Tuwashangae wote wanaosema 'madudu yanagunduliwa'. Yanagunduliwa vipi haya kwa sasa wakati yakitendeka watu walipigia kelele wizi huo wa wazi; lakini masikio yao yalizibwa na waliopiga kelele waliitwa wapinzani. Sasa wao wamegeuka na 'kuyaona' hayo madudu na wale walioyasema huko nyuma wanaitwa wachochezi na siyo wazalendo. What a crooked world.Vitu vingine ni aibu hata kuvisema. Jamani hivi Watanzania Elimu yetu inatufaa kweli? Uwozo unaozidi kugunduliwa ni aibu kubwa kwa taifa. Mambo haya yote maovu yakitendeka maprofessor walikuwa wapi? Rais alikuwa wapi? Vyombo vya sheria vilikuwa wapi? Siwezi kuuliza Watanzania walikuwa wapi, Kwani tulikuwa tumewekwa gizani. Wizi uliokuwepo Tanzania MUNGU tu anayejuwa. Nashangaa cabinet ya Kikwete wote wako huru. Tanzania ni nchi mojawapo muhindi anakuja na briefcase tupu anaondoka billionea akisaidiwa na Viongozi wetu Wakati Watanzania wasota na maisha magumu. MARAIS waliopita wasikaze kisabuni mumewatesa Watanzania kwa vitendo vyenu, kazi ya urais mlikuwa hamuiwezi