Pamoja na Bodi kumpendekeza, Dk Rashid aweka sharti la kurudi TANESCO!

Mbali ya Peter Ngumbulu hivi hii bodi ya Tanesco wajumbe wengine ni akina nani?............mwenye kujua please anisaidie kunipa majina yao hapa bodini JF

Wamo pia:

Semindu Pawa - Deputy Chairman
Beatus Segeja - huyu ni kutoka CRDB
 
Dont tell me hatuna watu wa kuongoza Tanesco isipokuwa Dr Rashid tu!
..Kama mkulu kamtaka nani wa kumpinga?
Sums up all..nchi ya wapumbavu..PERIOD
No sisi ni wapole mno na tutaendeleza upole huu mpaka wang'oke kwa hiyari yao
Sijui nani 'katuroga'! Hivi kweli hakuna mwingine zaidi ya Dr Rashid? Mambo mengine hayaingii akilini kabisa!
Aliyeturoga ni CCM ya azimio la zanzibar. Kwa kweli tumetukanwa na kupuuzwa vya kutosha. Naamni hata kukurupuka ktk maamuzi ni kufanya maamuzi magumu pia.
 
Tatizo Tanesco imejaa ukiritimba na kuingiliwa na siasa. Tanesco ina matatizo makubwa mengi ila ya msingi ni ifuatayo;

  • Uzalishaji wa umeme huatoshi kulingana na mahitaji ni lazima tuongeze vyanzo vya umeme, period. Hii inahitaji uwekezaji kwenye ufuaji wa umeme ama kujenga mabwawa mapya ama kununua mitambo mipya ya gesi maana hizi ndio vyanzo nafuu sio mitambo ya mafuta mazito e.g. Richmond turbine.
  • Tanesco inabidi igawanye kwenye makundi matatu yaani ufuaji umeme(power generation), usambazaji (transmission) na uuzaji (retail). Hii ndio inayotumika kwenye nchi nyingi na italeta ufanisi na kuona kwa urahisi wapi kwenye udhaifu.
  • Kuachwa kufanya mambo yake bila kuingiliwa na wanasiasa. Maana hivi sasa kila mtu ni mtaalamu kuhusu hili kampuni kuanzia waziri hadi kina Zitto (POAC) kila mmoja ana hoja zake na namna ya kuinusuru bila mafanikio.
  • Tuangalia kwa kina na kuwezesha kwa uwazi jinsi ya kutumia vyanzo mbadala vya umeme kama makaa ya mawe, uranium, vyanzo vya jua na upepo. serikali iwape tija wawekezaji wa ndani na nje katika hii sekta ila kuongeza tija na uzalishaji. Nchi nyingi hivi sasa zinawahimiza watu wao kuzalisha umeme binafsi yaani ama kwa kutumia jua au upepo na kupunguza matumizi ya gridi zao za taifa na utegemezi wa mafuta au gesi toka nje ya nchi zao. Hii ufanya kwa kupunguza kodi katika uzalishaji wa sola panel au ununuzi wake nasi tuige mfano huo.
  • Idrisa Rashid ana kashfa ambazo bado hajajibu kwa ufanisi kwenye dili ya rada na mambo ya richmond hivo ni bora atafutwe mtu mwingine kuongoza hii taasisi muhimu ya umma.
 
Dr yeye hana tabuu kwani kazii hiyoo wameamuaa kumlazimishiaa aifanye yeye kwani ndo kwao mwenye kulinda masilahi yao na at least shirika likajikongoja kwa sasa.
 
haa labda na yeye aliondoka na wafadhili watu akirudi tutaanza kupata misaada
 
Watu hawa wafuatao ni kundi la hatari sana sana katika nchi ya Tanzania...
1. Jakaya Kikwete
2. Edward Lowassa mamvi
3. Rostam Aziz
4. Idris Rashidi wa Tanesco
5. Dau wa NSSF
6. Chenge (mwizi wa rada)
7. Sofia Simba
8. Yusuph Makamba
9. Zitto Kabwe
10.
11.
 
Haya ni matusi makubwa sana kwa wasomi wengine wa kitanzania. Hivi kweli bila Idris Rashid kuwepo Tanesco hilo shirika litakufa??!! Jamani wakati mwingine wawe wanajua kuchagua aina ya matusi, haya si mazuri kabisa. Tuna vichwa kibao vya kuweza kuendesha hata nchi ije kuwa Tanesco.

mkuu tupo ukurasa mmoja
kama ni hivyo ni bora wambinfsishie ili liwe lake yeye na familia yake
 
cha ajabu nini?.Si juzi tu hapa waliletwa Net group solution, wafanye Management!!!!!.tena waliingizwa ofisin kwa mtutu wa bunduki!!!!.Watz bado sana.
 
