Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Mbunge makini hupimwa pia kwa mafanikio au maendeleo ya jimboni kwake (miradi ya kijamii ) licha ya mchango wake katika Taifa kwa ujumla
 
Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.
Rostam hana sababu ya kubatuzana na serikali bungeni maana kaishika na anuwezo wa kuambia nje ya bunge nataka kitu hiki kiwe hivi na kinakuwa.
 
Ikumbukwe pia, maswali yanayosikika mengi yalishaulizwa siku nyingi na yakaonekana ni bora yaende bungeni.Kuna maswali yanayoulizwa na kupatiwa majibu bila kusikika bungeni. Ni vizuri pia ikajulikana bunge lipo wakati wote na si tu katika kipindi hiki wanachosikika!
 
Kimsingi mbunge kuwa bubu completely bungeni si jambo jema. Zaidi ya interests za jimbo lake pia mbunge anawajibu kutetea interests za taifa. Yapo mambo chungu nzima ya kitaifa ambayo hujadiliwa bungeni, mbunge mzalendo hataacha kutoa mchango wake ati kwa sababu jimboni kwake mambo mazuri.
Swala la Rostam kutokuchangia lolote liko wazi kabisa. Rostam si mzalendo kabisa, ubunge ni kwa faida yake, maana yuko pale kuhakikisha mambo yake ya kufilisi nchi yanaenda vizuri. Inawezekana jimbo lake analihudumia vizuri lakini hiyo ili abaki kuwa pale kwa ajili ya dili zake.
 
Niliwahi kusema kuhusu RA na Bungeni, sio tuu hajawahi kuchangia, bali kipindi anachohudhuria kikao cha Bunge, akikaa sana ni siku 3 tuu. Sijawahi kumuona zaidi ya siku 3 mfululizo. Yeye na mkono, huja Dodoma na ndege zao. ya Mkono huridi Dar kusubiri kuja kumchukua. Ya RA humsubiri hapo Airport ya Dodoma.

RA haulizi swali lolote kwa sababu matatizo yote ya wananchi wake anayamaliza mwenywe kwa fedha yake ya mfukoni.

Pia hachangii hoja yoyote kwa vile kichwani hamna kitu, hata ukimuona kwa macho tuu usoni, hilo utaliona wazi.

Kuna baadhi ya wabunge hawachangii lolote kwa sababu wamesusa baada ya kukatiwa ulaji. Ila pia kuna wasio changia kwa sababu hawaoni umuhimu wowote kuchangia japo vichwani wako fiti, lakini kuna hawa wasiochangia kwa vile vichwani hawana kitu, japo pesa wanazo.
Hivi kweli wananchi wakielimishwa kuhusu majukumu ya mwakilishi wao Bungeni, bado watawachagua mabubu?.


utamwona vipi wakati almost mwaka mzima ulikuwa kitandani?

Hivi kipimo cha ufanisi wa mbune n kuuliza maswali au kutekeleza yale ambayo wananchi waliompeleka bungeni wanayataka?

hebu tupumzishe, and i stupidly thought kuwa of all people wewe ungekuwa unaelewa zaidi ufanyakazi wa bungeni kuliko wengine humu ahh sasa tofauti yako na kubenea ni nini?
 
WAKATI tukielekea mwaka wa lala salama wa Bunge la mwaka 2005-2010, huku baadhi ya wabunge wakiibuka mashujaa kwa kutoa michango mizito inayoitingisha serikali, imebainika kuwa baadhi yao hadi sasa hawajawahi kuuliza hata swali moja wala kuchangia.


Uchunguzi huo umefanywa na Mwananchi Jumapili kwa msaada wa tovuti ya bunge ambako kila mchango wa mbunge hurekodiwa kwa kuonyesha swali la msingi au la nyongeza alilouliza, majibu yake na mchango aliotoa.


Kati ya wabunge 319 walioko katika Bunge la sasa ambao hawajawahi kuuliza maswali ya msingi wanakadiriwa kufikia 50 na wasiouliza maswali ya msingi wala nyongeza ni zaidi ya 30.


Mawaziri na wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa, hawajahusishwa kwenye hesabu hizo kwa sababu wapo upande wa serikali na wote wamekuwa hawaulizi maswali. Wengine ambao hawakuhusishwa kwenye vipengele hivyo ni Spika na Naibu Spika, lakini wote wameonyeshwa kuwahi kuchangia hoja mbalimbali.


Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.


Wabunge wengine ambao wameonyeshwa hawajawahi kuuliza maswali, lakini wamekuwa wakichangia hoja mbalimbali nao ni Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM); John Shibuda, Harith Mwapachu, Ali Haji Ali, Omar Sheha Musa, Abdallah Sumry, Gideon Cheyo, Juma N'hunga, Nazir Karamagi, Anna Abdalah, Ali Haji Ali, Thomas Mwang'onda, Salum Khamis Salum, Hassan Rajabu Khatibu na Felix Mrema.


