Pamoja na siasa chafu na rushwa tutashinda Arumeru Mashariki Lema (mb)

Labda huko hakuna wapiga kura Wamasai na Lowassa asiende. Lakini kama kuna wamasai, unajuwa Laibon wao nani? na akisema kitu huyo hapingwi.

Kwani Arusha mjini hakuna wamasai? Mbona kimada wa huyo Laibon alibwagwa vibaya.
 
Hakika Lema ni shujaa wa kweli.Mimi nadhani kwa vile Jihn Mrema ni kamanda mkuu wa operesheni basi Meneja wa kampeni awe Lema.
 
“PAMOJA NA SIASA CHAFU NA RUSHWA TUTASHINDA ARUMERU MASHARIKI”

Nawasalimu

Leo asubuhi nimesikia habari za uzushi na majungu kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi Uhuru pamoja na gazeti la serikali la Habari leo . Hivyo basi kilichosemwa na magezeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 23/2/2012 ni uzushi na propaganda , Magazeti haya ya CCM yatatumika sana kipindi hiki kama yalivyotumika kule Igunga yalipojaribu kutaka kuwatenganisha watu hata kwa dini zao lakini baadae ukweli ulijulikana na ikawa aibu kwao .
Kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Taifa letu kutoka kwa mkoloni bado Watanzania wa Arumeru sio huru na Watanzania wote kwa ujumla bado wanaishi maisha magumu kama wakimbizi nje ya Nchi yao.
Ninafahamu wajibu wangu katika kupigania demokrasia safi ya Nchi yangu na wakati huu jimbo la Arumeru Mashariki litakuwa mfano wa mapambano hayo na nitakuwa mstari wa mbele bila hofu wala kumuogopa mtu yeyote na wa cheo chochote katika kupigania ukweli na haki.
Wajibu wangu na wa chama changu kwa sasa ni kutoa matumaini kwa watu wote wa Taifa letu , na tunazo sababu za msingi za kwenda kushinda jimbo la Arumeru na ni wito wangu kwa kila kijana wa Arumeru anayeishi mjini kuona fursa hii ni kwa ajili ya ukombozi wa Nchi yetu na sio Arumeru peke yake na hivyo kwenda kutoa elimu vijijini tulikoacha wazee wetu.
Jana nilikuwa Meru , wazee na vijana wamekataa kuburuzwa na siasa za CCM ambazo kwa miaka hamsini ya uhuru wa Nchi hii zimeshindwa kutatua matatizo yao bali kufikiri rushwa ya pesa kipindi hiki cha Kampeni ndio mahitaji yao ya Msingi.
Nimesikia Tendwa msajili wa vyama vya siasa naye ameanza kusaidia CCM kufanya propaganda chafu labda ni vyema akatambua wajibu wake na sio kuanza kufanya kazi za siasa za CCM ni vyema akajua kuwa yeyote anayeitetea uovu leo itakuwa hasara kwake au kwa familia yake kesho .
Mwisho . Ninajua macho ya Watanzania yako Arumeru mashariki , Ninawatia moyo wale mlioko mbali lakini mnapenda mabadiliko , sisi tulioko huku tutapambana kwa niaba yenu kufa na kupona kuhakikisha haki, usawa, na demokrasia vinapata thamani halisi bila uhuni wowote kufanikiwa , Msiogope pengine huwezi kabisa kufika Arumeru kusaidia ukombozi basi wewe huko uliko tuombee kwa Mwenyezi Mungu , hakika hatutakubali uhuni ,udhalimu , na Nguvu ya rushwa iwachagulie ndugu zetu wa Arumeru Mbunge , kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa bado hazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja. Hata hivyo Msiogope Udhalimu utashidwa Arumeru ““ Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu .
Godbless J Lema (Mb)

Well said Mp!Tendwa ameshindwa kuelewa wajibu wake ameanza kukurupuka na kua ni sehemu ya kitengo cha propaganda cha c.c.m,i hate that old man,nina hakika mwalimu angekua hai angesikitika sana kwa jinsi chama chake na watu kama kina Tendwa wanajaribu kuwagawa watanzania kwa misingi ya ukabila na udini,hizo ni dalili za kufa na kutapatapa kwa chama tawala,eti mwenyekiti wao alisimama na kusifia kua kitengo cha propaganda ni muhimu katika chama,what a shame,dunia ya leo una sifu propaganda? "Mtu au watu wanaowabagua wenzao kwa misingi ya dini,kabila au rangi ni watu walioishiwa sera kichwani,ni wapumbavu,natumia neno zuri tu wapumbavu" - J.K.Nyerere
 
