..mwandishi anaelezea aliyoyaona na kuyasikia Chato, jimboni kwa waziri Magufuli.
..ni tuhuma nzito za upendeleo,ukabila, na rushwa.
..ninapata wasiwasi kwamba ukiamua kumchunguza kwa umakini Pombe Magufuli unaweza ku-conclude kwamba ni "mchanyato" wa kiula,msuya, na mramba.
..wengine wanafikiri anafaa kuwa Waziri Mkuu au hata Raisi.
..ni tuhuma nzito za upendeleo,ukabila, na rushwa.
..ninapata wasiwasi kwamba ukiamua kumchunguza kwa umakini Pombe Magufuli unaweza ku-conclude kwamba ni "mchanyato" wa kiula,msuya, na mramba.
..wengine wanafikiri anafaa kuwa Waziri Mkuu au hata Raisi.
raia mwema said:Wakati ninarejea Dar es Salaam, kutoka Kagera, nilisimama Chato, Lunzewe, Isaka, Igunga, Singida, Dodoma, Morogoro. Sehemu zote hizi nimeshuhudia mikutano ya wagombea wa CCM, wakijinadi kwa wanachama ili kupigiwa kura ya maoni. Sehemu zote hizi kulikuwa na dalili za nguvu ya fedha.
Baadhi ya wagombea wamenunua simu za mkononi na kusambaza majimboni kwao. Kwingine pikipiki zimesambazwa. Kule Chato mgombea mmoja alikuwa akiwaelezea wanachama wa CCM, kwamba kwa vile analipenda sana jimbo alihakikisha barabara ya Bwanga-Kyamyorwa inapinda kupitia Chato, badala ya ramani yake ya kupitia Biharamulo mjini. Na kwamba ametumia kila uwezo wake kuhakikisha Mji wa Chato unakuwa na huduma muhimu na majengo ya kisasa kiasi una sifa zote za kuwa makao makuu ya Mkoa wa Geita.
Majigambo mengine ya mheshimiwa huyo ni kwamba amefanikiwa kuleta Mkoa mpya wa Geita na kuhakikisha Chato, inatengwa kutoka Mkoa wa Kagera.
Kwa wengi hili halikuwa jambo jipya maana siku zote mheshimiwa huyu hakukubali kuwa Chato ni sehemu ya Mkoa wa Kagera. Hakuna uhakika wa asilimia 100 kuonyesha kuwa watu wengi wa Chato, walitamani kutengwa kutoka Mkoa wa Kagera. Hivyo hili la kuimega Chato kwenda Mkoa wa Geita linaweza kumjenga au kumbomoa.
Kuipindisha barabara ni aina fulani ya rushwa. Ingawa barabara hii imechangia kiasi kikubwa kwa maendeleo ya Chato na Kimwani, imekwamisha maendeleo ya maeneo mengine kama vile Buziku, Lukola na Biharamulo mjini. Hata hivyo, barabara hii imejengwa kisiasa. Imeharibika mapema. Ukipita kwenye barabara hii huwezi kuamini kama ni mpya. Na kusema kweli kama mkadarasi aliyeijenga barabara hii amelipwa na kuondoka, atakuwa ametenda dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na kama kuna Mtanzania aliyemsaidia mkandarasi huyu kuhujumu Taifa letu, basi Mtanzania huyu ni bora apate zawadi ya kwenda jela si chini ya miaka mitano. Nchi nyingine kama China, mtu kama huyu anapigwa risasi na kutoweka kwenye uso wa dunia.
Na hili ndilo tatizo la mambo yote yanayofanyika kwa mtindo huu wa rushwa na hongo. Wagombea wakipitishwa kwa rushwa na hongo, wakifika madarakani wanajifanyia mambo yao. Hawana muda wa kuwakumbuka wapiga kura wao, maana walimalizana wakati wa uchaguzi. Mtu anayehonga ili apate ukandarasi wa kujenga barabara, akishafanikiwa anajenga ovyo ovyo maana amekwisha malizana na wahusika.
Mfano mzuri ni Barabara ya Bwanga-Kyamyorwa. Kama barabara hii ilikaguliwa na wahandisi wetu na kupitishwa, ina maana walihongwa, au wakandarasi waliojenga walitoa hongo ili kupata kazi hiyo. Hivyo walijenga kwa kiwango cha chini na kujiondokea. Kufuatana na barabara hii ilivyoharibika mtu hahitaji shahada ya uhandisi kutambua kwamba kazi ilifanywa chini viwango.
Hoja ninayoijenga hapa ni kwamba bila kutafuta dawa ya ugonjwa huu wa rushwa na hongo, tutaendelea kutawaliwa na watawala waliochaguliwa kwa rushwa na hongo na hawa kwa vyovyote vile hawawezi kuwa na mapenzi na maendeleo ya wananchi wote zaidi ya kupenda maendeleo yao binafsi na kuendelea kutafuta fedha ili washinde chaguzi nyingine na wakae madarakani milele.
Tunahitaji mfumo utakao tuwezesha kuwachagua viongozi wetu kwa kufuata sifa, uwezo wa kiakili na kutenda kazi, uzalendo, uadilifu na sifa nyinginezo za kiongozi makini.