Wengine ni Philemon Sarungi, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Abdisaalam Issa Khatib, Dk Ibrahim Msabaha, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale Mwiru, Salimu Yusufu Mohamed, Salum Ahamed Sadiq, Omar Sheha Mussa, Manju Msambya na Benedict Ole-Nangoro.


Wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa ufanisi wao wa kuchangia bungeni ni mdogo ni Abdul Aziz – Iringa (7); Dk James Msekela – Dodoma (6); Monica Mbega – Kilimanjaro (3); Dk Christine Ishengoma-Ruvuma (4) na William Lukuvi – Dar es Salaam (3). Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwahi kutoa michango bungeni mara mbili tu.


Katika Kundi la wabunge 13 wanaoongoza kwa kuuliza maswali ya msingi linaongozwa na Mgana Msindai (CCM) mwenye maswali 34 na kufuatiwa na William Shellukindo (29); Diana Chilolo (28), Paschal Degera (28), George Lubelege (25), Raphael Mwalyosi (24) na Mhoga Ruhwanya (23).


Wabunge wengine kwenye kundi hilo wana maswali 22 kila mmoja nao ni, James Msalika, Job Ndugai, Zitto Kabwe, Herbert Mtangi, Victor Mwambalaswa na Lucy Owenya.


Wabunge 11 vinara wa kuuliza maswali ya nyongeza ni Dk Wilbrod Slaa (71), Hamad Rashid Mohamed (71), Mgana Msindai (67), Esther Nyawazwa (58), George Lubelege (56), Diana Chilolo (54), Hafidh Ali Tahir (52), Geofrey Zambi (50) na wawili waliofungana kwa kuuliza 49, Jenista Mhagama na John Kilimba (49).


Katika kundi la kutoa michango mbalimbali kwenye vikao vya bunge linaongozwa na Naibu Spika Anne Makinda (495); akifuatiwa na Spika, Samweli Sita (494). Wengine ni Jenister Mhagama (193); Job Ndugai (147); Zitto Kabwe (125); Dk Slaa (106); Andrew Chenge (89); Suzan Lyimo (87); William Shelukindo (77); Geofrey Zambi (73); John Kilimba (69) na mawaziri wawili waliofungana kwa kufikisha michango 67 ambao ni Shamsa Mwangunga, Waziri wa Maliasili na Utalii na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa.


Mawaziri wengine wanaofuatia ni Dk Mary Nagu (64); Profesa David Mwakyusa (59); William Ngeleja (50); Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Johnson Mwanyika (47); Dk Makongoro Mahanga (45); Profesa Jumanne Maghembe (45); Stephen Wasira (41) na John Chiligati (40).


Akizungumzia kuhusu kumbukumbu hizo wiki iliyopita, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema kuwekwa kwa taarifa hizo hakuna maana zaidi ya kuweka kumbukumbu za michango ya wabunge, lakini akasema kulikuwa na marekebisho kwa wakati huo.


Alipotafutwa tena jana, alisema tovuti hiyo ya Bunge imefanyiwa marekebisho makubwa ili wananchi waweze kupata kwa undani kumbukumbu mbalimbali za vikao vya Bunge.


Pamoja na maboresho hayo, Dk Kashililah alisema: "Tuna mpango wa kuongeza maboresho zaidi yakiwepo ya kuwezesha watu kufuatilia vikao vya Bunge kupitia tovuti hiyo."


Licha ya baadhi ya wabunge kuwa na mchango hafifu, Bunge la sasa limeonekana kuwa mwiba mkali kwa viongozi serikalini hususan mawaziri, kutokana na baadhi ya wabunge kuwabana katika mambo mbalimbali ya utendaji mbovu na ufisadi, huku kufupishwa kwake kukipunguza nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia kwa baadhi yao ambao walikuwa hawajafanya hivyo.


Katika kipindi hicho miongoni mwa hoja nyingine zilizosisimua ni mjadala wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe kuhusu utoaji wa zabuni ya umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond Development Limited (LLC); na kusababisha Rais Jakaya Kikwete kuvunja baraza la mawaziri baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu pamoja na mawaziri wengine wawili.
 
RA is better than 75% ya hao wanaochangia!

Maendeleo angalau yanaonekana jimboni mwake, mengine anayaleta yeye mwenyewe.

Hivi ukiulizwa Mwapachu na RA nani mbunge mzuri utamtaja Mwapachu?

baniani mbaya.....
 
Hivi kuongea bungeni ni kufanya kazi au suala liko jimboni kwako ambao yale uliyoahidi unayatekeleza?
 
