Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kila jambo kwenye maisha lina sheria zake, zidharau kwa gharama zako mwenyewe!
Najua kuna huu mjadala umekuwa unaendelea wa watu wanaoenda kuunga mkono juhudi kwamba wananunuliwa na wengine wamekuwa wanasema CCM wanaiba kura na kushinda kwa hila ila ngoja nikuelezee vitu viwili vitatu vitakusaidia kwenye uchambuzi wako wa siasa za Tanzania.
Baadhi yetu humu hatukuzaliwa jana. Tumeona Tanzania hii katika hali tofauti tofauti, matatizo yakija, yakikaa na baada ya muda (ambao wakati mwingine ni miaka mingi) matatizo hayo yanapatiwa ufumbuzi. Nikupe mfano mmoja. Wangapi wanakumbuka kipindi kile mabasi yalikuwa yana vile vibao vidogo wanaweka kwa ndani kuonyesha linakwenda wapi? Madereva wakawa wakijisikia muda wowote katika siku wanabadilisha ruti kwenda sehemu nyingine yenye abiria hali iliyokuwa inawapa usumbufu mkubwa abiria. Ilichukua muda mrefu mpaka ufumbuzi ukapatikana ambao ulikuwa ni kuyapaka mabasi yote rangi maalumu. Ninachotaka kusema wakati ule tatizo lilipokuwepo, kelele zilikuwa nyingi, ushauri ulikuwa unatolewa kila siku lakini ilichukua muda mrefu sana uamuzi kuchukuliwa ila sikumbuki kama iliwahi kuwa ajenda ya mwanasiasa yeyote wa upinzani!
Nimetoa mfano huo mdogo kusema tu kwamba kwenye suala la changamoto mbalimbali za kijamii na maendeleo, CCM inazitatua ila siyo kwa kasi ambayo wengi tungependa. Wangapi mnakumbuka kero za Muhimbili? Wengi mnaweza msitambue lakini Tanzania tumefanya mapinduzi kwenye sekta ya afya ingawa changamoto bado ni nyingi ila tumetoka mbali sana. Wamarekani wana msemo 'taking your sweet a$$ time', kwa maana ya kufanya vitu taratibu mnooo. CCM na serikali zake inachukua muda mrefu sana kutatua kero za watu ila ukweli ni kuwa, kwa wakati wanaoamua wao wanakujaga kuzitatua. Kuna kiongozi wa CCM sikumbuki ni nani alisikika hivi karibuni akisema CCM inaamua kama sehemu fulani ipate maendeleo au hapana, kwa bahati mbaya sana huo ni ukweli mtupu.
Tatizo kubwa la ndugu zangu wapinzani ni kuendelea kudhani ajenda kubwakubwa mfano shutuma kubwa za rushwa zinaweza kuwasaidia. Mimi nadhani hilo linaweza kufanikiwa kwa kiasi fulani kidogo sana ila haliwezi kuwapeleka Magogoni. Kuna mwanasiasa mmoja wa Marekani Tip O'Neal aliwahi kusema 'All politics is local', ni msemo na filosofia ambayo imekuja kukubalika kama ukweli usiopingika. Msemo huo una maana kama unataka ushinde katika uchaguzi wowote, siasa zenye mantiki na maana kwa mpiga kura mmoja mmoja ni zile zinazohusu mambo yanayomuhusu moja kwa moja kwa maisha yake ya kila siku. Kero zile ambazo zinamsumbua kila siku ndiyo zinaamua kura yake anampa nani. Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti, wanasiasa makini wanaiangalia philosophy hiyo na kuiweka ifit katika mazingira na nyakati za wakati huo. Moja ya kauli mbiu za kampeni ya Bill Clinton mwaka 1992 ulikuwa msemo mmoja ambao na wenyewe umekuwa kama 'ukweli usiopingika' ni msemo unaosema 'It's the economy, stupid' ukiwa na maana ni uchumi ndiyo unaomatter kwa mpiga kura, mengine yote ni mbwembwe tu! Yote hii inarudi kule kule, all politics is local!
Nasema haya kusisitiza tu kwamba skendo sijui Bombadia, sijui mambo ya Makonda, sijui ndege gani sujui, mpiga kura wa kawaida kwa maoni yake hizo issues hazimuathiri moja kwa moja katika maisha yake ya kila siku ya kujitafutia mkate, nawaambia ukweli. Na huyo mpiga kura anaweza akawa sahihi au asiwe sahihi, hilo siyo ninalotaka kuzungumzia hapa, siku moja nilimsikia Halima Mdee akijaribu kuelimisha kuhusu jinsi gani issue hizo zina athari kwa mpiga kura moja kwa moja, ila ni kupoteza muda tu, kuna ukweli usiopingika nimeutaja hapo juu. Augustine Mrema alikuwa na style ya 'kulipua mabomu', ilimfikisha wapi?
Mimi nadhani CCM wameamua tu kucheza siasa za rafu na kibabe ila naamini wana uwezo wa kushinda chaguzi bila watu kutolewa ngeu na makandokando mengine yasiyoeleweka. Ushauri kwa wapinzani, siasa za kupigia kelele issue za kitaifa zinauza magazeti sana ila haziwezi kuwapeleka Ikulu.
CCM itaangushwa na gravity, kanuni nyingine ya maisha isiyopingika!
NYONGEZA: Naona niseme natambua kuna wanasiasa wengi tu wa upinzani, hasa ngazi za chini wamefuata kanuni za siasa nilizozitaka hapo juu kwa ufanisi mkubwa. Inapokuja sasa wakati wa kupigania kushika dola, kuna sehemu wanakwama au wanajisahau na kwa mtazamo wangu sababu kubwa ni hii.