BONGOLALA
JF-Expert Member
- Sep 14, 2009
- 16,507
- 11,883
Imeandikwa na Nakajumo James, Moshi; Tarehe: 4th November 2010
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Padri Stanslaus Sala wa Kanisa Katoliki jimbo la Moshi, Parokia ya Mtakatifu Theresa Lego Muro kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 14 kwa ahadi ya kumpa rosari na mche wa sabuni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Lucas Ng'hoboko, alisema jana kwamba, Padri huyo mkazi wa kata ya Kilema Kusini, Moshi Vijijini, inadaiwa alifanya tendo hilo Oktoba 30, saa 2 usiku.
Alisema, kiongozi huyo wa dini, alimtendea hayo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye alikuwa mfanyakazi wa kuhudumia mifugo katika Parokia hiyo, baada ya kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.
Kamanda Ng'hoboko alisema, Polisi ilipokea taarifa za tukio hilo Oktoba 31 katika kituo kikuu cha Polisi Moshi na mtoto huyo kupewa hati maalumu ya matibabu (PF3).
Alisema, mtoto huyo alifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na kwamba mtuhumiwa ametoroka.
"Tangu tumepata taarifa za tukio hili la kikatili, askari wangu wamekuwa wakifanya msako dhidi ya Padri huyo ili akikamatwa sheria iweze kufuata mkondo wake," alisema.
Kwa upande wake, akizungumzia tukio hilo, baba wa mtoto huyo, Amati Lyamuya, alisema kitendo hicho ni cha kikatili na kimeidhalilisha familia yake.
Mtoto huyo alidai kwamba, Padri alimchukua na kudai kuna makosa ameyafanya na kwamba alistahili adhabu ingawa hakumweleza aina ya kosa, lakini hakukataa akiamini hana kosa.
Alidai kuwa waliondoka na Padri na kuelekea seminari ya Karumali walipofika Kisanja msituni, Padri alimwamuru ashuke kwenye gari na kumlaza mlango wa mbele na kumwingilia kimwili.
"Tukiwa njiani kuelekea eneo hilo aliniambia kuwa baba yangu ameagiza nipewe adhabu … tulipofika kwenye ule msitu, alinivua nguo na kuniingilia, nilipiga kelele bila mafanikio na tuliporudi Parokiani, alinipa rozari na sabuni ili nisiseme," alidai mtoto huyo.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kilema Kusini, Adamu Mbuya, naye alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
source: www.habarileo.co.tz