Pamoja na yote, Dr. Slaa bado Atatinga Bungeni soon!

asilimia kubwa ya watanzania wangependa sana kumuona slaa akirudi tena bungeni.ila kamwe jk hatojaribu wala hata kufiria kumteua huyo shujaa eti arudi abungeni tena akaendelee kumvua nguo. Hapo ndo pabaya kwamba kisiasa silaa atunaye tena. Ila naamini lazima kwa hawa mashujaa wapya wanaoingia atatokea tu mmoja kama cyo wote wa kumrithi dk wa ukweli. Mungu bariki slaa,mungu bariki chadema.mungu bariki tanzania.

kauli yako arasululu inashiria kuwa elimu yako ya uraiai iko chini sana. Bungeni ni sehemu mojawapo ya utendaji wa siasa. Ipo kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa na chadema katika kipindi cha 2010-2015 nayo ni kukijenga chama kutoka ngazi ya juu hadi kufikia matawi na mashina. Kazi hii inatakiwa kufanywa kwa uratibu wa chadema makao makuu na katibu mkuu ndg w slaa ndio jukumu lake. Hiyo ni sehemu ya muhimu ya siasa kuliko kuwa bungeni.

Faida ya kukijenga chama hadi ngazi za chini kabla ya 2015, ni kuwa chadema itakuwa na watenda kazi kila kona ya tanzania na kupunguza urahisi wa kucahakachua kura za wagombea wake kama ilivyofanyika mwaka huu 2010. Kazi hii si ndogo, inaweza kufanywa na mtu makini kama nyerere aliyewe kujenga mtandao wa ccm kutoka chini mpaka taifa. Laiti asingefanya hivyo hawa aliowaacha nyuma wasingeweza kama ambavyo wameshindwawa kuendeleza mabenki, viwanda, mashamba n,k alivyoanzisha.

Wajibu wetu tunaopenda mabadiliko tunatakiwa tuachane na mtindo wa kushabikia siasa kwa msimu yaani wakati wa uchaguzi ili kukomesha wizi wa kura kama uliotokea 2010. Kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika mchakato wa siasa kwa wakati wote popote alipo kwa kufungua matawi ya chadema na kushawishi wapenzi wa chadema kujiunga katika matawi hayo ili chama kiweze kuwa na nguvu katika chaguzi mabali mbali.
 
ah ah ah! naona CHADEMA wamekubali kuwa padre mwasi Dr slaa kwisha kazi kachapa mweleka labda ajipange tena JK sio size yake hata kidogo..
 
Hizo ni njozi njema na mtabaki na labda!!!! yaani sasa huyu Slaa atakuwa mtu wa kuombea afe mbunge fulani jimbo fulani hata sumbawanga au karagwe etc..halafu adandie kugombea hilo jimbo??? lahaula kwata ama kweli siasa.......haya mjomba anza kufunga na rozali kwa sana kumbukuia enzi zako kabla hujausaliti ukatoliki,ili urudi bungeni kwa kifo cha mbunge yeyote aliyepo!
 
Ferds, huna haja ya kutukana watu wehu, kuwa spika sio lazima uwe mwanasheria, Chifu Adam Sapi Mkwawa hakuwa mwanasheria, Pius Msekwa hakuwa mwanasheria, Getrude Mongela wa Spika wa Bunge la Afrika, sio mwanasheria na Abrahman Kinana, aliyekuwa spika wa Bunge la Afrika Mashariki, ambaye ndio anayekuja kuwa spika wa sasa, sio mwanasheria, imetokea tuu kwa spika Stta ndiye mwanasheria.

Kinana? sawa pengine ni utabiri mzuri lakini bado hajachukua hata fomu. Lililo wazi ni kwamba Kinana hataki active politics vinginevyo angekuwa anagombea ubunge. Lakini labda kwenye ukatibu mkuu wa chama wanaweza kumweka hapo!
 
Slaa atarudi Bungeni kupitia jimbo la Hannang ambalo Chadema walimsimamisha Rose Kamili aliyeibiwa kura, na wamesema watapinga matokeo hayo mahakamani wakishinda, Slaa ndiye atagombea huko. Rose atakuwa ni mbunge tayari kwani atapita kwa wabunge wa viti maalum.
 
dk slaa amezoea vya kuchinja vya kunyongwa hawezi


angekuwa amezoea vya kunyongwa hapo.. vinginevyo hawezi
 
Back
Top Bottom