Kimsingi mbunge kuwa bubu completely bungeni si jambo jema. Zaidi ya interests za jimbo lake pia mbunge anawajibu kutetea interests za taifa. Yapo mambo chungu nzima ya kitaifa ambayo hujadiliwa bungeni, mbunge mzalendo hataacha kutoa mchango wake ati kwa sababu jimboni kwake mambo mazuri.
Swala la Rostam kutokuchangia lolote liko wazi kabisa. Rostam si mzalendo kabisa, ubunge ni kwa faida yake, maana yuko pale kuhakikisha mambo yake ya kufilisi nchi yanaenda vizuri. Inawezekana jimbo lake analihudumia vizuri lakini hiyo ili abaki kuwa pale kwa ajili ya dili zake.

I strongly agree with you mkuu. Soma hata sahihi yangu hapa chini. Rostam si mzalendo ni jizi tu la maliasili zetu. Kama anatumia pesa zake kuleta maendeleo jimboni kwake, hakuna tofauti na panya anayekuuma huku akikupulizia.
 
Hivi wewe GT ndo Rostam Aziz mwenyewe nini?

Unaongea utumbo kweli karibu mara zote. Hebu fikiria Bunge limekaa halafu watu wote wanakaa kimya kuna maana gani sasa ya kuwa na vikao vya Bunge? Au unaropoka tu. Hata kama si kuuliza swali basi achangie hoja za msingi za kuleta maendeleo. Yaani miaka 4 hata kufungua mdomo hakuna! Huyu jamaa yuko bungeni kwa maslahi yake binafsi tu wala hana shida na maendeleo ya wadanganyika. Yeye ni kwenda bungeni kutengeneza chanels zake za kuinyonya hii nchi tu basi. Rostam Aziz ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. He is too wicked I can say.
Hivi huyo mtu anayefikiri kuwa wananchi wanataka tu maji na shule ni nani na ana maana gani? Wakati wananchi wanategemea kusikia sera na sheria mpya zikiundwa na hizo zilizopo kukaribatiwa, wanategemea huyo mbunge achangie kuikaripia serekali inapokumbatia mafisadi na ufisadi eeh..........
Alafu we ukae kimya eti wananchi wangu wamelizika na shule sijui maji... wakisema we ni fisadi itakuwaje
 
Ikumbukwe pia, maswali yanayosikika mengi yalishaulizwa siku nyingi na yakaonekana ni bora yaende bungeni.Kuna maswali yanayoulizwa na kupatiwa majibu bila kusikika bungeni. Ni vizuri pia ikajulikana bunge lipo wakati wote na si tu katika kipindi hiki wanachosikika!

kwa hiyo hao wasiosikka wanaulizaga wakiwa nje ya bunge?
 
True mkuu... may i also differ with on that one?? as you rightly said, kazi ya mbunge sio kuongea tu na sio lazima asikike... most of the effective wabunges are good in submitting their hojas kwa maandishi kwasababu ya collective resposibility na culture tuliojiwekea ya kuogopa kukosoana. on the other side, hakuna haja ya kusimama na kurudia kupongeza kwa sababu tu ya kuongea

Again, most of the effctive and influencial bunge decisions were not reached kwa vocals, watu wanawasilisha alternatively!!

Lastly, i still believe kwamba first task ya mbunge ni kuwakilisha jimbo lake



Nadhani ingekuwa vema wasifike kabisa bungeni mara baada ya kuwakilisha hojas zao kwa maandishi...!

Kila dakika 1 , i mean kila mshale wa saa unapozunguka kwa mbunge kuwepo pale Bungeni ni fedha ya mlala hoi inazunguka na kutumika..


why should those kind of NANA`S kuwa pale ?
 
Kuhusu uwakilishi kwa jimboni anakotoka nakubaliana nako na napingana nako pia. Kuwakilisha ninakopingana nako ni kule kwa kung'ang'ania tu kuvutia kamba unakotoka. Uwakilishi wa namna hii hauwezi kulisaidia taifa na kila kitu kinakuwa into pieces badala ya kuwa kama one entity.Mathalan kuna sehemu huko kusini ktk pitapita yangu nilikutana na line kubwa tu ya umeme lakini nyumba zote za pembezoni hakuna hata nyumba inayotumia umeme..nilipoulizwa nikaambiwa.. aah mazee umeme uliletwa huku kisiasa na hamna mtu mwenye hela ya kuvuta umeme nyumbani kwake.. Ktk ishu kama hii ni kwamba TANESCO hapanshaka wamelamba garasa hapo na ndio maana kila siku wanalalamikia kupata hasara achilia mbali fedha ya kufidia mirija ya wafedhuli wengine. Kwa upande mwingine tunasikia kila siku makao makuu ya Kigoma Ujiji hakuna umeme wa gridi ya taifa....hapo ndipo unapoona matunda ya siasa ya kuvutia kamba unapotoka.