Kamanda lema kwanza nikupongeze kumsomesha mtoto wa binamu yangu wa sombetini,go go kamanda.GOD BLESS lema
 
Kwanza kamanda nikupongeze kumlipia ada mtoto wa binamu yangu wa sombetini,TUNAKUKUBALI MKUU.GOD BLESS lema
 
“PAMOJA NA SIASA CHAFU NA RUSHWA TUTASHINDA ARUMERU MASHARIKI”

Nawasalimu

Leo asubuhi nimesikia habari za uzushi na majungu kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi Uhuru pamoja na gazeti la serikali la Habari leo . Hivyo basi kilichosemwa na magezeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 23/2/2012 ni uzushi na propaganda , Magazeti haya ya CCM yatatumika sana kipindi hiki kama yalivyotumika kule Igunga yalipojaribu kutaka kuwatenganisha watu hata kwa dini zao lakini baadae ukweli ulijulikana na ikawa aibu kwao .
Kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Taifa letu kutoka kwa mkoloni bado Watanzania wa Arumeru sio huru na Watanzania wote kwa ujumla bado wanaishi maisha magumu kama wakimbizi nje ya Nchi yao.
Ninafahamu wajibu wangu katika kupigania demokrasia safi ya Nchi yangu na wakati huu jimbo la Arumeru Mashariki litakuwa mfano wa mapambano hayo na nitakuwa mstari wa mbele bila hofu wala kumuogopa mtu yeyote na wa cheo chochote katika kupigania ukweli na haki.
Wajibu wangu na wa chama changu kwa sasa ni kutoa matumaini kwa watu wote wa Taifa letu , na tunazo sababu za msingi za kwenda kushinda jimbo la Arumeru na ni wito wangu kwa kila kijana wa Arumeru anayeishi mjini kuona fursa hii ni kwa ajili ya ukombozi wa Nchi yetu na sio Arumeru peke yake na hivyo kwenda kutoa elimu vijijini tulikoacha wazee wetu.
Jana nilikuwa Meru , wazee na vijana wamekataa kuburuzwa na siasa za CCM ambazo kwa miaka hamsini ya uhuru wa Nchi hii zimeshindwa kutatua matatizo yao bali kufikiri rushwa ya pesa kipindi hiki cha Kampeni ndio mahitaji yao ya Msingi.
Nimesikia Tendwa msajili wa vyama vya siasa naye ameanza kusaidia CCM kufanya propaganda chafu labda ni vyema akatambua wajibu wake na sio kuanza kufanya kazi za siasa za CCM ni vyema akajua kuwa yeyote anayeitetea uovu leo itakuwa hasara kwake au kwa familia yake kesho .
Mwisho . Ninajua macho ya Watanzania yako Arumeru mashariki , Ninawatia moyo wale mlioko mbali lakini mnapenda mabadiliko , sisi tulioko huku tutapambana kwa niaba yenu kufa na kupona kuhakikisha haki, usawa, na demokrasia vinapata thamani halisi bila uhuni wowote kufanikiwa , Msiogope pengine huwezi kabisa kufika Arumeru kusaidia ukombozi basi wewe huko uliko tuombee kwa Mwenyezi Mungu , hakika hatutakubali uhuni ,udhalimu , na Nguvu ya rushwa iwachagulie ndugu zetu wa Arumeru Mbunge , kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa bado hazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja. Hata hivyo Msiogope Udhalimu utashidwa Arumeru ““ Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu .
Godbless J Lema (Mb)

Mkuu tunashukuru sana kwa maneno yako yaliojaa busara, Hakika tutashinda Arumeru, Mungu atatuongoza katika vita yetu dhidi ya udhalimu. Mungu Ibariki Chadema Mungu ibariki Tanzania.
 
Huyu kamanda napenda misimamo yake sana, taifa letu hapa lilipofika linaitaji viongozi jasiri aina ya Lema. c.c.m haitakiwi kuchekewa, coz hawa jamaa ni hatari zaidi ya Polonium 210. Godbless you Lema.
 
