Panapo majaliwa mwakani nitajiunga rasmi na siasa za nchi hii. Je, ungependa nifanye siasa na chama kipi?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,619
52,415
Kwema Wakuu!

Baada ya kuzifuatilia Siasa za nchi hii Kwa takribani miaka kumi sasa, nachelea kusema mwakani Mungu akipenda nitajiunga na mambo ya Siasa.

Nitafanya Siasa za kuibadilisha nchi hii naam kuikomboa nchi hii pale walipoishia wakombozi wengine.
Nitafanya Siasa za kubadilisha fikra za watu wangu.

Nafahamu Siasa za nchi hii zinahitaji unafiki wa kiwango cha juu kabisa, lakini nitakapojiunga nitauweka mzunguko wangu katika haki isiyoumiza.

Nitawapa ukweli wautakao ukweli.
Nitakaa kimya kwao wasioutaka huo ukweli.
Nitawaheshimu wazalendo wa nchi hii, tena nitawapuuza kundi la mbwa mwitu.

Hata hivyo nitajiunga na Siasa Kwa sababu gani?
Je ni Kwa sababu za ulafi au tumbo langu?
Au je ni Kwa sababu ni sehemu ya Ajira?

Hasha! Nitajiunga na Siasa ili kukamilisha ukombozi Kwa wale niliopangiwa niwakomboe. Nitamaliza zamu yangu Kwa miaka isiyozidi miaka kumi na tano, kisha nitarudi katika ukuhani na kuwalingania watu na kujilingania Mimi mwenyewe.

Hapo nitadumu Kwa miaka mingine isiyozidi ishirini. Nitamaliza utume wangu. Nitapumzika nikikisubiri kifo Kwa hamu kubwa, naam kifo rafiki yangu tuliyepotezana tangu nilipozaliwa.

Nafahamu nchi hii wapo waliojimilikisha, wapo wajionao wakubwa, wapo wajionao ndio wenye midomo na mikono ya Kula.
Hawa nitajiunga nao, kisha watakapoona Mimi ni mwaminifu kwao hata wasinitilie Shaka, nitawakata mikono Yao, kisha nitaziba midomo yao na kuacha katundu kadogo wapate wala kupitisha kidogo cha wao kuishi.

MASIKINI wa nchi hii sitawakomboa isipokuwa watajikomboa wenyewe, wala katika Siasa zangu sitawakuwa Kwa ajili ya kundi lolote isipokuwa watu wote wa nchi hii.

Matajiri Kwa masikini
Werevu Kwa wajinga
Wenye hekima Kwa wapumbavu
Wasomi Kwa wasiosoma
Wanaume Kwa wanawake
Waumini Kwa wapagani.

Nitapiga Mbiu na kutangaza nchi hii ni Kwa watu wote, wazuri Kwa Wabaya, wema Kwa waovu, wenye macho Kwa vipofu, nguvu ya ukombozi itakaa mdomoni mwangu.

Ukombozi wa kumkomboa Tajiri katika Utajiri wake.
Ukombozi wa kumkomboa Askari magereza asiwe Kama mfungwa.
Ukombozi wa kuwakomboa Watawala wasiwe Kama Watumwa.

Wala sitajihusisha na watu wa chini, masikini, fukara na wanyonge.
Wala sitajihusisha na kukomboa wanawake.

Taikon atajiingiza katika siasa kukomboa maprofesa wasiwe Kama wajinga,

Tena nitakomboa wale wote wajiaonao wamekombolewa, nitawapa maisha Wale wote wajionao wanamaisha.

Nitawakomboa Wale wote wajionao hawateseki kumbe ndio wanaoteseka,

Kwa maana nimegundua katika miaka yangu ya utoto mpaka sasa yakuwa dunia inahangaika Kwa sababu watu hukomboa wasiostahili kukombolewa, huua wasiostahili kuuawa, hufunga jela wasiostahili kufungwa, huheshimu wasiostahili kuheshimiwa.

Basi huwezi kumkomboa masikini pasipo kumkomboa Tajiri, Kwa maana umasikini WA fukara huletwa na unyonyaji na ubinafsi wa matajiri.

Ili masikini akombolewe itampasa mkomboaji amkomboe Tajiri.

