Rostam hana sababu ya kubatuzana na serikali bungeni maana kaishika na anuwezo wa kuambia nje ya bunge nataka kitu hiki kiwe hivi na kinakuwa.Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.
Niliwahi kusema kuhusu RA na Bungeni, sio tuu hajawahi kuchangia, bali kipindi anachohudhuria kikao cha Bunge, akikaa sana ni siku 3 tuu. Sijawahi kumuona zaidi ya siku 3 mfululizo. Yeye na mkono, huja Dodoma na ndege zao. ya Mkono huridi Dar kusubiri kuja kumchukua. Ya RA humsubiri hapo Airport ya Dodoma.
RA haulizi swali lolote kwa sababu matatizo yote ya wananchi wake anayamaliza mwenywe kwa fedha yake ya mfukoni.
Pia hachangii hoja yoyote kwa vile kichwani hamna kitu, hata ukimuona kwa macho tuu usoni, hilo utaliona wazi.
Kuna baadhi ya wabunge hawachangii lolote kwa sababu wamesusa baada ya kukatiwa ulaji. Ila pia kuna wasio changia kwa sababu hawaoni umuhimu wowote kuchangia japo vichwani wako fiti, lakini kuna hawa wasiochangia kwa vile vichwani hawana kitu, japo pesa wanazo.
Hivi kweli wananchi wakielimishwa kuhusu majukumu ya mwakilishi wao Bungeni, bado watawachagua mabubu?.
huu mchakato wa kitoto sana wabunge wote wataongea ili waonekana wameongea tu basi.hata jf kuna watu wengi tu hawachangii, je nao ni bubu?
Kimsingi mbunge kuwa bubu completely bungeni si jambo jema. Zaidi ya interests za jimbo lake pia mbunge anawajibu kutetea interests za taifa. Yapo mambo chungu nzima ya kitaifa ambayo hujadiliwa bungeni, mbunge mzalendo hataacha kutoa mchango wake ati kwa sababu jimboni kwake mambo mazuri.
Swala la Rostam kutokuchangia lolote liko wazi kabisa. Rostam si mzalendo kabisa, ubunge ni kwa faida yake, maana yuko pale kuhakikisha mambo yake ya kufilisi nchi yanaenda vizuri. Inawezekana jimbo lake analihudumia vizuri lakini hiyo ili abaki kuwa pale kwa ajili ya dili zake.
Hivi huyo mtu anayefikiri kuwa wananchi wanataka tu maji na shule ni nani na ana maana gani? Wakati wananchi wanategemea kusikia sera na sheria mpya zikiundwa na hizo zilizopo kukaribatiwa, wanategemea huyo mbunge achangie kuikaripia serekali inapokumbatia mafisadi na ufisadi eeh..........Hivi wewe GT ndo Rostam Aziz mwenyewe nini?
Unaongea utumbo kweli karibu mara zote. Hebu fikiria Bunge limekaa halafu watu wote wanakaa kimya kuna maana gani sasa ya kuwa na vikao vya Bunge? Au unaropoka tu. Hata kama si kuuliza swali basi achangie hoja za msingi za kuleta maendeleo. Yaani miaka 4 hata kufungua mdomo hakuna! Huyu jamaa yuko bungeni kwa maslahi yake binafsi tu wala hana shida na maendeleo ya wadanganyika. Yeye ni kwenda bungeni kutengeneza chanels zake za kuinyonya hii nchi tu basi. Rostam Aziz ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. He is too wicked I can say.
Ikumbukwe pia, maswali yanayosikika mengi yalishaulizwa siku nyingi na yakaonekana ni bora yaende bungeni.Kuna maswali yanayoulizwa na kupatiwa majibu bila kusikika bungeni. Ni vizuri pia ikajulikana bunge lipo wakati wote na si tu katika kipindi hiki wanachosikika!
True mkuu... may i also differ with on that one?? as you rightly said, kazi ya mbunge sio kuongea tu na sio lazima asikike... most of the effective wabunges are good in submitting their hojas kwa maandishi kwasababu ya collective resposibility na culture tuliojiwekea ya kuogopa kukosoana. on the other side, hakuna haja ya kusimama na kurudia kupongeza kwa sababu tu ya kuongea
Again, most of the effctive and influencial bunge decisions were not reached kwa vocals, watu wanawasilisha alternatively!!
Lastly, i still believe kwamba first task ya mbunge ni kuwakilisha jimbo lake
Kuhusu uwakilishi kwa jimboni anakotoka nakubaliana nako na napingana nako pia. Kuwakilisha ninakopingana nako ni kule kwa kung'ang'ania tu kuvutia kamba unakotoka. Uwakilishi wa namna hii hauwezi kulisaidia taifa na kila kitu kinakuwa into pieces badala ya kuwa kama one entity.Mathalan kuna sehemu huko kusini ktk pitapita yangu nilikutana na line kubwa tu ya umeme lakini nyumba zote za pembezoni hakuna hata nyumba inayotumia umeme..nilipoulizwa nikaambiwa.. aah mazee umeme uliletwa huku kisiasa na hamna mtu mwenye hela ya kuvuta umeme nyumbani kwake.. Ktk ishu kama hii ni kwamba TANESCO hapanshaka wamelamba garasa hapo na ndio maana kila siku wanalalamikia kupata hasara achilia mbali fedha ya kufidia mirija ya wafedhuli wengine. Kwa upande mwingine tunasikia kila siku makao makuu ya Kigoma Ujiji hakuna umeme wa gridi ya taifa....hapo ndipo unapoona matunda ya siasa ya kuvutia kamba unapotoka.
Nadhani ingekuwa vema wasifike kabisa bungeni mara baada ya kuwakilisha hojas zao kwa maandishi...!
Kila dakika 1 , i mean kila mshale wa saa unapozunguka kwa mbunge kuwepo pale Bungeni ni fedha ya mlala hoi inazunguka na kutumika..
why should those kind of NANA`S kuwa pale ?
Hivi huyo mtu anayefikiri kuwa wananchi wanataka tu maji na shule ni nani na ana maana gani? Wakati wananchi wanategemea kusikia sera na sheria mpya zikiundwa na hizo zilizopo kukaribatiwa, wanategemea huyo mbunge achangie kuikaripia serekali inapokumbatia mafisadi na ufisadi eeh..........
Alafu we ukae kimya eti wananchi wangu wamelizika na shule sijui maji... wakisema we ni fisadi itakuwaje
Well said mkuu... je wananchi wa kawaida wana upeo wa kugundua kuhusu ser makini za kitaifa? au wengi huchagua mbunge kutokana na ahadi za maendeleo kwa jimbo husika?
na kuna wengine hata hawachangii kwa maandishi, lakini huwazungumza moja kwa moja na mawaziri na mambo yao yananyooka kwenye miradi ya majimboni kwaoOk kuweka records vizuri, ikumbukwe kuwa bunge hukaa kwa kipindi maalumu na hakuna muda wa kutosha wa kila mbunge kuchangia kwa maana ya kupewa maiki kutoa chenga au mchele. Kunapokosekana muda basi wabunge mbalimbali huchangia kwa maandishi na wizara husika hutakiwa kuyafanyia kazi. Hivyo basi sio kila anayeonekana mkimya bungeni basi hajachangia wapo wengine huchangia kwa maandishi..mkitaka rekodi nendeni kwenye wizara husika watawaonesha rekodi za kila mbunge na hoja aliyoitoa.
Inawezekana wananchi wa Igunga wamelizika na hilo maendeleo jimboni ila uwakilishi wa kweli bungeni hakuna kwani hii imekaaje?Katika gazeti la Leo Jumapili la Mwananchi kuna Habari kwamba Mbunge wa Igunga Mr. Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali hata moja akiwa Bungeni, Lakini wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa pengine imechangiwa na ubusy alikuwa nao Mbunge huyo wa Igunga.
Kwa Mara nyingi yeye mwenyewe amekaririwa na baadhi na vyombo vya habari kuwa amekuwa yeye amefanya mambo makubwa sana katika Jimbo la Igunga Mjini Tabora.