Labda huko hakuna wapiga kura Wamasai na Lowassa asiende. Lakini kama kuna wamasai, unajuwa Laibon wao nani? na akisema kitu huyo hapingwi.
Kwanza inaonekana wewe hujui vema Arusha joigrafia yake na wakazi wake. Arumeru hii inayogombaniwa hapa wakazi wake si wamasai, wakazi wa eneo hili wanaitwa Wameru, zamani walikuwa na historia ya vita na wamasai ingawa kwa sasa haipo tena. Ikiwa unahesabu kura kwa ukabila wa watu hapa umekosea mkuu wangu.
Tusubiri tuone nini kitatokea katika hili Jimbo
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru Washiri vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao  ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema, alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi, alisema.

Msajili alisema; ujambazi wa siasa hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
nao wanapaswa kuziepuka.

Hii sio habari,kwa mwandishi habari mwenye maadili na kuheshimu misingi ya kazi yake.Alipaswa ku-ballance story,na hivyo angemuuliza tendwa kama ifuatavyo.

*Mheshimiwa Tendwa,kulingana na uzito wa kauli hii,ni kwa nini umechukua hatua ya kuitoa katika vyombo vya habari,badala ya kuwaita viongozi wa chadema na kufanya nao kikao kuhusiana na hili na pia ukapata maoni yao?
*Je kwa hatua hii ya kuja kutoa taarifa hii kwenye vyombo vya habari,huoni kwamba unaingilia na kuvuruga mchakato mzima wa uchaguzi jimboni humo.ukizingatia nafasi yako kama msajili wa vyama vya siasa. Nchini?
*Je unakubnali kuwajibika kwa madhara yoyote yatakayojitokeza kutokana na kauli hii,kwa wewe kutokuchukua hatua zozote kulikemea,badala ya hivi ufanyavyo.ikizingatiwa kuwa wewe ni mlezi wa vyama vyote,kwa nafasi uliyonayo.

Baada ya hapo ndio ingekuwa habari rasmi,sasa naanza kupata picha kwa nini Mkapa alikuwa anakataa kuongea na wandishi wea kibongo bongo kwa kuwaita makanjanja.
 
Kamanda nakuunga mkono Tendwa na CCM ni sawa na chanda na pete CHADEMA lazima tusimame pamoja hata wakiahamishia jeshi hapo hawataweza lazima tushinde tu komaa kamanda
 
Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu

Tungepata watu kama mia hivi wanaohamini maneno haya ya Kamanda Lema nchi ingekuwa imenyooka muda mrefu sana.Mimi natafuta nafasi hapa ofisini,nitakuwa na wapambanaji hata kwa siku moja kule Arumeru Mashariki,naamini kwa hakika wakati huu haki itashinda dhidi ya hujuma,udhalimu,ubadhirifu,uuaji,ufirauni,ushenzi,ujambazi,upumbavu,ujinga,ulaghai,ushetani,ujoka,uhafidhina nk ya CCM...

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Arumeru Mashariki ,Mungu Ibariki CHADEMA,
 
Mkuu, si ungemtumia-PM tu inatosha.

alivyofanya ndiyo sahihi, mibunge ya ccm inajidai kusomesha wanafunzi kibao lakini hatujapata ushuhuda clean kama huu, amewasiliana hadharani na mbunge wake aliyemchagua.
 
Nilisema jana hapa JF tena kwa unyenyekevu mkubwa kwamba kusimama mbele ya hadhira kuinadi CCM kwa nyakati hizi ni shughuli pevu...basi kuna mdau hapa alinishambulia eti mie muongo na alishanipotezea...japo alinishangaza...kanipotezea wakati huohuo kakomenti post yangu...!!!Ukweli CCM kwa sasa haina mbinu zaidi ya rushwa na vyombo vya dola...na ndiyo maana unamuona pale Mwigulu anatambia pesa.
 
Haya mambo ya "kaombe radhi" ni mbinu za CCM. Nadhani nyote mnakumbuka kule Igunga walivosema Chadema waombe radhi kwa kudhalilisha hijabu, naona wameshaanza tena Lema aombe radhi wameru!
 
Back
Top Bottom