Pamoja na siasa chafu na rushwa tutashinda Arumeru Mashariki Lema (mb)


Tungepata watu kama mia hivi wanaohamini maneno haya ya Kamanda Lema nchi ingekuwa imenyooka muda mrefu sana.Mimi natafuta nafasi hapa ofisini,nitakuwa na wapambanaji hata kwa siku moja kule Arumeru Mashariki,naamini kwa hakika wakati huu haki itashinda dhidi ya hujuma,udhalimu,ubadhirifu,uuaji,ufirauni,ushenzi,ujambazi,upumbavu,ujinga,ulaghai,ushetani,ujoka,uhafidhina nk ya CCM...

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Arumeru Mashariki ,Mungu Ibariki CHADEMA,

Ni kweli mkuu umenena.
 
Go go go kamanda LEMA waambie hao....QUOTE (Ni Afadhali vita inayotafuta haki na
usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha
utu wa Mwanadamu)
 
Mbunge mmoja wa CCM MwiguluNchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa badohazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja.
CCM bila pesa za rushwa kwishney kabisa badala ya kwenda kueneza sera yeye amekaa hotelini kusubiri pesa itumwe, oohh Nyerere njoo ukione chama chako ulichowaachia kina Mwigulu.
 
Ukiwa na vijana wenye nia ya dhati kama G. Lema Tanzania itakombolewa si siku nyingi zijazo. Hongera kamanda endelea kuwalisha vijana unga wa rutuba ili tumtoe bi Kirembwe madarakani.
 
Ritz umeshajibiwa,kwani lema kunisomeshea binamu yangu ni siri? Anamlipia ada ktk shule ya kata.
 
ccm wanataka kuanza wizi wao LEMA andaa makamanda wa kutosha, ccm hana chao Arumeru ndio maana wamehamua kumtumia Tedwa kama mlopokaji wa ccm
 
Jamani wanamageuzi wote, msitishike na propaganda za magazeti ya uhuru na habari leo etc kwani ni za ccm na tayari hao magamba wameshaanza kupiga kampeni zao chafu but ukweli utabaki palepale kuwa lema ni tishio kwa ccm.
 
Duh!Acha CDM isonge mbele...ukweli imesheheni vichwa...nashawishika kabisa kuwa huu ni mpango wa Mungu kuwakomboa Watanzania kupitia CDM...Kampeni hazijaanza...CDM hawajapitisha jina la mgombea wao Arumeru Mashariki...Lema ni Mbunge wa Arusha Mjini...Lakini CCM tayari wanahaha kumu sapresi Lema...!!??Yangu macho na masikio...Na ninaomba iwe hivi:Mgombea Joshua Nasari;Kampeni Meneja:Godbless Lema....
 
chonde chonde Lema kesi ya kutumia lugha ya matusi wakati wa kampeni za kugombea Ubunge jimbo la Arusha mjini imekukalia vibaya mahakamani ukifika Arumeru punguza jaziba mwaga sera.
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri’ vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

‘’Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema,” alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

‘’Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi,” alisema.

Msajili alisema; ‘’ujambazi wa siasa’’ hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
nao wanapaswa kuziepuka.


Tendwa alikosea kuongea na waandishi wa habari angewaunganisha hao wazee na waandishi wa habari na wajulikane.
Hapo tunajua M/kiti wa kijiji katafuta jinsi ya kupakua mfuko wa Tendwa kaona aingie kwa jjea hiyo, sasa tuone kama Tendwa hujaumbuka. Kitakachowasaidia kutoa aibu labda ni pesa mnazo mwaga wakati wananchi wanaendelea kufa masikini.
 
Kamanda Lema we unajulikana kwa ushindani wa hoja na si nguvu.
Mahali popote unaposimama wanamagamba wahisi kwenda 'call'.
Tunakuamini, tunakuthamini na tuko nyuma yako.
Uchaguzi wa Arumeru si kama chaguzi zingine, watu hawako tayari kuvishwa kanga, kofia na fulana wanataka maendeleo.
Huyo pashkuna mmendea wake za watu asifikirie huku kuna mwanamke atamshobokea, akicheza anadhiriwa hadharani. Kwanza magamba kuweni makini na wake zenu wanaohudhuria utratibu wa mikutano yenu akichelewa kurudi ujue anam entertain bwana mkubwa wenu!!!!!!!!!!! Haha ha haaaa, ndo kazi imemleta huku sijui anafikiri na huku wako that loose?
MAPAMBANO DAIMA;
CHADEMA KWA MAGEUZI YA KWELI,
KATIBA MPYA,
ERADICATIONOF MAFISADI NA
UREJESHAJI WA RASLIMALI KWA USTAWI WA TAIFA.
 
Back
Top Bottom