Pamoja na siasa chafu na rushwa tutashinda Arumeru Mashariki Lema (mb)

MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri’ vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

‘’Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema,” alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

‘’Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi,” alisema.

Msajili alisema; ‘’ujambazi wa siasa’’ hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
nao wanapaswa kuziepuka.

propaganda za magamba zimeanza,igunga udini walitumia udini, Arumeru mila na desturi kuzingatiwa brave lema mpaka kieleweke
 
kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru ................mh!!!!
 
Back
Top Bottom