Watu hawa wafuatao ni kundi la hatari sana sana katika nchi ya Tanzania...
1. Jakaya Kikwete
2. Edward Lowassa mamvi
3. Rostam Aziz
4. Idris Rashidi wa Tanesco
5. Dau wa NSSF
6. Chenge (mwizi wa rada)
7. Sofia Simba
8. Yusuph Makamba
9. Zitto Kabwe
10. apson-mkuu wa usalama wa zmani
11. subash patel na wenzake
11.
sawa kabisa, mtu hatari namba moja ni jakaya kikwete huyu ndo mwizi namba moja wa pesa za epa, wale wafanyakazi wa benki kuu waliotolewa mbuzi wa kafara wanasali usiku na mchana na very soon, Mungu ambaye hahongwi atamuumbua kikwete na maharamia wenzake, katika hiyo list umesahau genge la mafia linaloshirikiana na kikwete ambao ni akina apson, subash patel, hawa wote ni majambazi. ni bahati mbaya kuwa nchi inaongozwa na genge la mafia
 
Nafikiri tuangalie huko kote alikopita ameachangia mazuri yapi? Kama anatetea kununua mitambo iliyotumika kinyume na sheria ya serikali ya manunuzi, atakuwa na matatizo kwa maana sheria ikimsogelea atasema ilikuwa mipya! Kwanza ule mtambo wa songas pale Ubungo ulitakiwa ujenge kule Kinyerezi lakini ufisadi ukafanya ujengwe pale Ubungo kwenye watu wengi kinyume na mambo ya mazingira, yeye alikuwa wapi? Halafu hayo masharti anampa nani? Au anamwambia nani ambaye ananguvu kimadaraka kwa wanasiasa kuwa wasimfuatilie? Kikwete? Kama anafanya madudu kwa nini kamati ya bunge isiiingilie? Huyu anawaambia watu wake kuwa nikirudi tachonga 'deal' ili wapate zaidi ya bil. 50 lakini ya radar yasitokee tena hapa!! Kwanza huyu ni mfanya biashara na atuambie hiyo kitu yake inaitwa Tanzania Mtaji Fund (TMF) ni nini? Na inafanya nini? Na hiyo mitaji ni ya nini? Na anaitoa wapi? Na kwa ajili ya akina nani?
 
Tanesco na TRL ndio vinasikika sana lakini ndugu wana jamii Tangu management ya Ki-canada kuondoka
ndani ya TTCL mpaka leo bado inaongozwa na Kaimu CEO.Hali inazidi kuwa mbaya na kampuni inazidi
kutafunwa na wajanja.Nafasi zote nne za juu zikatangazwa na watu wakafanya interview na majibu
yakatoka wengi wakaonekana hawafai na sasa nafasi ya chief sales and markerting
imetangazwa tena kwa kuonekana kuwa wote waliofanya interview kwa nafasi hiyo inaonekana hawafai na
ipo siku inakuja ambapo tutaambiwa kuwa wa-canada wanatakiwa kurudi na wao watatoa masharti kuwa
kitu fulani hawataki.
 
Personally I have nothing against Dr. Rashid kurudi TANESCO. Kama mchakato mzima ulizingatia vigezo vya utendaji bora. Maana kama waliapply watu wengi na jopo likaona kwamba Rashid ndo anastahili nadhani si vyema kulalamika. Unless tunajua ni akina nani waliomba hii nafasi na walikuwa na vigezo vipi. Sema tatizo kubwa nililonalo mimi ni kwamba, TANZANIA tunaendesha mambo kienyeji. WE DONT HAVE TANSPARENCY. Kama serikali ingekuwa transparent sioni haya malalamiko yangetoka wapi. Maana wengi wenye interests wangefuatilia na kujua ni kwa nini huyu kapendekezwa na si mwingine. To, me this is the biggest challenge facing banana republics kama zetu. Hatuko wawazi katika utendaji wetu. Laiti tungelijua, umuhimu wa uwazi, hakika tungepunguza minong`ono mingi na kuboresha utendaji wa shughuli zetu za kila siku.

And why should we involve the President anyway, kama kamati ya wataalamu imeshaona kwamba fulani anafaa? kama alivyosema jamaa hapo juu. Kuongoza nchi especially kama zetu masikini..ni nightmare.
 
It always take time for we to make good atempt lets wait for that very time . May be
 
Back
Top Bottom