Tena huwezi kumkomboa mdhambi pasipo kumkomboa mtu Mwema, tena aliyemwema ndiye angepaswa kukombolewa ili Ile Hali ya wenye dhambi isionekane. Naam mwema ndiye hupaswa kuangamizwa ili kumuondoa Muovu. Na Kama ni Mungu alipaswa kuangamizwa ili Uovu WA Shetani usionekane, naam ndio maana Akamtoa Mwanaye(asiye na hatia) kufa Kwa ajili ya Uovu. Kwa wasioamini habari hizo basi wataamini katika habari za kafara au matambiko, kafara hutolewa iliyosafi wala haichukuliwi kafara chafu.

Kwa maana ujinga unaenea Kwa sababu ya werevu kukaa kimya.
Tena ubaya unaongezeka Kwa sababu ya Wema kukaa kimya.
Hivyo huwezi kuukomboa ubaya bila kukomboa wema(waliowema)

Taikon atajiunga na chama cha Siasa, atapangiwa miiko yake, lakini atavunja miiko ya kuheshimu watu waovu, Wabaya na wenye roho za ulafi.

Atakabiliwa na waovu lakini Kwa vile hapambanagi na waovu isipokuwa hukomboa waliowema basi atawashinda waovu automatically.

Kwa maana kila apambanaye na Uovu atashindwa, na wote waliopanbana na waovu walishindwa, Kwa sababu hakuna ukombozi Kwa watu waovu Bali upo ukombozi Kwa ajili ya watu wema.

Kama ilivyoandikwa, ushindane na mtu mwovu ndivyo Taikon atakavyofanya Siasa zake.

Na mwovu yeyote atakayetaka kupambana na Mimi atahesabika ni mtu Mwema atakaye ukombozi naye nitamkomboa, naye akataaye ukombozi Uovu wake utamuangamiza, naye hatahesabika nilimuangamiza Mimi.

Sitatetea masikini Kama walivyopita wengine, wala sitatetea wanyonge, mayatima na Wajane, Kama walivyojitangaza wengine.

Wala sitawakomboa waliokwenye Giza, isipokuwa nitawakomboa wenye nuru ili jury Yao izidi kung'ara wawaangazia waliogizani.

Sitawafanya mabubu waongee Ila nitawafanya wanaoongea waongee Kwa ajili ya mabubu
Sitawafanya vipofu waone Ila niwafanya wenye kuona wawaongoze vipofu wasioona., Kwa maana mwenye macho haambiwi tazama.
Sitawafanya viwete watembee Ila nitawafanya wenye kutembea wawabebe wasioweza kutembea.

Sitawafanya viziwi wasikie Ila nitawafanya wenye kusikia wawape maelekezo wasiosikia.
Kwa maana asiyesikia la Mkuu huvunjika Guu.

Taikon atakuwa real, hatavunja sheria ya nature ya Mama yetu Dunia. Tena atatimiza mapenzi ya Baba yake aishiye sirini.

Nami sitafufua watu katika makaburi Yao, Bali nitawapa waliohai nguvu ya kukumbuka haki za wafu waishio Duniani. Hayo yote nitayafanya.

Nami najua watakaonipinga ndio watahitaji uponyaji lakini uponyaji huo nitawapa wanaoniunga Mkono, Kwa maana wanaoniunga Mkono wakipona automatically wapinzani watakuwa wamepona. Wala sitapigana nao, Kwa maana uponyaji sio Kwa ajili yao.

Nitapeperusha bendera ya nchi.

Majeshi na vyombo vya Dola vitageuka Raia, na Raia nitawageuza vyombo vya Dola.
Kwa maana Jeshi hakuwezi kuwa Jeshi pasipo Raia kuwa Jeshi. Na kamwe Dola haiwezi kuwa Dola Kama Raia wake wakiwa hohe hahe.

Hata hivyo hayo nitayatenda pasipo kuyafanya, yatamkwa nami katika vinywa vya watu na mioyoni mwao.


Nitajiunga CCM?
Au je nitajiunga CHADEMA?
Au je nitajiunga chama gani?

Ngoja tuone mwakani.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
mkuu utatumbukia kwenye shimo la uongo,uzushi,upigaji na tamaa kama upo tayari kwa hayo basi ingia tu chama chochote.
 
Back
Top Bottom