Mkuu hapo tuko pamoja mia kwa mia... they need to have a bigger picture of their role... sadly, most of them dont realise or dont have that wisdom of knowing their scope of work is beyond their constituencies
 
Nadhani ingekuwa vema wasifike kabisa bungeni mara baada ya kuwakilisha hojas zao kwa maandishi...!

Kila dakika 1 , i mean kila mshale wa saa unapozunguka kwa mbunge kuwepo pale Bungeni ni fedha ya mlala hoi inazunguka na kutumika..


why should those kind of NANA`S kuwa pale ?

Thanks, i agree with you but i do also wish to say that most effective decisions sometimes made or outcomes achieved are not necessarily made when one is working in the office... Tatizo kubwa ni jinsi walivyo money driven in most of cases... na hilo nia tatizo la kitaifa, we jaribu kumuita DMO kwenye kikao cha kutathmini kazi yake utaona anavyokuwa kama hakuna colours
 
Hivi huyo mtu anayefikiri kuwa wananchi wanataka tu maji na shule ni nani na ana maana gani? Wakati wananchi wanategemea kusikia sera na sheria mpya zikiundwa na hizo zilizopo kukaribatiwa, wanategemea huyo mbunge achangie kuikaripia serekali inapokumbatia mafisadi na ufisadi eeh..........
Alafu we ukae kimya eti wananchi wangu wamelizika na shule sijui maji... wakisema we ni fisadi itakuwaje

Well said mkuu... je wananchi wa kawaida wana upeo wa kugundua kuhusu ser makini za kitaifa? au wengi huchagua mbunge kutokana na ahadi za maendeleo kwa jimbo husika?
 
Well said mkuu... je wananchi wa kawaida wana upeo wa kugundua kuhusu ser makini za kitaifa? au wengi huchagua mbunge kutokana na ahadi za maendeleo kwa jimbo husika?


Mkuu this time mbunge wangu akijitokeza tena kujaribu kuwashawishi wananchi pale jimboni kwetu nitajaribu kumwaibisha , Wajua kale kamtindo ka ahadi / sera feki wengi wao wanakatumia sana,

Nilishangaa mwezi december hata pale mjini, makao makuu ya Wilaya penyewe barabara haifai ndugu yangu , mashimo barabara nzima ni mahandaki mkuu..! Kwa wale wenye vigari vidogo ni usumbufu kabisa.

Nitaanza na Halmashauri ya mji kisha nifike Idara ya Ujenzi , Baada ya hapo nadhani mbunge atakuwa na hali mbaya sana sana kwa awamu ijayo .

Kwanini tuwe na Mbunge ambaye kazi zake ni kuja kuomba kura tu, na akisha pata haonekani kabisa jimboni kwake. Tukiuliza twaambiwa yupo Dar es salaam ndipo ofisi yake ilipo. !!!!
 
Ok kuweka records vizuri, ikumbukwe kuwa bunge hukaa kwa kipindi maalumu na hakuna muda wa kutosha wa kila mbunge kuchangia kwa maana ya kupewa maiki kutoa chenga au mchele. Kunapokosekana muda basi wabunge mbalimbali huchangia kwa maandishi na wizara husika hutakiwa kuyafanyia kazi. Hivyo basi sio kila anayeonekana mkimya bungeni basi hajachangia wapo wengine huchangia kwa maandishi..mkitaka rekodi nendeni kwenye wizara husika watawaonesha rekodi za kila mbunge na hoja aliyoitoa.
na kuna wengine hata hawachangii kwa maandishi, lakini huwazungumza moja kwa moja na mawaziri na mambo yao yananyooka kwenye miradi ya majimboni kwao
 
Katika gazeti la Leo Jumapili la Mwananchi kuna Habari kwamba Mbunge wa Igunga Mr. Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali hata moja akiwa Bungeni, Lakini wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa pengine imechangiwa na ubusy alikuwa nao Mbunge huyo wa Igunga.

Kwa Mara nyingi yeye mwenyewe amekaririwa na baadhi na vyombo vya habari kuwa amekuwa yeye amefanya mambo makubwa sana katika Jimbo la Igunga Mjini Tabora.
 
Katika gazeti la Leo Jumapili la Mwananchi kuna Habari kwamba Mbunge wa Igunga Mr. Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali hata moja akiwa Bungeni, Lakini wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa pengine imechangiwa na ubusy alikuwa nao Mbunge huyo wa Igunga.

Kwa Mara nyingi yeye mwenyewe amekaririwa na baadhi na vyombo vya habari kuwa amekuwa yeye amefanya mambo makubwa sana katika Jimbo la Igunga Mjini Tabora.
Inawezekana wananchi wa Igunga wamelizika na hilo maendeleo jimboni ila uwakilishi wa kweli bungeni hakuna kwani hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom