Orodha ya watumishi waliopata vibali vya uhamisho wa kubadilishana vituo vya kazi kuanzia Novemba 2021 – Januari 2022

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,128
2,337
ORODHA YA WATUMISHI WALIOPATA VIBALI VYA UHAMISHO WA KUBADILISHANA VITUO VYA KAZI KUANZIA NOVEMBA,2021 – JANUARI,2022 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI

Prof.Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa watumishi 1544 wa kubadilishana vituo vya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za MItaa.

Prof.Shemdoe amesema kuwa Ofisi ya Rais –TAMISEMI inaendelea kufanyia kazi uhamisho wa kubadilishana tu kwa sasa na kwa wale walioomba uhamisho usiokuwa wa kubadilishana kuanzia Julai,2021 – Januari,2022 kwenda Halmashauri za Wilaya waendelee kusubiri wakati tathmini kwenye halmashauri zote ikiendelea kufanyika ili kufanya msawazo.

Pia, amewataka watumishi wote wa Mamlaka za Serikali za MItaa waliowasilisha maombi yao ya uhamisho OR-TAMISEMI kwa kipindi cha Januari 2018 – Juni,2021 kuomba upya kuhamia kwenye maeneo hayo ila isiwe kwenye Majiji,Manispaa na Halmashauri za Miji.

Maombi hayo ya uhamisho yazingatie taratibu zote za uhamisho kama ilivyoainishwa kwenye Waraka wa Uhamisho No.2 wa mwaka 2018.

Aidha, amewataka watumishi waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kuja Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo na kuwa orodha ya majina ya watumishi waliopata vibali vya uhamisho inapatikana kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

Endapo mtumishi atakua na changamoto yeyote asisite kupiga simu kwenye Kituo cha huduma kwa mteja kwa namba za simu: +255735-160210, +255262-160210 ama kuandika barua pepe kwenye anwani yetu ya huduma@tamisemi.go.tz

Imetolewa na Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
30.01.2022


👇👇👇👇👇👇
 

Attachments

  • Orodha ya watumishi waliopata vibali vya Uhamisho wa kubadilishana vituo vya kazi, Nov 2021 – ...pdf
    637.6 KB · Views: 137
Tamisemi mungu anawaona, mnatoa vijina vichache huku majina mengi mmeyatupa makabatini.
Mnatoa majina machache kumdanganya SSH ila ukweli ni kwamba TAMISEMI ni jipu mnatakiwa mtumbuliwe.
 
Hivi bila kubadirishana na mtu, hamna namna nyingine ya kuhama.
 
ORODHA YA WATUMISHI WALIOPATA VIBALI VYA UHAMISHO WA
KUBADILISHANA VITUO VYA KAZI KUANZIA NOVEMBA,2021 – JANUARI,2022

👇👇👇👇👇👇
Naona zaidi ya 95% ya Wanaohama ni Waalimu. Kila la heri waliopata nafasi za kuhama
 
Kuna MWANANGA mmoja tangu 2012 anatafutaga uhamisho ni MWALIMU sijui alipataga ngoja nimtumie hii ajitafute
 
Kwahiyo kama huna wa kubadilishana naye imekula kwako..huu ni upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi Mwl. wa Sekondari Manispaa ya Morogoro natafuta mtu wa kubadilishana nae kituo cha kazi yeye aje Morogoro na mimi niende Dar es Salaam wilaya ya Ubungo au Kinondoni kwa mawasiliano 0765101554 na 0717101055
 
Mimi Mwl. wa Sekondari Manispaa ya Morogoro natafuta mtu wa kubadilishana nae kituo cha kazi yeye aje Morogoro na mimi niende Dar es Salaam wilaya ya Ubungo au Kinondoni kwa mawasiliano 0765101554 na 0717101055
Mjini patamu, pambana unaweza kupata wa kubadilishana naye
 
Mimi Mwl. wa Sekondari Manispaa ya Morogoro natafuta mtu wa kubadilishana nae kituo cha kazi yeye aje Morogoro na mimi niende Dar es Salaam wilaya ya Ubungo au Kinondoni kwa mawasiliano 0765101554 na 0717101055
Kwa hili nikupe pole..kila mtu ana taka kuja mjini na wa mjini hawataki kuondoka...ila endelea kua na imani ipo siku myb utafanikishaila chances ni dogo sana.
 
Natafta mwalimu wa kubadilishana nae mimi nije Kanda ya ziwa mikoa ya geita ,mwanza na shinyanga yeye aje mkoa wa katavi
 
Back
Top Bottom