Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 575
- 2,560
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima ametahadharisha unafiki wa kisiasa unaoendelea miongoni mwa Watanzania kwa sasa kwa kupenda kusifia kila jambo kuwa utaliua taifa.
Amesema tabia hiyo inaendelea kupata mashiko nchini kutokana na upeo mdogo wa watu kushindwa kujua misingi ya haki za binadamu na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele .
Akizungumza leo Dar es Salaam, Septemba 30, 2022 katika kongamano la viongozi wa dini zote linaloangazia haki za binadamu nchini, kiongozi huyo amesema tabia hiyo iliyojengeka isipokomeshwa ni wazi mahusiano mazuri miongoni mwa Watanzania yanaenda kupotea.
"Unafiki unaharibu nchi, unafiki wa kisiasa uliopo miongoni mwa Watanzania kupenda kusifia viongozi ili tu kujipendekeza wapate vyeo unaenda kuliua Taifa na tatizo hili linaendelea kwa sababu watu hawajui misingi ya haki za binadamu," amesema Padri Kitima
Kiongozi huyo wa kiroho amesema hata kujitoa kwenye mahakama ya haki iliyopo Arusha na kuwahamisha wananchi kutoka Loliondo kwenda Handeni mkoani Tanga ni uvunjivu wa haki za binadamu.
"Kwa sababu nchi imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki za binadamu," amesema
Amesema wao kama viongozi wa dini baada ya kuona tabia hiyo hususan miaka mitano iliyopita, mwaka 2020 walianza kuandika kitabu Cha elimu ya haki za binadamu kwa lengo la kuanza kutoka elimu watu wote.
"Haki za binadamu haziombwi, zinapiganiwa, dini ni kiungo muhimu na tumeona tufanye hivi na tunatarajia kuwafikia viongozi 16,000 nchi nzima na kushuka kwa Watanzania wote," amesema
Chanzo: Mwananchi