Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,999
- 46,826
Dunia ya sasa ili watoto waweze kufikia hali nzuri au za kawaida za kimaisha, waweze kujitegemea kwa kipato halali na kuishi maisha ya staha/"decent life" wanahitaji shule bora, vyuo bora, ajira bora, biashara zao au za wazazi wakimaliza masomo yao.
Bahati mbaya sana wazazi wengi wanazaa watoto wengi ambao hawawezi kuwapatia au kuwaongoza kupata hata robo ya haya mahitaji, matokeo yake wengi wanaangukia katika uhalifu kama huu wa Panya Road na kudanga. Wengine amboa hawapendi matatizo wanaishia kuwa madereva bodaboda na wamachinga wakiishi maisha ya kubangaiza ili mradi siku ipite.
Serikali, mashirika binafsi na raia wenyewe lazima sasa wafanye kampeni na mpango kabambe wa kuhakikisha idadi ya ongezeko la watu inadhibitiwa na raia wa nchi hii has maskini hawazai zaidi ya watoto wawili.
Mnaosema Tanzania ina idadi ndogo ya watu huku ikiwa na rasilimali nyingi hivyo raia wazidi kufyatua tu waonyeshini sasa Panya road hayo mashamba na mapori mnayosema yako wazi, waonyeshini hizo rasilimali ila watu waache kuishi roho juu mitaani mwao.