already processed', je ni nani alisema kuwa bidhaa zinazoonekana katika mabanda yote hayo hazijawa processed kwa namna moja au nyingine?
Mayalla angalia sana wewe ni kioo na kwa kupitia chombo kikubwa cha mawasiliano kama TV na Asasi yenu ya PPR unaweza kupotosha sana jamii kama sio na wewe pia kuendelea kujipotosha na kujiaibisha. Tafadhali achana kabisa na matumizi mabaya ya hiyo misamiati unapotangaza biashara ya Watanzania!