Papaa Musofe mbaroni kwa mauaji!

First person on the right..........

2.JPG

Umenifanya nicheke na hiyo signature yako. Ati a very small valley? LOL
 
Pedeshee Papa Musofe hawezi kushikiliwa na kituo cha Polisi kama Magomeni, Mutu ya Mbongo kama ni Polisi case basi ataombwa afike makao makuu ya Polisi au Central na si vinginevyo.

Hebu ngoja niwaulize wapambe wake kama leo order ya Supu pale MK ilikuwepo kama kawaida au lah!!
Na mkumbuke order ya Supu ni shilling laki mbili kwa ajili ya wapambe tu.
 
Gazeti la nipashe lina story ya kukamatwa kwake.
Aliua mtu alie mkopesha hela kwa kuweka rehani nyumba
 
Jamani tupeni hii habari in details.
[h=2]Papaa Msofe mbaroni kwa tuhuma za mauaji[/h]1st August 2012

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam linamshilikia mfanyabishara maarufu, Marijan Abubakari maarufu kama Papaa Msofe kwa tuhuma za mauaji.
Habari zinasema kuwa Papaa Msofe alikamatwa na Polisi juzi jijini Dar es Salaam na anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Magomeni jijini humo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha Papaa Msofe kushikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji.
“Ni kweli tunamshikilia Papaa Msofe katika Kituo cha Polisi cha Magomeni na tunaendelea kumhoji na kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na tukio analotuhumiwa nalo,” alisema Kamanda Kenyela.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kenyela, alisema Papaa Msofe alikamatwa baada ya kutokea mauaji ya Onesphori Kituli, mkazi wa Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.
Alisema kabla ya kutokea mauaji hayo, Papaa Msofe na marehemu walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Sh. milioni 30.
Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa na Kamanda Kenyela, zinasema kuwa bado kuna mtu mwingine ambaye anahusishwa na tuhuma hizo za mauaji, lakini mpaka sasa hajakamatwa.
Kamanda Kenyela alifafanua kwamba Papaa Msofe alimpa marehemu fedha hizo kwa makubaliano kwamba ikiwa atashindwa kuzilipa atachukua nyumba yake.
Kabla ya mauji hayo ilidaiwa kwamba, Papaa Msofe na mwenzake walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo.
Kamanda Kenyela alisema kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo, marehemu alifungua kesi mahakamani na kwamba siku ya hukumu alikutwa amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake na kwamba hakuna mali yoyote iliyochukuliwa.
Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya upepelezi kukamilika.

Source:
http://www.ippmedia.com/
 
Huyu huwa hatapeli, anawaibia wazungu mabwege! Ni kweli kwenye payroll yake pale polisi orodha ni ndeeeeeeeeeefu, kuanzia IGP, DCI, RPC.................................na kuendelea! Chunguza MJOMBA, utabaini!!
 
Hii siyo Case kwa Papaa Msofe take my word. huyu ana access ya kwenda mpaka kwenye vaults za BOT na kuwaonesha Wazungu kwamba zile dhahabu zote ni mali yake.

Polisi hawa wa Ulimboka hawana ubavu wa kumfanya lolote huyu jamaa, kama humjui Msofe kutana na wapambe wake kwanza utadhani umekutana na Matajili sembuse King maker mwenyewe. acha kabisa.
 
ooooh brother kamdedisha nani tena aaah sa ntapata wapi ugali wa kilasiku ngoja nikamcheki umwerani migomigo duu kweli malipo ni hapahapa kawaumiza watu weeeeeeeeee sas zam yake.le grand mupao mutu ya pakee duh rest in peaces brother
jamani leo unamkana brother!?hamna kesi hapo,hawatathubutu kukubali ajitetee maana atawaumbua wengi kutokana na ukaribu wake na jeshi la polisi na serikali, HATMA YAKE ITAKUA MAMBWDPANDE,
 
wanakutumia wee, wakikuchoka kosa dogo tu unakwenda nalo, jamaa anakwenda sasa, atakuwa soon papaa wa segerea
 
Da!chuma ya reli haipati kutu papaa musofe...jamaa kawaumiza sana watz wanyonge yeye na Alex Masawe
mkuu hapo kwa alex massawe sidhani kama ni sawa ndio ni marafiki na msofe ila wamekutana juzi tu miaka ya 2006 ila michezo yao tofauti kabisa....Papaa yeye ni conman na swindler while Mzee alex ni Retired Gangster....
 
Hii siyo Case kwa Papaa Msofe take my word. huyu ana access ya kwenda mpaka kwenye vaults za BOT na kuwaonesha Wazungu kwamba zile dhahabu zote ni mali yake.

Polisi hawa wa Ulimboka hawana ubavu wa kumfanya lolote huyu jamaa, kama humjui Msofe kutana na wapambe wake kwanza utadhani umekutana na Matajili sembuse King maker mwenyewe. acha kabisa.[/QUOTE ]


...Mkuu Mhalifu ni Mhalifu tu. Tusimpe sifa zisizostahili kwa sababu hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Kuna siku kila kitu lazima kifike Mwisho. Wako wapi kina Al Capone? Hata hapa Bongo mbona walikuwepo wahalifu wa kimataifa waliokubuhu lakini mwisho wa siku Walivaa pingu?? Anaweza akaepuka hata hili lakini Pingu zake zipo mahali zinamsubiri. Mark ma Words!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom