chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,663
Kuna jambo linatia tafakari kidogo, CCM pamoja na awamu ya sita, kwa kweli wamefanya mengi sana ya kimaendeleo. Ili kuitendea haki CCM na uongozi wa serikali, lazima yasemwe mikutanoni.
Hii ya kutembea na kuaminisha watu kwamba hakuna lililofanyika nadhani si sahihi. Unaita mtumishi mmoja, ana ka suala kamoja tu ka kiutendaji, unakashikia bango hako, husemi chochote kuhusu mengine mazuri yaliyofanywa na CCM eneo hilo. Mfano, Kagera, kuna miradi mipya lukuki imepelekwa na Samia, yakaangaliwa mabaya tu tena kwa lengo la kujitafutia umaarufu binafsi, hakuongelea meli mpya ukarabati mkubwa wa bandari, na kadhalika, ukiangalia, hii ni kwa mikoa yote anafanya hivyo.
Hata JPM, alijikita kwanza kuonyesha mafanikio ya CCM japo yamepatikana katika hali ya uchumi mgumu. Na kisha akasemea mapungufu, kwa nini huyu amejikita kwenye upande wa kuonyesha kwamba awamu ya sita haijafanya kitu kwamba kila sehemu ni shida tu?
Maana uongo ukirudiwa, unakuwa ukweli, sasa ukiwa ukweli wananchi tutawaambia nini 2025? Maana kiongozi wa CCM wa uenezi anasema serikali iko hovyo, na wapinzani wanasema iko hovyo, tunadhani wananchi wataamuaje? Hatukatai CCM kuyatambua mapungufu na kuyafanyia kazi, lakini mbona tunaweka nguvu kubwa kufanya mafanikio yaonekane kama hakuna?
Kuna mtu anajua kwamba wale wanaohamishwa bonde la msimbazi mama Samia, sio Benki ya Dunia, mama Samia kupitia ikulu katoa amri kila mmoja apewe milioni nne akanunue kiwanja kigamboni au chanika, hiyo ni mbali na fidia anayolipwa? Sawa, shida zipo, mbona mazuri huyasemi?
Tutumie asilimia 75 ya muda kuwaeleza wananchi nini tumefanya, tuwaeleze mapungufu, na na wao watueleze mapungufu, tuone namna ya kuyafanyia kazi.
Kwa hali ilivyo, sidhani kama kuna strategy ya mawasiliano ndani ya chama. Mwenenzi anasema akimaliza ziara anapeleka taarifa kwa Rais! Kwa nini isiwe kwa Katibu Mkuu, ambaye ndio immediate boss?
Ziara nzima hakuna anayeambiwa kuhusu SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, shule nzuri hazitembelewi, anatembelea makaburi tu, wengine wanasema anatembelea makaburi kwa sababu za kishirikina tu, sijui kuchota mchanga apeleke kwa wataalamu ili wamchanganyie mavumba awe mkubwa kama hao viongozi, kwa nini hakuna sauti kubwa kwa miradi kama Kigongo Busisi, Lami,.miradi ya maji na kadhalika.
Hatumuoni anatembelea miradi ya mfano kwa kila wilaya au Halmashauri, iko mingi sana, ya kila aina, tena ya kisasa, ila yeye anatafuta sehemu za chokochoko tu dhidi ya serikali iliyo madarakani, na kudhoofisha imani ya wananchi kwa serikali. Sawa, atafute za chokochoko, lakini mbona nzuri hazisemi wala kuziona?
Chama kinatakiwa kuwa juu ya mtu, lakini naona mtu anataka kuwa juu ya chama.
Hii inaweka taswira kwamba, kwa mlango wa nyuma, anambomoa Samia kisiasa kwamba hajafanya kitu chochote, wakati wenzake ndani ya CCM wametumia muda mwingi kuonyesha Samia kafanya makubwa nchini.