Pasaka hii twende tukapumzike Kisiba Campsite. Hautojutia, wewe na umpendaye

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
1706590476034.jpg

Kisiba Campsite Ni Eneo la Kitalii linalopatikana Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Shughuli unazoweza kufanya, Uwapo eneo la kisiba unaweza kufanya shughuli mbalimbali za kitalii ikiwemo kuogelea (Swimming) kupumzika , Kuendesha boti la muanzi (canoeing with bamboo boat) matembezi ya kulizunguka ziwa, kupunga upepo, matembezi ndani ya msitu wa Kisiba, lakini pia mtalii anaweza kufurahia kufanya kambi.

Ukiachana na muonekano wa eneo hili la kitalii, pia ni eneo mojawapo lililojaa masimulizi mbalimbali ya wajerumani ikisadikika kwamba ndani ya ziwa hili wajerumani waliweza kutupa vitu vyao vya Thamani.

Vivutio vya kitalii vilivyo Karibu, Kisiba campsite pia iko karibu na vivutio mbalimbali vya kitalii ambapo mtalii akilala hapa ataweza kuvitembelea kwa uharaka sana ikiwemo, Maporomoko ya Maji Kapologwe, Majengo ya kale ya Wajerumani, Mti mkubwa wa katembo ambao unauwezo wa kuzungukwa na watu nane (8) mpaka kumi na mbili (12), Maji moto pamoja na maziwa mengine yaliyotokana na milipuko ya kivolkeno kama (Ziwa Ikapu, kyamba ngungulu, Itende, Ilamba, Kiungululu na Kingili lakini pia ni miongoni mwa njia fupi na ambazo utaweza kuona vivutio Vingi kuelekea Ziwa Nyasa (Matema Beach)

Namna ya Kufika, Kisiba Campsite inafikika kirahisi sana kwa usafiri binafsi unaweza kuingilia Tukuyu Mjini ama Ushirika pana umbali wa kilomita 18, lakini kwa usafiri wa Uma unaweza kushukia Tukuyu Mjini kisha ukapanda Noah zinazoelekea Lwangwa ama Itete Nauli Tsh 4,000/=, kwa pikipiki ni Tsh 7000/= mpaka 10,000/=

KARIBU TUKUYU RUNGWE KARIBU MBEYA TANZANIA
 
View attachment 2887995

Mbona uwasilishaji wa mada hapa JF uko nusu nusu sana? Kizazi gani hiki? Weka bei za vingilio watu wajue wanajipanga vipi, sio lazima mpaka uulizwe.
 
Back
Top Bottom